Wakati wa maadhimisho ya miaka 250 ya Uhuru wa Marekani (#Freedom250), Brigedia Jenerali Hargens wa Jeshi la Walinzi wa Taifa la Nebraska alimkabidhi Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Salum Haji Othman, bendera ya Marekani iliyopandishwa katika Jengo la Bunge la Marekani wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 250 wa uhuru wa Marekani.
CDA Lentz aliishukuru JWTZ kwa dhamira yake ya dhati ya kuimarisha usalama wa kikanda na kwa ushirikiano thabiti kati ya mataifa yetu mawili, tunapoendelea kufanya kazi pamoja kuendeleza amani, usalama, na ustawi kwa wananchi wetu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres, na kusisitiza dhamira ya Tanzania ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, amani na maendeleo endelevu.
Baada ya mazungumzo yao, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) alimkabidhi Mhe. António Guterres zawadi ya kitabu kuhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutambua kuvutiwa kwa muda mrefu kwa Katibu Mkuu huyo na maono, uongozi na mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuhimiza amani, maendeleo na ushirikiano wa kimataifa.
Ujenzi wa Mtambo wa Kisasa wa Kuchakata Maji Taka wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
Utekelezaji wake umefika asilimia 70 ambapo mradi ukikamilika katika awamu ya kwanza utakuwa na uwezo wa kuchakata maji taka yenye ujazo wa mita za ujazo 16,000 kwa siku kwa kuhudumia maeneo ya Mbezi Beach na Kawe.
Mradi utaongezewa uwezo wa kuchakata maji taka hadi kufikia mita za ujazo elfu 22 kwa siku ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya huduma za usafi wa mazingira katika maeneo hayo.
Wizara ya Fedha imependekeza kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa vifaa vya umeme vinavyotumika kwenye magari. Hatua hii inalenga kupunguza gharama za upatikanaji wa vifaa hivyo na kuongeza matumizi yake nchini.
Aidha, msamaha huo unapendekezwa pia kwa vipuri vya mifumo ya gesi vinavyotumika kwenye magari. Lengo ni kutoa unafuu kwa watumiaji, kupunguza gharama za matengenezo na matumizi ya magari yanayotumia gesi, pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala hapa nchini.
Waziri wa Fedha, Khamis Mussa Omar, ameliambia Bunge kuwa Serikali imependekeza kupunguza tozo na gharama mbalimbali kwa wazalishaji wa maudhui mitandaoni. Hatua hiyo inalenga kupunguza mzigo kwa sekta hiyo na kuimarisha mazingira ya biashara ya kidigitali.
Serikali imesema kuwa uamuzi huo unatarajiwa kuwapa fursa zaidi vijana kujiajiri kupitia utengenezaji wa maudhui ya mtandaoni, pamoja na kukuza ajira mpya zinazotokana na sekta ya ubunifu na teknolojia ya kidigitali nchini.
Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam wameshiriki Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Singapore, lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Jukwaa hilo limewakutanisha viongozi wa Serikali, wafanyabiashara, wawekezaji na taasisi mbalimbali za kifedha kutoka Tanzania na Singapore kwa lengo la kuimarisha biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika kuwawezesha vijana katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na elimu ya ujasiriamali.
Amesema serikali imejikita pia katika kukuza uchumi wa kidijitali ili kuongeza ushiriki wa vijana katika mageuzi ya teknolojia na maendeleo ya kisasa.
Aidha, Rais Samia amesema Tanzania imejipanga kuimarisha mageuzi ya kidijitali pamoja na matumizi ya majukwaa ya kidijitali kwa lengo la kukuza uchumi wa kisasa katika kipindi cha miaka ijayo.
Ameongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza fursa za ajira na ubunifu kwa vijana katika sekta ya teknolojia na uchumi wa kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimpokea rasmi Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam, aliyewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa, tarehe 9 Juni, 2026, Ikulu Dar es Salaam