Brand za magari ya umeme na yanayotumia mafuta zinazozalishwa China zimeingia kwa kasi katika soko la Tanzania. Kampuni kama BYD, Chery, Geely, na Changan ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa magari duniani, zikiwa na teknolojia ya kisasa, viwango bora vya usalama, na uwezo mkubwa wa uzalishaji.
Hii inaleta fursa ya kipekee kwa Tanzania kuacha taratibu kuwa dampo, au kwa lugha ngumu zaidi kuwa kaburi la magari ya mtumba ambayo katika masoko ya nje tayari hayana road worthiness, yanatumia teknolojia zilizopitwa na wakati, na yana viwango duni vya usalama. Badala yake, nchi inaweza kuelekea katika matumizi ya magari mapya, salama, na rafiki kwa mazingira.
Ninashauri Serikali izingatie sera ya kupunguza au kuondoa kodi kwa magari ya umeme, na kupunguza kodi kwa magari mapya yanayotumia umeme na mafuta hadi isizidi asilimia 20 ya bei ya gari. Hatua hii itawezesha Watanzania wengi zaidi kumiliki magari mapya yenye teknolojia ya kisasa, viwango bora vya usalama, na matumizi madogo ya nishati au uchafuzi wa mazingira.
Kwa mazingira ya uchumi wa Tanzania, ambapo car financing bado si rahisi kufikiwa na wananchi wengi na manunuzi hufanyika kwa mfumo wa malipo ya papo kwa papo (upfront payment), punguzo la kodi litapunguza mzigo mkubwa wa bei kwa mnunuzi wa mwisho. Hii italeta unafuu wa moja kwa moja kwa wananchi katika ununuzi wa magari.
Sera kama hii itakuwa na manufaa kwa pande zote. Itawanufaisha wananchi kwa kupata magari salama na ya kisasa, itaongeza mapato ya serikali kupitia ongezeko la mauzo badala ya kutegemea kodi kubwa kwa idadi ndogo ya magari, na italinda mazingira kwa kupunguza uchafuzi unaotokana na magari chakavu.
Zaidi ya hapo, itavutia makampuni mengi zaidi kuanzisha dealership rasmi nchini na hata kuwekeza katika viwanda vya kuunganisha magari (assembly plants), jambo litakaloongeza ajira, ujuzi wa ndani, na mapato ya viwanda.
Pendekezo hili linaweza kuwa sehemu ya mabadiliko ya sera yanayochochewa kupitia maeneo maalumu ya kiuchumi (special economic zones) chini ya TISEZA @InvestTanzania, ili Tanzania iwe kitovu cha magari mapya na teknolojia safi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Tusikubali kuwa wa mwisho kwenye masuala ya kisera na kimabadiliko katika ukanda wetu, kwani tuna fursa ya kipekee kuwa wa kwanza na kuongoza
Still Okay To Date ni filamu kali ya Kitanzania iliyobeba hadithi nzuri ya penzi linaloingia ukakasi baada ya vitu kufichuka!
Ukitaza filamu hii utakubali kuwa sasa Tanzania imepiga hatua kubwa sana kwenye kusogeza kurudumua la Tasnia ya Filamu Tazama filamu hii Jumamosi saa 9