Mnataka kufunika uhalifu wa kiwango hiki?
Mnataka mauaji ya kutisha kama haya niliyoona kwenye video yanyamaziwe?
Nani alietoa amri kuua watu wengi kiasi hiki?
Ukiacha mauaji ya kwenye vita,
sijaona mauaji ya kisiasa makubwa kiasi hiki.
Hata makaburu hawakuua watu wengi kwa pamoja kiasi hiki..
Je hawa wauaji ni Watanzania wenzetu?
Watu walioingia na kukuta watu wanaangalia mpira na wakawaua wote kama kuku.
Hili halitaweza kufunikwa, lazima watu wawajibike
Pale SAUT-Mtwara, kuna faza mmoja aliitwa Faza Mbano, alikuwa akifundisha Course inaitwa Fundamental Ethics,
Jambo moja nakumbuka kuishi nalo hadi leo na limekuwa msaada kwenye maisha yangu, kuna module inaitwa CONSCIENCE (Dhamiri), Alidai, Dhamiri ni MHAKAMA kuu ya mwisho duniani.
Dhamiri haipokei rushwa na haitoi rushwa, ni kipimo cha mwisho cha maadili na ukweli.
Kama wewe ni mshenzi lakini wasiojua wanakuona mwema, basi Dhamiri comes In na inakwambia black and while kwamba wewe ni MSHENZI, 😀🙌
Na kama wewe ni MWEMA kabisa na huna hatia lakini watu wanakupakaza mabaya, Dhamiri comes In na inakwambia kabisa kwamba wewe ni mtu MWEMA.
Faza Mbano alisema, “Dhamiri hukushangilia pale wengine wote wanapokuwa kinyume, lakini Dhamiri hukutukana pale wengine wote wanapokushangilia kwa sababu Dhamiri ndiyo hakimu wa kweli kwenye maisha ya wanadamu��
Lakini Ogopa kabisa mtu ambaye dhamiri yake ni mfu alimaliza Faza Mbano.
Nimetoka Ukonga kumuona Mwenyekiti, Yuko imara na anawasalimia wote.
Anatoa pole kwa Watanzania wote waliopoteza maisha, familia ndugu na marafiki.
Anatambua watu waliopoteza viungo na kubaki na ulemavu.
Ametoa pole kwa wote waliopoteza mali pia.
Damu ya wenzetu haijamwagika bure na hakuna atakaefunika jambo hili bila uwajibikaji.
Msimamo wa Mwenyekiti uko thabiti, Yuko imara na mwenye afya njema.
HIZI NDIYO TAFAKARI ZA KITUME .
Mababa Askofu TEC watoa tafakari ya hapa tulipo na tunatokaje.Hawa ndiyo Wachungaji wa kondoo.Tujihadhari sana na wala Kondoo.
Hawa ndio vijana wa CHADEMA ambao wanawindwa usiku kucha kuuliwa.
Sikiliza kwa makini nondo HIZO, Maswali KONKI haya hayawezi kujibiwa na MACHAWA. Ndiomaana watawala wanaona bora watuue wabaki na CHAWA wazee wa PONGEZI.
HATUTAKUBALI, TUTAENDELEA KUHOJI KILA SIKU MPAKA TUTAKAPOSIKILIZWA NA KUIPATA TANGANYIKA YETU.
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵😎
Anaandika Askofu Bagonza (NB: HII NI PHD INAONGEA SOMA KWA MAKINI).
Mimi ngoja niwaunge mkono BAKWATA kuhusu hoja yao ya AMANI ni bora kuliko HAKI halafu niwaulize.
- Kwa miaka 60 tuna amani na tunaitwa Kisiwa cha amani. Kwa hiyo amani ilikuwepo, je haki ilikuja?
- Wanasema haki ni mchakato. Nakubali. Wamekuwa na miaka 60 ya amani bila mchakato wa haki. Wanataka miaka mingapi ili wachakate na kuleta haki?
