Mahakama Kuu ya Tanzania, masijala kuu jijini Dar Es Salaam imegiza shauri la mwanasiasa Mkongwe Nchini Dr.Wilbroad Slaa lirejeshwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake. Shauri hilo lilipelekwa Mahakama kuu baada ya Mahakama yaHakimu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 225
Mhe. Lissu anaendelea hapa.
Kama mtakumbuka nilisema ninavyoishi Ukonga, siruhusiwi kuonana na Mawakili wangu in private.
Mnaruhusiwa kutembelea Magereza naomba mliangalie na hili kama itawapendeza inawapa Mamlaka ya kutoa mapendekezo na mamlaka za Magereza kurekebisha masuala yanayohusu wafungwa kama haya niliyosema.
Ni muhimu kwamba kuwasiliana na washauri wangu wa kisheria ilindwe kama sheria inavyosema bila kusikilizwa na maafisa wa Magereza.
Ni hayo tu Waheshimiwa
Mhe. Tundu Lissu amemaliza na amekaa sasa.
Majaji wanaandika hapa.
Anasimama Renatus Mkude kuwa tutampatia hizi nyaraka ndani ya siku 14 tutampatia.
Hili la masuala ya utawala wa mambo ya magereza kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha National Prosecution Act na sisi ofisi ya DPP tutatembelea ili kuhakisha kunakuwa na fair trial.
Wameombwa Majaji anasema DPP ataenda eti huko Magereza kuangalia haki za Mtuhumiwa. Uongo uongo uongo. Hawana hata aibu hawa jamaa.
Majaji wanaandika baada ya kusikia hayo kutoka kwa Wakili wa Serikali, Renatus Mkude.
Majaji wanajadili pale.
Yuko Jaji muda wote yeye huwa anacheka anafurahi tu sijui huwa anatabasamu jambo gani? Wanaofika hapa Mahakamani wanamfahamu vizuri.
Jaji Ndunguru: Tumesikia hoja za Jamhuri na Hoja za Mshitakiwa nae kama ambavyo mshitakiwa ameturahisishia kuwa mikono yetu imefungwa kwamba yapo hayo maombi ya marejeo Mahakama ya Rufani.
Sasa shauri hili linasimama hadi pale Mahakama ya Rufani itakapotoa uamuzi.
Suala la Gerezani wakili wa Serikali amesema na sisi pia tumelichukua.
Mwenendo wa shauri hili unasimama hadi pale mambo ya Court of Appeal yatakapoisha.
So kesi hii imeahirishwa hadi hapo itakapoitwa tena.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 224
Majaji wameingia muda huu saa nane Kamili Mchana.
Wanaandika pale juu.
Mheshimiwa Lissu ameingia na kuteta jambo na Dr. Nshala tunamsikia anasema waende kokote watakapotaka kwenda tutakutana nao huko. Sasa sijui ni wapi anamaanisha.
Anasimama Renatus Mkude Wakili wa Serikali kwa niaba ya jopo la Mawakili wa Serikali tunaomba radhi kwani tulifikiri tungetumia lisaa limoja.
Mchana huu nipo na Ajuaye, Thawabu Issa na Cathbert Mbiringe. Kwa wote tunawakilisha jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Shauri lilipangwa kuendelea na mashahidi. Lakini tumetafakari na tunaitafsiri kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha Appellate Jurisdiction Act na kanuni ya 65(1) ya kanuni za Mahakama ya Rufani.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) anatoa taarifa ya kuwasilisha taarifa ya mapitio (revision)
Hapa kwanza anakosea Mapitio ni Review alipaswa kusema Marejeo ndio Revision sijui kasoma wapi nae huyu jamaa.😂😂😂
Anaendelea hapa Renatus Mkude, kuwa Notice of motion hiyo imeambatanishwa na kiapo cha Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ambayo taarifa hii ya kutoa notice kwenda Mahakama ya Rufani imesainiwa leo Tar. 24/02/2026.
Na kupokelewa kwa mifumo ya kielektroniki inayotambulika na Mahakama na kusajili kama. CRIMINAL REVISION NO. 7203216/2026 imepokelewa na Mahakama ya Rufani Tanzania hapa Dar es salaam.
Ambalo chimbuko lake ni Criminal Sessions No. 19605/2025 ambayo iko mbele yenu Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu. (Ndunguru, Karyemaha, Kiwonde)
Kwa kuwa shahidi wetu aliyekuwa anafuata ACP Mahamba tuliyemuombea notice additional substamce of evidence na ikakataliwa.
Ni Rai yetu kwamba kwa kuwa shauri hili limeshapokelewa Mahakama ya Rufani haiwezi kusimama ili kuweza kutoa nafasi kwa shauri husika huko Mahakama ya Rufani kuweza kuamuliwa.
Ni hayo tu kwa sasa.
Tunamsubiri Mh. Lissu atajibu nini?
Mhe. Lissu anaanza.
Baada ya kuzikiliza wasilisho la upande wa Mashitaka nina haya ya kusema.
1. Kwa vile mimi nipo gerezani na wanajua nataka wanipatie hiyo nakala ya Notice of Motion waliyofile niweze kuiona.
2. Ninafahamu na ninatumaini na wao wanajua kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 8(2)(d) cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa ambacho wamekitaja (Appellate Jurisdiction Act) wanafahamu kwamba hakiruhusu rufaa wala mapitio wala marejeo ya maamuzi ya Mahakama ambayo hayamalizi shauri la msingi. (Interlocutory decisions) sina shaka na wao wanalifahamu hilo.
3. Waheshimiwa Majaji siwaombi mtoe uamuzi wowote kuhusu hili ninalolisema.
Nataka iwe kwenye record kwamba nafahamu na naamini upande wa mashitaka wanafahamu lengo la kupeleka ombi la marejeo Mahakama ya rufani na wanafahamu hairuhusiwi ni kurefusha mashauri haya ili niendelee kukaa Gerezani. Ni hilo tu.
Kwamba tupeleke Mahakama ya Rufani ili huyu mbaya wao ambae ni mimi aendelee kukaa Gerezani.
Kwa vile wananipeleka kwe ye Mahakama ya Rufani nataka niwaeleze kuwa nitawafuata huko huko naenda kuwashughulikia huko huko.
Kama ambavyo kesi yao is dead on arrival najua hata hii revision yao pia imeshakufa.
