Bwana Chalamila, Mimi nimehudumu kwenye kamati ya Nishati na madini ya bunge kwa miaka mitano.
Najua utaratibu wa uagizaji wa mafuta kama ninavyojua kiganja cha mkono wangu.
BPS imeundwa nikiwa mbunge nimeshiriki .
Mnatakiwa kujibu maswali rahisi nyie watetezi mafisadi na Cartels.
1. Mafuta yanatumia siku ngapi kuanzia kununua mpaka yanafika Dar?
2. Mgogoro umeanza tarehe 28/2/2026, mafuta hutumia siku 50 mpaka 60 kufika bandari yetu ya Dar, hivyo mafuta yaliyonunuliwa baada ya mgogoro kuanza na bei kuanza bado hayajaingia nchini.
Kwanini mafuta yaliyonunuliwa na kuingia Nchini kwa bei ya chini yauzwe kwa bei ya juu?
3. BPS wananunua mafuta kwa wingi na mara zote yanatumika miezi mitatu au minne kama alivyosema katibu mkuu wa wizara… imekuaje mafuta ya kwenye reserve yapande bei?
4. Kuna tozo na kodi kwenye lita moja ya mafuta zaidi ya 18 au 31% yaani kila sh 100 anayotoa Mtanzania kununua mafuta anakatwa sh 31, achilia mbali 4% ya logistics ikiwemo Demurrage ambayo ni uzembe unasababisha Watanzania kubeba mzigo huu.
5. Muhimu sana tenda ilitangazwa lini na wapi? Nani na nani walishindana? Nani alishinda na kwa bei ipi? Wewe umesema mama ndio aliwambia TPDC waagize!!! Hii ni sawa na Richmond nyingine.. sheria inasemaje?
Sisi tunasema:
1. Mafuta yaliyopo hayastahili kupanda bei kwasababu yaliagizwa na kuingia kwa bei ya chini.
2. Mzigo wa kodi na tozo uondoke kwasababu ni nyingi na kubwa mno kuliko Nchi zote Afrika mashariki, ndio maana hata Nchi zisizo na bandari zinauza mafuta chini kuliko sisi.
3. Kuendelea kukandamiza Watanzania na dhuluma hii ya wazi kutaleta balaa kubwa kwenye maisha hasa ya mtu wa chini.
Maana mafuta yakipanda kila kitu kinapanda..
Bwana Chalamila na yule kijana jifunzeni kwanza mambo haya.
Dunia ya sasa watu wana taarifa mkononi…
Mazungumzo yoyote unayofanya na Watanzania ujue sio wajinga, watafuatilia na wataringanisha taarifa hizo.
Watanzania wa sasa sio wa mwaka 47.
Nasema kwa uhakika hakuna mahali popote duniani mafuta yamefika 8,000 usd wala 6,000 Euro kwa lita.
Hakuna popote mafuta yanauzwa 400usd wala 600 Euro duniani.
USD 100 ni sawa na 260,000 Kwahiyo usd 400 ni sawa na 1,040,000.
Euro 600 ni sawa na 1,820,000
Kama ni 6,000 ni sawa na sh
18,200,000=
Kama ni usd 8,000 ni sawa na milioni 20.8 .
Lita moja ya mafuta Marekani inategemeana na state na state.
Kwa mfano Washington DC area kwa gallon 1 ambayo ina lita 3.8 ni usd 3.80 ambayo kwa pesa za Kitanzania ni 9,600, ukigawa kwa lita 3.8 ni sawa 2,526 kwa lita, ambayo hapa sisi kwa Tarime 4,020, kwa hapa Dar ni 3820.
Na kwa Marekani nzima wastani wa gallon moja ni usd 4.10.
Kwahiyo kwa wastani sana ni sh 2,600 za Kitanzania kwa lita.
Marekani ndio wako vitani na wao ndio wana uchumi mkubwa, lakini mafuta Marekani ni rahisi kwa zaidi kwa sh 1500 kwa kila lita tunayonunua huku..
Ukiwa na 10,000 ya Tanzania Marekani utanunua lita 4, na ukiwa ma hiyo hiyo hela hapa Tanzania utanunua lita 2 na point kidogo.
UPDATE: Guinea-Bissau’s military says it has taken full control of the country after detaining President Umaro Sissoco Embaló. The officers say they’ve suspended the electoral process and closed all borders indefinitely. It’s still unclear whether anyone else was detained along with the president.