“70% of public climate finance to developing countries was in the form of loans and only 30% has been offered as grants
Developing countries are paying more back to wealthy nations for climate finance loans than they receive” David Abudho, Oxfam in Africa Climate Justice Lead
Read the full report co-authored with @CARE : https://t.co/bg7xXgqvec
#COP30 #MakeRichPollutersPay
Results of the Online Donor Feedback Survey:
🔗: https://t.co/RTC21NgnmB
• 33% say that email is the communication tool most likely to inspire them to give.
• 46% have given a tribute gift within the past 12 months.
• 36% have donated to a nonprofit by using a QR Code.
Every woman deserves the right to make choices about her body without stigma, discrimination, or fear. Access to safe abortion saves lives and ensures equality.
#Justice4Her#DefendThePromise
Care Over Criminization
Mtaalamu wa masuala ya uzazi, familia na malezi Dkt. Katanta Simwanza amesema matumizi ya dawa za kulevya kwa wanawake kama sehemu ya kukata Hedhi, yanaweza kuathiri tezi za Hypothalamus na Pituitary zinazopatikana katika ubongo ambazo ni muhimu katika udhibiti wa homoni ikiwemo zinazohusu mzunguko wa hedhi.
"Homoni zinazohusika na mzunguko wa hedhi ni pamoja na estrogeni na progesteroni ambazo huhitajika ili kudumisha mzunguko wa hedhi wa kawaida, dawa za kulevya zinaweza kuvuruga uzalishaji wa homoni hizi na kusababisha mzunguko wa hedhi kutokuwa wa kawaida ama kutokuwepo kabisa." Amesema Dkt. Simwanza.
Kauli ya Dkt. Simwanza imekuja baada ya uwepo wa taarifa za baadhi ya wanawake wanaotumia dawa za kulevya kukata hedhi ambapo mfamasia mkuu kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzania Bi. Upendo Chenya amesema matumizi ya dawa kama bangi, Cocaine na Heroine huwa na athari moja kwa moja kwenye uzazi.
"Baadhi ya wanawake hasa wanaofanya biashara ya kuuza miili ya hutumia dawa hizo ili kukata hedhi, jambo hilo ni hatari kwani linaenda kusababisha changamoto katika mfumo wa uzazi." Amesema Upendo wakati wa mdahalo wa kitaifa ulioandaliwa na taasisi ya Msichana Initiative kuhusu masuala ya hedhi salama uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Dkt. Isaya Mhando, Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi ameeleza kuwa mchakato wa hedhi huanzia kwenye ubongo, hivyo ukiathirika husababisha hata mzunguko wa hedhi kuvurugika, akisema mfumo huo ulivurugika husababisha changamoto ya upatikanaji wa mimba.
Matumizi ya dawa za kulevya pia kulingana na Dkt. Isaya husababisha matatizo ya ugumba kutokana na ubora wa mayai na mfumo wa uzazi kuharibika, akionya kuwa ni hatari kwa matumizi ya dawa hizo kwa wanawake.