Tutarudi hapa yakiisha huko ya Mahakama ya rufani tutarejea hapa na nitawashughulikia tukirudi.
Jambo la Mwisho Mawakili wangu wametaka kunipa nyaraka hapa lakini siwezi kupewa hadi nyie mseme.
Sijui wanaogopa nini watu wa magereza nisipewe huo uamuzi hapo ni makaratasi tu.
Naambiwa ni hukumu kutoka huko Umoja Wa Mataifa lakini Magereza wanaogopa nisipewe.
Tena ni uamuzi unaohusiana na mimi kuwepo Gerezani. Tatizo liko wapi?
Jaji anasema uko wapi? Umepelekwa wameuona wamesema wape Mawakili wa Serikali.
Wako wanasoma hapa Mawakili wa Serikali huo uamuzi.
Anasimama Renatus Mkude anasema mimi ni member wa working group za UN Human Rights Council.
Jaji: Tumesema apewe au asipewe?
Renatus Mkude: Apewe tu.
Part 225 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KUTOKA_MAHAKAMA_KUU
Majira ya saa nane kasoro tano, wameingia Mawakili wengine wa Serikali.
Ananitonya Wakili mmoja hapa kwamba amechungulia nyaraka aliyonayo Renatus Mkude ni Notice of Motion kwenda Mahakama ya Rufani nafikiri wanaenda kufanya Revision ya uamuzi uliofanywa leo na Majaji wa Mahakama kuu leo kuhusu ile notice ya kuongeza ushahidi wa Amin Mahamba.
Huku ni kupoteza muda wa shauri hili.
Kwa kifupi kisheria tunaambiwa kukata rufaa au kupeleka maombi ya kufanya marejeo mahakama ya rufani haizuii kesi kuendelea.
Mahakama inayo mamlaka pia kukataa maombi yoyote ya Jamhuri ya kutaka kuahirisha kesi hii ikiona wanachotaka kulifanya Jamhuri ni kupoteza muda na kukiuka haki za msingi za Mshitakiwa.
Muda mfupi ujao tutajua ukweli wa mambo.
Kwa sasa tunajaribu kuchokonoa kidogokidogo kinachoendelea.
Tuendelee kuwa pamoja.✊
#UPDATES_KUTOKA_MAHAKAMA_KUU
Muda huu saa nane kasoro mchana.
Ameingia Wakili wa Serikali Renatus Mkude, tunasubiri Majaji nao waingie, amekuja peke yake akiwa na kikaratasi kimoja kinachosadikika kuwa ni kiapo fulani ambacho wameshakifile Mahakamani.
Hatujui kinahusiana na kufuta mashitaka, kukata rufaa au jambo gani lakin amekuja peke yake na hako ka nyaraka kake.
Muda mfupi ujao tutajua nini ni nini? Au nini kinaendelea..
#KIMENUKA_MAHAKAMA_KUU!!!
Wananchi waliofika Mahakamani muda huu saa saba na nusu wameanza kuimba
Tunaitakaaaaa Jamhuri!…
Tunataitaka Jamhuriiiiiiii!….
Tunaitaaka Jamhuriiii!…
Wanaimba huo wimbo Mahakamani, wameanzisha wakazi wa kule GAZA.
JAMBO LA KUSHANGAZA MAHAKAMANI.
Muda huu wameingia wasaidizi na walinzi wa Majaji wamechukua Computer na vifaa vya Mahakama wameondoka navyo.
Inaonekana muda huu kesi haiwezi kuendelea maana wanaondoa kila kitu Mahakamani.
Taarifa tuliyonayo Mawakili wa Serikali hawajaonekana na hawajarudi Mahakamani so muda huu Karani amesimama hapa na kusema kuwa kuna jambo limejitokeza anaenda kutafuta ufafanuzi kwa Msajili wa Mahakama atarudi kuleta mrejesho.
Kwahiyo tupo njiapanda hatujui kinachoendelea hadi sasa.
Kesi imewashinda wanalazimisha ni aibu kwa Mahakama kuiamuru Jamhuri kuwa ilete Mashahidi baada ya lisaa limoja kwasasa ni masaa mawili yanaelekea matatu hakuna kinachoendelea.
Mawakili wa Serikali wanaamua kesi iendelee au isiendelee.
Vituko, Vichekesho na Maajabu.
Tunaendelea tuone mwisho wa hizi drama zao.
Wako Muhabarishaji,
Hilda Newton.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 24, 2026
Last time tuliishia Part 222 so leo tunaendelea na-;
Part 223
Majaji wameingia na Mshitakiwa pia ameingia.
Karani anasoma shauri hapa.
Anasimama Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Thawabu, Cathbert Mbiringe.
Anasema leo tumekuja kwa ajili ya kupokea ruling na sisi tuko tayari.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Lissu: Na mimi niko tayari.
Jaji anaanza kusoma hapa UAMUZI.
Uamuzi huu unatokana na pingamizi lililowekwa na pingamizi la mshitakiwa kutokana na taarifa ya kuongezwa kwa ushahidi.
Taarifa hiyo ililetwa tarehe 18/02/2026 na upande wa Mashitaka kwamba unatokana na pingamizi lililowasilishwa na mshitakiwa.
Notice hiyo ililetwa kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Mshitakiwa alieleza Mahakama kwamba kifungu hicho kinaelezea shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa wakati wa mwenendo kabidhi na hivyo walichokileta upande wa mashitaka ni kuleta ushahidi mpya.
Upande wa mashitaka walijibu notice ipo halali kwa mujibu wa sheria na imekibidhi matakwa ya kisheria na ipo kwa mujibu wa sheria.
Huo ndio ulikuwa msingi wa hoja za pande zote mbili.
Mahakama imeona hoja inayopaswa kuamuliwa ni je notice hiyo ipo kwa mujibu wa sheria?
Ili kurahisisha Mahakama imeona ili reproduce notice hiyo inavyosema.
Anasoma notice inavyosema kwamba ni notice ya kuongeza maelezo ya ziada ya shahidi husika ambae ni Amin Mahamba.
Hakuna mashaka kwamba upande wa mashitaka wanataka kuongeza ushahidi wa Amin Mahamba.
Kwa vile Amin Mahamba ni shahidi na statement yake ilishasomwa wakati wa committal ilishasomwa.
Notice inasema ushahidi unaotaka kuletwa ni wakati wa uchaguzi wa tar. 29/10/2026.
