Ukienda kwa duka na unaambiwa uchague biscuit moja tu, unaisoma packet yote kwanza. Hiyo decision ilikuwa na pressure kuliko kuchagua course ya university 😂🍪
Kuna ile siku unachora picha ya family kwa art class. Kila mtu anakuwa na kichwa kubwa, miguu kama toothpick, lakini unaipresent kwa confidence ya Picasso 😂🎨
Kuna vile ulikuwa unaenda kununua mkate na unakutana na mbwa njiani. Ghafla route ya dakika mbili inakuwa mission ya kijeshi. Unangoja mbwa aingie kwa gate ndio upite 😂😭
Kuna vile unakaa na watu wazima wakiongea kuhusu mambo ya zamani. Ukisikia jina la mtu unamjua, unaanza kusikiliza kwa makini kama documentary imeanza 😂👀