Mungu aliyekuokoa na risasi 32 za mfulilizo ndiye huyo anaendelea kukulinda kwenye kuta cha Magereza . Stay strong ๐ช umeonyesha maana harisi ya "UPINZANI"
Really politician #FreeTunduLissu#KatibaMpya
Katika siasa za ndani ya na nje ya chama chetu, FAM sitomsamehe kwa namna yeyote, alituuza sana.
Ilikuwaje siku hii akampa tuzo Samia?
FAM ndiyo Chanzo cha Lissu kusota Gerezani
FAM ndiyo chanzo cha Chadema kushitakiwa na kusumbuliwa na msajili.
๐๐๐
Karibuni katika SHOW ZA TL.
1.Leo patakuwa na uamuzi mdogo kutoka kwa Jopo la Majaji kuhusu pingamizi (Objection) lililowekwa na Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu juu ya Shahidi kutoa ushahidi wake akiwa katika kibox (kizimba) kilichozibwa bila majaji Kumuona Shahidi,bila mtuhumiwa Kumuona Shahidi na bila Wahudhuriaji Kumuona Shahidi.
Kwa mujibu wa maelezo ya Tundu Lissu ushahidi wa namna hiyo ni ushahidi wa watuwasiojulikana na ni ushahidi wa gizani.
2.Leo tena hapo hapo Mahakama Kuu patakuwa na kesi ya madai dhidi ya CHADEMA, kesi namba 8323 ya nwaka 2025 Saidi Issa Mohammed na wenzake wawili katika ukumbi mwingine mbele ya Jaji Mwanga.
N.B
Tunapitishwa katika moto mkali lakini tutashinda.
@IAMartin_@JamesMbowe4 Tarehe 21/01/2025 watu hatukulala mlidhani tulikesha bure? Ilikuwa siku yenye kubadili historia ya nchi yetu. Hii tarehe ndo ilitoa mwanga wa chama cha upinzani kuwa chini ya wananchi wenyewe na kuondoa mapandikizi ya chama dola. Wajumbe wa CDM walifanya maamuzi ya kihistoria.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 152
Anaendelea Mhe. Lissu.
Tuna haki yakutembelewa, waheshimiwa Majaji kuna masharti kwenye hiyo kanuni ikiwemo sharti la kutembelewa na mfungwa mwenzako, sharti lingine ni askari magereza wakuone na kukusikiliza ila kwa Mawakili kanuni haisemi hivyo.
Waheshimiwa Majaji tangu tarehe 10/04/2025 mpaka 12/11/2025 nilikuwa natembelewa bila tatizo.
Na ndugu, familia, marafiki na Mimi ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, walikuwa wananitembelea wana Chadema
Tanzania nzima.
Niliitwa kwa Bwana Jela nikaambiwa ni marufu kwa viongozi na wanaChadema kukutembelea Gerezani.
Chadema ni Chama halali na sio kosa kwa wanaChadema na viongozi wenzangu kunitembelea lakini kuanzia Tar. 12/11/2025 hawajaruhusiwa.
Maafisa magereza ni maafisa wa umma so yale magereza sio mali zao binafsi.
Hawana mamlaka ya kubagua nani aje gerezani nani asije. Katiba inasema usibague watu kwa mtizamo wao wa kisiasa, dini au kabila na hili vilevile naomba niwaeleze mlifahamu kuhusu violation ya haki ya Mfungwa kutembelewa.
Waheshimiwa Majaji sasa naomba swala la tatu niliseme.
Linahusu uendeshaji wa kesi hii. Na naomba niweke wazi kuwa siwalaumu kwa chochote nitakachosema hapa. Na hiki nitakachosema siwalaumu mawakili wa serikali na nyie majaji.
Haki zangu zimekiukwa sio kwa kosa lenu wala la Mawakili wa Serikali.
Waheshimiwa Majaji leo hii ni siku ya 307 tangu niwekwe mahabusu.
Miezi 10 week 44 niko mahabusu. Waheshimiwa majaji katika siku zote hizi kesi hii imesikilizwa kwa siku 14 tu na leo ni siku ya 15 kesi hii inasikilizwa katika siku 307.
Kuna siku 88 ambazo kesi haijasikilizwa kabisa, niko gerezani hakuna kinachoendelea.
Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokiukwa. Justice delayed is justice denied.
Na Katiba yetu inaelekeza Mahakama ziendeshe mashauri kwa namna ambayo haitachelewesha Haki. Ibara ya 147 ya Katiba inasema.
Kifungu cha 5 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinasema mashauri yanaendeshwe kwa haraka.
Tatizo lipo kwenye utaratibu wa session ndio tatizo na hilo ni tatizo la wanaoamua kesi iendeshe kwa njia ya session.
Naomba niwasomee kilichosemwa na Tume ya Haki jinai kuhusu kuendesha mashauri ya jinai kwenye ripoti ya July 2023, ukurasa wa 17 na 18 unasema kuhusu vikao vya mahakama kuu (high court session) tume inasema uendeshaji wa mashauri kwa njia ya vikao huchelewesha mashauri hayo.
Kati ya mashauri 2000 ni mashauri 700 tu ndio yalisikilizwa pekee kwa mtindo wa session.
Hivyo basi uendeshaji wa kesi kwa kutumia session unaamuriwa na Jaji Mkuu zikiisha siku tunasubiri aseme tena ndo maana zimepita siku 88 bila kesi hii kuendelea hadi atakapopanga tena huyo Jaji Mkuu.
Ucheleweshaji huu sio kosa lenu wala mawakili wa Serikali ni kosa la utaratibu tulionao.
Je huu utaratibu wa session uko wapi kwenye CPA ambayo ni sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Leo hapa High Court Dar es salaam kuna majaji wakutosha lakini ili kesi yangu isikilizwe lazima Jaji atoke Songea, mwingine Mtwara sijui na lazima walipwe, Usafiri, Chakula na kila kitu.
Usipowalipa kesi haiendelei na mimi mtuhumiwa nateseka huko jela. Walishindwa nini kuwapangia majaji wa hapa ili kesi isikilizwe kila siku.
Zamani majaji walikuwa wachache sana lakini siku hizi kila mkoa kuna majaji. Nashangaaa mambo haya kwa utaratibu huu sasa.
Jaji anasema soma kifungu cha 185 na anakisoma hapa kinasema Mahakama inamamlaka ya ku conduct seatings.
Mhe. Lissu anasema kuna tofauti kati ya seatings na sessions.
Kwahiyo kwenye hili ni tofauti na ku conduct seatings. Mahakama kuu zote zinakaa kusikiliza kesi hizo ni seatings zote.
Mimi nasema utaratibu wa sessions ni mbaya zaidi kwa kesi kama ya Uhaini.
Jaji ameleta kifungu namna Lissu alivyolitafsiri ameishia kusema hebu tuendeleee basi mshitakiwa ๐๐๐
Kosa la Uhaini ni Sue Generis sio sawa na wizi wa kuku, ujambazi na makosa mengine.
Part 153 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.