Anasoma kifungu cha 308 cha CPA kinavyosema.
Ukiangalia kifungu hicho kinatoa masharti au mazingira ambayo notice hiyo ni reasonable au laaa.
Masharti ni kwamba
1. Maelezo yatoke kwa shahidi
2. Uwe ni ule ushahidi ambao haukusomwa wakati wa committal
3. Uwe ni ushahidi ambao haukusomwa wakati wa proceedings
Kifungu cha 308 ndio kinachosema hawezi kutoa ushahidi hadi watakapoleta notice na hivyo basi ukiangalia hayo kifungu hicho cha 308 kinafungua mlango kwa shahidi ambae alikuwepo na bahati mbaya maelezo yake hayakuletwa.
Amin Mahamba maelezo yake yalikuwepo wakati wa commital, anataka kuleta mambo ya Uchaguzi ambayo hayakuwepo wakati wa committal.
Ipo kinyume na kifungu cha 308 cha CPA.
Hivyo basi kifungu cha 308 kinaweza kuruhusu notice hiyo tumeona kwamba kifungu hicho hakiruhusu kabisa.
Shauri la Remina Omary Abdul tumeona linahusiana na vielelezo vya wakati wa committal. Shauri hilo haliwezi kutibu chochote katika hoja iliyopo mbele yetu.
Hiyo notice ya kuongezwa kwa ushahidi ambayo imeletwa na upande wa mashitaka haitambuliwi na kifungu cha 308 cha CPA.
Kimsingi tunasema kwamba fundamentally haiko sahihi na baada ya kusema hayo basi notice hiyo ni incompetent na tiba pekeee iliyopo ni kwamba notice hiyo lazima iwe struck out. Ni hayo tu.
Anasimaa. RENATUS MKUDE anasema baada ya kupokea ruling tunatafakari tunaomba ahirisho ya lisaa limoja.
Twende kutafakari.
Bado majaji wanashauriana pale juu.
Nafikiri leo KATUGA atajua vizuri nani ni Bingwa wa Sheria😂
Anasimama Mh. Lissu anasema mmesema kuwa mashahidi waletwe leo na mlisema tutasikiliza uamuzi wa pingamizi na tutasikiliza shauri leo.
Sasa wanasema tuahirishe kusikiliza ili wakatafakari.
Wanaenda kutafakari nini? Ili iweje? Huu uamuzi haukatiwi rufaa.
Tusipoteze muda kila tunapopoteza muda anayeumia ni mimi sasa wao walipaswa kuleta mashahidi na wasitupotezee muda kabisa, tuendelee kusikiliza shauri hili.
Majaji wanaandika kidogo
Anasimama Renatus Mkude anasema tumemsikia Mshitakiwa
Tuna mambo mawili.
1. Tumepokea ruling ya Mahakama na tumeikubali
2. Jambo la pili ni kwamba tulimtaja shahidi ambae lazima tuwezi kumuandaa shahidi yetu
Jaji Ndunguru anasema tulisema muwe na mashahidi wakutosha. Tukiendelea kubishana tutapoteza muda, turudi mahakaman saa 5 kamili
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 222
Katuga anasema kifungu cha 308 ni mlinzi wa kifungu cha 263 cha CPA ni kumfanya mshitakiwa awe aware na ushahidi wote anaokutana nao Mahakama kuu.
Ushahidi upo wa aina nne, real, documentary, testimonial na nyingine nimesahau nitaikumbuka.
Kwahiyo kwa maana ya aina ya shahidi nne zinatakiwa zioneshwe kwa mshitakiwa kabla ya kuwa committed kwenda High Court na kwakuwa kuna takwa hili la 263 kukawekwa kifungu cha 308 ambacho ni mlinzi sasa.
Kwamba hakutakuwa na ushahidi utakaoingia hadi uwekwe wazi basi prosecution wampe notice kuhusiana na ushahidi huo ni lini prosecution wamegundua huo ushahidi. Je mshitakiwa alikuwa na reasonable time kuupitia.
Kif. 308(4) kinazungumzia substance or witness.
Kesi ya Remina Omary Abdul vs Jamhuri CA 189/2020 Mahakama ya Rufaa ilisema, INASEMA IF PART OF THE EVIDENCE IS NOT DISCLOSED.
Mahakama ili quote with approval maneno kuwa additional evidence is allowed.
Sisi tunasema mbali na statement yake kusomwa tunataka kuleta mambo mengine ambayo hayakujumuishwa.
Notice hii ina comply na tafsiri ya sheria na sio tafsiri ya mtu. Iko sheria na tunaomba ikubaliwe.
Katuga kuna maneno pia yamesemwa kuwa notice hii ikiachwa hizo sio hoja. Unamtisha nani? Naona kama anatutisha ni hoja ambayo itafungua pandora na hiyo pandora ni ipi?
Tunaomba mapingamizi yatupiliwe mbali.
Anasimama Mh. Lissu kumjibu Kituga.
Nimesikiliza majibu yao naomba niseme yafuatayo.
1. Kifungu cha 308 cha CPA kinahusu shahidi mpya. Shahidi mpya kimesema ni yule ambaye maelezo yake au substance ya maelezo yake haikusomwa kwenye committal. Kwahiyo kifungu hicho kinahusu shahidi mpya na sio ushahidi mpya. Suala ni shahidi wa ziada na sio ushahidi wa ziada wa shahidi ambae tayari maelezo yake yapo tayari.
2. Kwenye notice hii suala la kuamua sio reasonable au laa. Ni suala la kinacholetwa ni shahid mpya au laa.
3. Hiyo kesi ya Remina Omary Abdul waliyoleta si mara ya kwanza inazungumzwa kwenye Mahakama hii. Ililetwa kipindi kile cha Committal. Inahusu kifungu cha 263 tu. Ukurasa wa 32 ni kuhusu section 246 ambacho ni 263 ya sasa. Kwahiyo hiyo kesi inahusiana na mambo ya Committal basi kifanyeni kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Mlango wa Amin Mahamba ulifungwa kwenye committal kama mnataka tafuteni shahidi mwingine sio Amin Mahamba.
Hoja ya kwamba hili ni pingamizi limeletwa pre mature nasema liko timely maana yanayohusika na kesi hii yalishakamilika na kuletwa Mahakamani.