- Huo ufundi wa kutenganisha Haki na Amani wameupata wapi tuutafute maana mitume wote na manabii waliukosa?!
Zaburi 85
10 : Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana.
Mithali 14
34 : Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.
Isaya 32
17 : Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
Anaandika Askofu Bagonza
Mimi ngoja niwaunge mkono BAKWATA kuhusu hoja yao ya AMANI ni bora kuliko HAKI halafu niwaulize.
- Kwa miaka 60 tuna amani na tunaitwa Kisiwa cha amani. Kwa hiyo amani ilikuwepo, je haki ilikuja?
- Wanasema haki ni mchakato. Nakubali. Wamekuwa na miaka 60 ya amani bila mchakato wa haki. Wanataka miaka mingapi ili wachakate na kuleta haki?
- Huo ufundi wa kutenganisha Haki na Amani wameupata wapi tuutafute maana mitume wote na manabii waliukosa?!
Zaburi 85
10 : Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana.
Mithali 14
34 : Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.
Isaya 32
17 : Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
VIDEO:
Watanzania wameshauriwa kuendelea kutuma taarifa za ushahidi zinazoonesha namna matukio ya ukatili yalivyofanyika nchini kabla, wakati na baada ya 'maandamano' ya Oktoba 29.2025 (Siku ya Uchaguzi Mkuu) kwa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), matukio ambayo yamesababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali kwenye maeneo mbalimbali nchini
Wakili Dickson Matata amewaeleza Wanahabari leo, Jumanne Novemba 11.2025, kuwa licha ya kwamba chama hicho kwa sasa kimejikita kutoa msaada wa kisheria kwa watu walioshikiliwa kwenye Vituo vya Polisi na wale waliofikishwa Mahakamani na kusomewa kesi tofauti ikiwemo uhaini na unyang'anyi wa kutumia silaha, lakini pia linaendelea kupokea taarifa nyingine za matukio hayo kwa ajili ya kuzichakata na kuchukua hatua stahiki.
BREAKING NEWS.🚨
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, anataka kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji na ukiukwaji wa haki unaohusishwa na uchaguzi wa Tanzania wa Oktoba 29.
WANANGU KUMEANZA KUCHANGAMKA.
REPOST 500
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
VIDEO:
Leo Novemba 11, 2025, Kanisa Kuu la Moyo Safi wa Bikira Maria, Jimbo Katoliki Bagamoyo, limeadhimisha Misa Takatifu ya kuwaombea waliouwawa na waliojeruhiwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2025, ibada iliyoongozwa na Askofu Stephano Lameck Musomba O.S.A.
Katika mahubiri yake, Askofu Musomba alisema misa hiyo imeadhimishwa kwa nia za kuwaombea waliopoteza maisha, kuwaombea waliojeruhiwa na wanaendelea kuteseka, pamoja na kuombea haki na amani nchini.
“Tunaadhimisha misa hii nia zetu tatu, kwanza tunawaombea waliouawa wakati wa uchaguzi mkuu. Tunasema waliuawa kwa sababu watu hawa hawakuumwa, walipigwa risasi. Tunawaombea waliojeruhi na wapo katika maumivu makali, Mungu awape wepesi waweze kupona. Tunaombea haki na amani katika nchi yetu,” alisema Askofu Musomba.
Aidha, Askofu Musomba amesisitiza umuhimu wa kulinda utu wa binadamu na kuheshimu haki za kila mmoja, akilaani vikali matukio ya vurugu na vifo vya raia.
“Binadamu ana haki zake. Palipo na haki pana furaha, umoja, uelewano na undugu. Wale waliolenga risasi ni nani hao? Waliouawa sisi ni ndugu zao, tunalia. Tunaomboleza. Mwanadamu siyo mnyama wa kawaida kama nguruwe kwamba utasema nipate kitoweo, unapata faida ipi?” alihoji.