Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema Wiki ijayo atakuwa na kikao na Viongozi wa Dini ambapo ajenda kubwa ya kikao hicho ni kutokomeza Adui ili Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan apenye bila kupingwa.
RC Chalamila amesema hayo Airport Dar es salaam leo mbele ya Rais Samia wakati wa mapokezi rasmi ya ndege mpya ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767 -300F.
Chalamila amenukuliwa akisema “Mh. Rais hizi ni cheche tu ndogondogo ili kuwatisha na kuwapa ukweli wenzetu ambao wameendelea kutubishia sana lakini hapa Dar es salaam kwa wiki ijayo nitakuwa na kikao na viongozi wa dini, ajenda kubwa ni tokomeza adui ili Rais Samia apenye bila kupingwa, Rais Samia Oyeee, Yanga oyeee”
#MillardAyoUPDATES