Effect yake ni kunibadilishia shitaka maana shitaka langu ni la tar. 03/04/2025 haya ya October ni mambo mapya.
Mkiyaruhusu kwa kuruhusu notice hiyo na nimesema niko tayari, je wao watayaweza? Kwasababu ya October kuna genocide kuna mass killings, mass murder. Ya October ni magumu sana.
Pingamizi langu litalinda integrity ya shauri hili na mashauri haya. I'm only trying to help them wanafikiri kuna deal pale hakuna deal yoyote.
Angalieni kifungu cha 308 cha CPA.
Hii notice ifutiliwe mbali, naomba hivyo.
Majaji wanateta hapa.
Tunasubiri uamuzi wao kuhusu pingamizi hili.
Jaji Ndunguru amejadiliana na wenzake kwa muda mrefu sana hapa.
Anasema ili tuweze kuandika uamuzi na tutarudi kesho saa tatu asubuhi na tutaendelea na mashahidi wengine.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 221
Jaji Ndunguru ameteta sana na wenzake kama dakika 10 hivi.
Sasa anawasha kipaza sauti.
Anasema yafuatayo: tumesikiliza hoja zote hivyo vijembe vyenu msivilete.
Sasa mshitakiwa alisema anapingamizi na tukasema upande wa mashitaka walete open statement ili Mahakama iamue.
Mambo mengine ya kwamba imeambatana na nini na nini kipo wapi hayo sio mambo ya msingi.
Mshitakiwa endelea sasa, hawa upande wa mashitaka mmemaliza hapo, presentation ya notice na justification ya notice.
Watu wanacheka hapa 😂😂😂😂
Nafikiri mpaka sasa Katuga ameelewa nani ni Bingwa wa Sheria.
Mhe. Lissu amasimam, sasa Waheshimiwa Majaji kwa kuanzia niseme hivi waliyosema wenzetu.
1. Upande wa mashitaka unasema notice yao haileti shahidi mpya bali inaongezea ushahidi wa shahidi ambae ushahidi wake ulishatolewa kwenye committal.
2. Wamemtaja huyo shahidi kwa jina kabisa.
3. Wamesema wameleta viambatanisho vinavyotakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 308(2) cha CPA.
Sasa baada ya kusema twende kifungu kinavyosema cha 308
A witness whose statement or evidence was not read during committal......
Kifungu kinasema shahidi mpya.
Kinachotakiwa kuletwa ni jina la shahidi wa ziada, huyu ndio anaweza kutolewa notice.
Wamesema wenyewe hawaleti shahidi mpya bali wanaongezea ushahidi wa shahidi aliyepo.
Sasa huyu shahidi ambae tayari yupo na wamemtaja huyo Shahidi ACP Amin Mahamba.
Sasa waheshimiwa Majaji naomba niwaalike kwenye ukurasa wa 90 na 91 na 99 na 100 wa record ya committal proceedings na ukurasa wa 134 wa record ya Mahakama hii ambapo upande wa mashitaka ulitaja majina ya mashahidi wao.
Huyo Amin Mahamba yupo na mimi maelezo yake ninayo hapa sasa Waheshimiwa majaji hiyo notice inaingiaje mahakamani.
Ushahidi wake tayari upo mahakamani na notice inatakiwa iwe ya shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa mahakamani.
Hii sio notice ya additional witness ni notice ya additional evidence ambayo haipo kisheria nimetafuta CPA yote hicho wanachosema hakipo.
Jambo lingine ni kwamba wanaleta ushahidi wa mtu aliyefanya upelelezi wa matukio ya uchaguzi mkuu 2025 sasa Majaji matukio ya tukio ya tarehe 29/10 mimi tayari niko mahabusu
Anasimama Katuga anasema tunapinga anaanza kujadili ushahidi wetu kama mtakubali ni sawa tu.
Lissu: Si ndio kayaleta haya mwenyewe wanakatazaje nisiyazungumzie?
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa endelea.
Lissu: amesema mwenyewe kwa mdomo wake hapa Mahakamani. Nilimwambia asibwabwaje sana. Akang'ang'ania kuanza kusema mambo ya tarehe 29/10 ndio maana na mimi nasema hayo ya tarehe 29 mimi nilikuwa jela.
Wanafikiri hayo yatawasaidia maana wanataka kugeuza mashitaka kwa kuleta mambo ya tarehe 29/10/2026. They can not amend the information through the back door. Kama mnataka ku amend information nendeni kwenye kifungu cha 294 ch CPA.
Hiyo wanayoiita notice haipo kisheria. Haitambuliki. Hiyo notice muifutilie mbali. Yaani notice na yaliyomo.
Na mwisho, Wahe. Majaji hiyo notice ikiachwa ikawa sehemu ya record ya Mahakama itafungua sanduku la pandora ambalo lina kila aina ya mambo mabaya ambayo sidhani kama itaweza kushughulika mambo hayo.
Wanataka tuzungumze mambo ya October 29 mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida. Mkifungua huo mlango tutaenda huko. Tutazungumzia mauaji ya kimbali na tutaulizana nani aliyeua watanzania. Hii kitu haina mashiko. Are they ready? Mimi niko tayari. Isiruhusiwe ikiruhusiwa niko tayari?
Jaji tafadhali naomba tusiende huko.
Katuga aliambiwa na Lissu kuwa huwezi kunifundisha Sheria akakataaa. Baada ya Lissu kumaliza hapa. Katuga amekuwa mdogo sana yani. Ni kama anataka kulia.
Katuga anasimama anasema napaswa kufanya nini reply au rejoinder
Mhe. Lissu anasema fanyeni reply halafu mimi ndio nitakuja kumaliza.
Wanakubaliana hivyo.
Part 222 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 23, 2026
Last time tuliishia Part 219 so leo tunaendelea na-;
Part 220
Mh. Tundu Lissu anaingia Mahakamani.
Mawakili wa Serikali wapo tayari na Majaji wana kila dalili ya kuingia muda wowote.
Kelele za Shujaa Shujaa Shujaa zinasikika.
Mh. Lissu ameingia anateta jambo pale na Wakili Kisabo na Mahinyila ni kama anawaagiza jambo.
Namuona Wakili Kisabo anachukua simu ni kama anafanya mawasiliano.
Majaji wameingia kuna mtu simu yake imeita, watu wanamshangaa.
Anasimama Kalani anasoma case number.
Anasimama Renatus Mkude, tupo Ajuaye, Katuga, Thawabu Issa na Cathbert Mbiringe. Shauri lilipangwa kwa ajili ya kusikiliza Notice ya kuongeza mashahidi na ushahidi na sisi tuko tayari.
Majaji wanaandika kidogo.
Wanamuuliza Mshitakiwa.
Mhe. Lissu anajibu na yeye kuwa yuko tayari.
Wanaitwa Upande wa Mshitaka anasimama Katuga kuanza.
Mhe. Lissu waheshimiwa Majaji nimepinga hiyo notice toka ijumaa kwahiyo ningesikilizwa.
Katuga Mheshimiwa Jaji utaratibu ni sisi kuiwasilisha ili yeye apinge kama ana hoja ya kupinga hii sio Application.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji hicho wanachoita notice sio notice kabisa na hakitambuliki kisheria.
Jaji sisi tulitaka waeleze nini kinaendelea tu.
Mhe. Lissu: Kama ni hivyo sawa.
Katuga: Mnamo tar. 18/02/2026 kwa njia ya mtandao tulifile notice ya kuongeza ushahidi (notice to file additional statement of evidence) tuliifile kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Pamoja na notice hiyo tuliambatanisha substance ya ushahidi huo, ushahidi huu haumleti shahidi mpya bali ni nyongeza ya Ushahidi wa ACP, Amin Mahamba.
Kwamba ushahidi huu haujakuwa committed Mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Notice hii inakuja kukidhi matakwa ya kifungu cha 308 cha CPA ambacho kinasema hakuna shahidi au maelezo ya shahidi vitatolewa mahakamani unless viwe vimesomwa wakati wa mwenendo kabidhi (committal)
Kifungu hicho kinafafanua maana ya substance of evidence ikiwa ni pamoja na kitu chochote ikiwemo nyaraka na vitu vingine vinavyoshikika.
Kama ambavyo notice inajieleza, substance ya ushahidi kwamba Amin Mahamba alikuwa ni kiongozi wa timu ya upelelezi wakati wa uchaguzi wa 2025 na baada ya uchaguzi.
Na kile alichokipata kutokana na upelelezi ni kitu ambacho haukusomwa pale kwenye committal.
Ushahidi huo tumeupata na kuugundua wakati tumejiandaa kumuita ACP Amin Mahamba siku ya tarehe 16/02/2026 kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA hakijaeleza ni kwa jinsi gani notice itakuwa. Hata kwenye zile prescribed form zilizopo kwenye Sheria hii haijawekwa.
Kifungu hicho kinasema notice ieleze jina la shahidi, substance ya ushahidi na details za shahidi kiujumla kwa mujibu wa kifungu cha 308 (2) cha CPA.
Hivyo vyote tumefanya kwenye notice yetu kucover matukio ya tarehe 29/10/2025.
Anasimama Mhe. Lissu, anasema waheshimiwa mbona kama anaendelea kufanya mambo ambayo hamjamuelekeza.
Katuga waheshimiwa kwani hiyo introduction iko chini ya Sheria gani? Sisi tunaintroduce kwa namna tunayoona ili mwenzetu.
Mhe, Lissu: Asinifundishe Sheria, asijaribu kabisa kunifundisha Sheria, anaanzaje kufanya submission ya hiyo notice kabla uhalali wake haujaamuliwa.
Katuga: Waheshimiwa hakuna bingwa wa Sheria, mabingwa ni nyie tu Majaji.
Majaji wanateta pale juu.
Tunasubiri muongozo wao.
Part 221 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 217
Anaendelea Mhe. Lissu na Cross examination.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi ili nikuhoji vizuri naomba uwaambie waheshimiwa majaji kama upo tayari maelezo yako yapokelewe kama kielelezo
Coplo Amani : nipo tayari
Serikali: hatuna pingamizi.
Mahakama; maelezo haya yanapokelewa kama exhibit D14
Mhe. Lissu: Waheshimiwa naomba exhibit D14.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi maelezo yako sasa ni kielelezo D14 naomba uyaangilie vizuri
Swali langu la kwanza umesema unafanya kazi katika kitengo cha upelelezi chini ya Mkuu wa upepelezi wilaya
Coplo Amani : ni kweli
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama hayo maneno yapo kwenye D14
Coplo Amani : yapo
Mhe. Lissu: wapi
Coplo Amani : angalia page ya pili
Mhe. Lissu: soma
Shahidi anasoma
Mhe. Lissu: Naomba niangalie hayo maelezo na waheshimiwa majaji naomba na nyie muangalie kwenye typed.
Mhe. Lissu: naomba na mimi nisome waheshimiwa majaji, yupo sahihi kama alivyosoma ya kwangu ndio yamekosewa.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako shahidi umesema wewe ni msaidizi katika shughuli zote za upelelezi wilaya ya Mbeya
Coplo Amani : sahihi kabisa
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama hayo maneno yapo kwenye kielelezo D14
Coplo Amani : hayo maelezo hayapo
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako umesema ulikua unaelezea Kituo cha polisi Ilomba ulisema ni Kituo kidogo cha polisi kilicho chini kituo cha kati cha mbeya kama out post na ukisema ivi ina maana hakija-qualify kuwa Kituo cha Polisi?
Coplo Amani : sahihi
Mhe. Lissu: kama hayo maneno yapo kwenye maeleezo yako
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: 4 april 2024 kwa majibu wa maelezo yako ulipewa maelekezo na Jorum kwenda mtaa wa Mtengule
Coplo Amani : Kweli
Mhe. Lissu: Lakini alikupa namba ya simu askari wa intelijensia ili akuongoze ukamkamate mhalifu
Coplo Amani : sahihi
Mhe. Lissu: waambie kama hayo maneno kwamba ulipewa namba ya simu yapo kwenye maelezo yako.
Coplo Amani : hayo maelezo hayapo katika kielelezo D14
Mhe. Lissu: uliwaeleze askari wa intelijensia kama askari wanaojichanganya na raia kama vile boda boda
Coplo Amani : ni kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama huo ufafanuzi wako upo kwenye maelezo yako.
Coplo Amani : hakuna
Mhe. Lissu: : Baada ya kupewa namba ya mtu wa intelijensi uliwasiliana nae na badae ulikutana nae mtaa wa Mtengule
Coplo Amani : Kweli
Mhe. Lissu: waeleze kama hayo maneno yapo kwenye maelezo yako
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Umesema huyo Askari wa intelijensia alikuongoza na kukuonyesha huyo mtuhumiwa katika kijiwe cha boda boda na kulikua na watu wengi, waeleze kama hayo maneno yapo kwenye statement yako
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Umesema taarifa ulizopewa mtuhumiwa ndiye anayehamasisha wenzake kufanya vurugu na kuzuia uchaguzi wa 2025
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: waonyeshe hayo maneno kama yapo katika maelezo yako.
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Sasa ushahidi wako unasema ivi baada ya kuonyeshwa huyo mtuhumiwa ulimfata na kumtoa pembeni ya kijiwe, kisha ukajitambulisha kwake kwa jina na ukamwambia tuhuma zake za kuhamasisha vurugu na kuzuia uchaguzi wa 2025, sasa angalia D14 na ueleze kama hayo maeno yapo?
Coplo Amani: hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako umesema, ulimueleza kuwa anahitajika kituo cha polisi Ilomba na alikubali kwenda, ni kweli au si kweli
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Waeleze kama hayo maneno yapo katika maelezo yako D14
Coplo Amani: Ndio yapo
Mhe. Lissu: yapo wapi, utusomee?
Coplo Amani : hayapo
Mhe. Lissu: Umesema kwamba, kwenye maelezo yako tuhuma iliyokuwa inamkabili ni kinyume na kifungu cha 390, waeleze waheshimiwa majaji kama kwenye maelezo yako yapo?
Coplo Amani : hayapo.
Mhe. Lissu: umesema baada ya kumhoji alikubali kuwa anashawishi wenzake juu ya vurugu na wakati akiangalia YouTube aliona Tundu Lissu akihamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi wa 2025
Coplo Amani :Kweli
Part 218 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 216
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa Maswali ya Dodoso.
Anasimama Mheshimiwa Lissu kwa ajili ya kumfanyia Cross Examination Shahidi ambae anaitwa Coplo Amani.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa kwa kuanzia naomba nipatiwe kielelezo D12, waheshimiwa majaji haya ni maelezo ya P3.
Mhe. Lissu : Sasa shahidi naomba uwaeleze majaji kama uliandika maelezo polisi
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama unaweza kuyatambua ukionyeshwa
Coplo Amani : nikionyeshwa nitaweza kuyatambua
Mhe. Lissu: naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake aliyoandika polisi.
Coplo Amani : haya ndio maelezo yangu
Mhe. Lissu: asante sana, sasa shahidi hayo maelezo yako naomba uwaeleze majaji kama uliyaandika mwenyewe au uliandikiwa na askari mwingine?
Coplo Amani : haya maelezo niliandikiwa na askari mwingine
Mhe. Lissu: mtaje jina tafadhali
Coplo Amani : Anaitwa H9207 detective coplo Robert
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako hayo waeleze majaji kama ni utaratibu mtu anayeandika maelezo ya shahidi hawezi akawa ndio mtu huyohuyo kama shahidi?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji pamoja na majibu mazuri ya shahidi huyu nataka ku-impeach credibility yake, nitamsomea maelezo yake, nitamuonyesha maeneo nitakayotaka kumuuliza maswali halafu nitamtaka ayawasilishe kama kilelezo.
Mhe. Lissu anamsomea maelezo yake
Mhe. Lissu : Haya ndio maelezo yako kama nilivyoyasoma?
Coplo Amani : Waheshimiwa majaji mshtakiwa kuna maeneo amekosea naomba nimrekebishe, sio kata ya Isuesue ni Isyesye 😁
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji kwakua na nyie mnarekodi hii mimi nimeona imeandikwa isuesue waheshimiwa…
Kwenye maneno “ni dereva wa bodaboda isuesue Mwintengule”… kwenye original Isyesye… kwahiyo tutaenda na ya kwako.
Kuna eneo lingine ambalo lina shida?
Coplo Amani : hapana.
Mhe. Lissu : Sasa kuna maeneo nataka kukuhoji kwa ajili ya kukukanusha kama ifuatavyo;
1. Kwamba unafanya kazi chini ya OCCID Mbeya mjini
2. Kwamba wewe ni msaidizi wa upelelezi ndani ya Mbeya mjini
3. Umeelezea Kituo cha Polisi cha Ilomba kwamba ni kituo kidogo kilichopo chini ya kituo cha Kati Mbeya umesema ni kama out post.
4. Umeeleza kwamba kaimu OCCID Inspekta Jorum alipokupa maelekezo ya kwenda kumkamata P3 alikupa namba ya simu ya askari wa kitengo cha intelijensia kwa ajili ya kwenda kumkamata P3
5. Kwamba hawa askari huwa wanajichanganya na raia kama dereva boda boda n.k
6. Baada ya kupewa namba ya simu ukawasiliama nae na mkakutana Isyesye.
7. Kwamba kulikua na watu wengi na mlipita na akakuonyesha mtuhumiwa kwenye kituo cha boda boda.
8. Taarifa mlizopewa na Jorum ni mtuhumiwa ndiye anayehamasisha wenzake kufanya vurugu uchaguzi wa 2025
9. Baada ya kuonyeshwa huyo mtuhumiwa ulimfata na kumtoa pembeni ya kijiwe na kisha ulijitambulisha kwake kwa jina na kumueleza tuhuma zake.
10. Ulimwambia baada ya kumtoa pembeni kwamba anahitajika Kituo cha Polisi Ilomba na yeye alikubali kwenda.
11. Ni ushahidi wako maelezo aliyoandika mtuhumiwa ni uchochezi, kusababisha vurugu na kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
12. Shitaka uliloandika lilikua ni kukiuka masharti ya kifungu cha 390 cha Penal code
13. Wakati ukimhoji alikwambia kwamba aliona taarifa kwenye YouTube akamuona Lissu akiwa anahamisisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi 2025.
14. Baada ya kuandika maelezo yake ulimjulisha inspeka Jorum akakuelekea kumuachia kwa dhamana na we anaripoti kila baada ya siku tatu
15. Ni ushahidi unaohusu tareh 17 april 2025 kwamba siku hiyo wakati ukiwa Ilomba Kituo cha Polisi ulielekezwa na inspekta Horum kuandika maelezo ya mtuhumiwa kama shahidi kuhusiana maelezo ya Mwenyekiti wake Tundu Lissu na yeye kuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana wenzake kufanya vurugu.
16. Baada ya kurekodi malezo hayo na ulimjulisha Inspekta Jorum na ukamkabidhi malezo hayo.
Part 217 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 215
Katuga anaendelea kumuongoza Shahidi ambae ni Coplo Amani
Wakili wa Serikali: Kikafuata nini?
Coplo Amani: Baada ya kuonyeshwa mtu huyo, nilimfata na nikamuita nikamtoa eneo hilo la bodaboda tukakaa pembeni kidogo, nikajitambulisha kwake kwamba mimi ni G9304 natoka Kituo cha Polisi kati Mbeya, baada ya hapo nilimueleza tuhuma yake ya kuhamsisha vurugu na kuharibu uchaguzi wa 2025.
Wakili: Uchaguzi ulihusu nini?
Coplo Amani : Uchaguzi ulikua unahusu rais, wabunge pamoja na madiwani.
Wakili: Ukafanya nini?
Coplo Amani : Baada ya kumueleza tuhuma zake nikamueleza kwamba anahitajika Kituo cha Polisi Ilomba.
Wakili: kikafuata nini?
Coplo Amani : Baada ya hapo hakubisha na alikubali kwenda kituo cha polisi Ilomba.
Wakili: ukafanya nini?
Coplo Amani : niliondoka nae mpaka Kituo cha Polisi Ilomba
Wakili: ukafanya nini?
Coplo Amani : Baada ya kufika kituo cha Polisi nilimjulisha Inspekta Joram, akanipa maelekezo ya kumuandika mtuhumiwa maelezo.
Wakili: anaitwa nani huyo mtuhumiwa?
Coplo Amani: Mtuhumiwa huyo katika shauri hili anajulikana kama P3.
Wakili: Ikawaje?
Coplo Amani : Nilimuandika maelezo kwa tuhuma za uchochezi na kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Nini kikafuata?
Coplo Amani : Baada ya hayo maelekezo nilimuandika maelezo kama nilivyoelekezwa na nilimuandika maelezo kama mtuhumiwa.
Wakili: kwa kosa gani?
Coplo Amani : makosa hayo ni kinyume cha kifungu cha 390 cha sheria ya kanuni ya adhabu
Wakili: Ikawaje?
Coplo Amani :. Baada ya kumhoji mtuhumiwa alinieleza kwamba ni kweli alihamasisha wenzake kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025
Wakili: Nini Kingine?
Shahidi: Pia alinieleza siku hiyo ya tarehe 4 April 2025 alikua akipitia taarifa mbalimbali na wakati anaendelea kupitia taarifa kwenye mtandao wa youtube alisikia mtu ambaye alimtaja kama Mwenyekiti wa CHADEMA anayeitwa Tundu Antiphas Lissu akiomgea na kutoa kauli za kuhamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wakili: kikafuata nini?
Coplo Amani : Baada ya kumaliza kumuandika maelezo nilimjulisha Inspekta Joram na akanipa maelezo kwamba mtuhumiwa adhamimiwe na aripoti kituo cha polisi Ilomba na aripoti kila baada ya siku tatu.
Wakili: nini kilifanyika Tarehe 17 April
Coplo Amani : Tarehe 17 april 2025 nikiwa kituo cha polisi Ilomba nilipewa maelekezo na Inspekta Joram ya kuandika maelezo kama shahidi.
Wakili: Kingine?
Coplo Amani : Nilipewa maelekezo ya kumwandika kama shahidi kuhusiana na kile alichoeleza kwenye maelezo yake kwamba aliona mwenyekiti wake wa CHADEMA akihamasisha vurugu na kuharinubuchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba baada ya kuona kauli ile yeye kama mfuasi wa CHADEMA, alihamasika kutokana na kauli zile na alikua tayari kuwashawishi vijana wenzake kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Baada ya hapo?
Coplo Amani : Baada ya kumaliza kumuandika maelezo nilimjulisha Inspekta Joram.
Wakili: Ukafanya nini?
Coplo Amani : Hayo maelezo nilimkabidhi inspekta Joram.
Wakili wa Serikali : Waheshimiwa majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.
Part 216 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 214
Leo Mhe. Lissu ameingia Mahakamani akiwa amepiga Jeans na T-Shirt fulani hivi nyeusi yenye neno moja lililoandikwa kwa herufi kubwa "DUDA"
Kaka David Jumbe anasema DUDA ni neno la Kinyaturu ambalo maana yake ni mtoto ambae anapendwa sana.
Majaji wameingia,
Naona wanaandika kidogo pale juu.
Wakili wa Serikali anasimama, anasema upande wa Serikali wapo Kama walivokuwa asubuhi.
Wakili wa serikali: Shahidi anayefata sio shahidi wa kulindwa, anaitwa Coplo Amani.
Shahidi anaingia Mahakamani.
Jaji anamuuliza unaitwa nani?
Naitwa G9304 detective Coplo Amani
Una miaka mingapi: Nina miaka 35
Dini yako: Shahidi: mkristo
Kazi yako: Shahidi: mimi ni askari polisi.
Wakili wa Serikali : Toka lini?
Coplo Amani : Nimekua askari polisi tangu 2012
Wakili: unaifanyia wapi hiyo kazi?
Coplo Amani : Kazi yangu naifanyia mkoa wa Mbeya wilaya wa Mbeya mjini, kituo cha polisi cha kati Mbeya.
Wakili: Kituo gani?
Coplo Amani : Kituo cha Kati Mbeya nipo tangu 2012
Wakili: Una elimu gani ya Polisi?
Coplo Amani : Elimu yangu niliipata 2011-2012 ndani ya chuo cha polisi Moshi
Wakili: Ulivyohitimu ikawaje?
Coplo Amani: Baada ya kuhitimu mafunzo nilipangiwa Kituo cha Polisi Kati Mbeya Mkoa wa Mbeya.
Wakili: Kitengo gani upo?
Coplo Amani : Kituo cha Polisi Kati Mbeya nipo kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai
Wakili: Unafanya kazi chini ya nani hapo?
Coplo Amani : Nikiwa chini ya ofisi ya mpelelezi wa wilaya ya Mbeya kwa kifupi ni OCCID
Wakili: Kingine?
Coplo Amani: Katika ofisi hiyo nipo kama msaidizi wa shughuli zote za upelelezi ndani ya wilaya ya Mbeya mjini.
Wakili: Majukumu yako ni yapi?
Coplo Amani: Majukumu yangu ni kufanya doria, kupeleleza kesi zote za jinai, kukamata watuhumiwa wote wa makosa ya jinai na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa jinai
Wakili: Unakumbuka nini tarehe 04 April?
Coplo Amani : April 4, 2025 nakumbuka nilikua Kituo cha Polisi Ilomba ambacho kipo Wilaya ya Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbaya, hiki ni kituo kidogo cha polisi kinajulikana kama outpost
Wakili: Unajua nini kuhusu hicho kituo cha Polisi?
Coplo Amani : Kituo cha Polisi Ilomba kipo chini ya kituo cha polisi kati Mbeya.
Wakili: Nini kikaendelea?
Coplo Amani: Nilipewa maelekezo na Inspekta Joram, ambaye ni kaimu wa upelele Wilaya ya Mbeya mjini.
Wakili: Akakwambia nini?
Coplo Amani : Alinipa maelekezo ya kwenda Isyesye mtaa wa Mwamtengule ambapo alinieleza kwamba kuna watu wanapanga njama za kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Wakili: kingine?
Coplo Amani: Lakini pia alinipa namba ya simu kwamba niwasiliane na askari mwenzangu, ambaye yupo kitengo cha intelijensia ili aende akanionyeshe watu hao wanaojipanga kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Kazi yako inahusiana na nini?
Coplo Amani: Askari ambaye yupo intelijensi ni askari wanaofanya kazi ya kujichanganya na wananchi ili wapate taarifa mbalimbali za uhalifu.
Wakili: mnafanyaje kazi?
Coplo Amani: Askari wa intelijensia huwa wanajichanganya katika shughuli mbalimbali za wananchi, wengine ni bodaboda n.k ili kupata taarifa za makosa ya jinai.
Wakili: nini kilifuata?
Coplo Amani : Baada ya maelekezo hayo niliwasiliana na huyo askari tukakutana Isyesye mtaa wa Mwantengule
Wakili: Mkafanya nini?
Coplo Amani : Tulivyokutana akaniongoza na kunionyesha mtuhumiwa ambaye nilipaswa kumkamata.
Wakili: Kulikuwaje?
Coplo Amani : Pale kulikua na watu wengi tukapita kwa siri na akanionyesha mtuhumiwa katika kijiwe cha bodaboda akiwa na wenzake.
Wakili: Ukafanya nini?
Coplo Amani : Huyo mtu niliyetakiwa kumkamata ndiye aliyekuwa anahamasisha wenzake kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Part 215 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 213
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P9
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji hilo pingamizi la Wakili la Serikali halina maana yoyote, kwasababu shahidi mwenyewe amesema kwamba summons alipelekewa summons na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti ni ofisa wa serikali, lakini vilevile Mahakama haitaweza kujua kama huyu shahidi ni mkweli au ni muongo kwahiyo swali langu ni halali na ninaomba pingamizi lao litupitiliwe mbali, lakini huyo Mwenyekiti sio mtu ambaye amelindwa na sheria.
Katuga: Sisi tunaomba swali hilo shahidi asiulizwa kwasababu swali hilo litapelekea utambuzi wa shahidi huyu na kama tunavyojua humu ndani kuna wafuasi wake, researchers wake wanaweza wakaenda kumtafuta ili kumtambua shahidi huyu.
Mhe. Lissu: naomba ondoa hiyo kauli yako mimi sijazungumzia kuhusu wafuasi wangu humu.
Katuga: Naondoa hiyo ilikua ni by the way lakini msimamo wetu ni kwamba swali hilo shahidi asiulizwe
Mahakama: tunadhani uendelee na x-examination bila hilo jina.
Mhe.Lissu: Lakin waheshimiwa majaji mnaweza kuona namna cross examination yangu inavyokua limited lakini naomba niendelee.
Mhe. Lissu: shahidi umekujaje hapa
Shahidi wa kificho P9: nimependa bus
Mhe. Lissu: nani amekulipia nauli
Shahidi wa kificho P9 : nimejilipia mwenyewe
Mhe. Lissu: Umefikia wapi
Shahidi wa kificho P9 : Kwa ndugu yangu.
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama kuna kiongozi au mfuasi anajua kama unakuja kutoa ushahidi
Shahidi wa kificho P9: Ndio wapo baadhi
Mhe. Lissu: waliwahi kukutishia
Shahidi wa kificho P9 : ndio
Mhe. Lissu: unajua hilo ni kosa
Shahidi wa kificho P9 : hilo ni kosa la jinai
Mhe. Lissu: umewataja,
Shahidi wa kificho P9 : siwezi kuwataja kwa usalama
Mhe.Lissu: waeleze majaji kama ulitoa taarifa kituo cha polis
Shahidi wa kificho P9 : ndio
Mhe. Lissu: Kituo cha polisi kipi?
Shahidi wa kificho P9: Sasa nikitoa taarifa hiyo hapa si itakua navunja usalama?
Mhe. Lissu: Hebu jibu swali bwana tusisumbuane
Mahakama: Shahidi hebu jibu hilo swali
Shahidi wa kificho P9: Nilitoa kituo cha polisi Ilomba
Mhe. Lissu: Ulipewa RB
Shahidi wa kificho P9: ndio
Mhe. Lissu: umeitoa hapa mahakamani?
Shahidi wa kificho P9 : hapana
Mhe. Lissu: Polisi walichukua hatua gani?
Shahidi wa kificho P9: Walisema watafatilia
Mhe. Lissu: waambie waheshimiwa majaji kama kuna mtu yoyote amekamatwa
Shahidi wa kificho P9 : hapana
Mhe. Lissu: Waambie kama kuna mtu yoyote amepelekwa mahakamani:
Shahidi wa kificho P9 : hakuna
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Wakili wa Serikali: Leo tunashahidi mmoja, tunaomba break kidogo halafu tuje na shahidi mmoja aliyebaki, kwasababu jana hatukupumzika.
Mahakama: Mshitakiwa unasemaje
Mhe. Lissu: Tukienda kwa utaratibu huu tutachukua mida mrefu sana, Mahakama ilisema upande wa serikali ulete mashahidi wasiopungua watatu, kwanin hawajaleta hao mashahidi wengine.
Upande wa mashtaka wanatakiwa wawe na mshahidi wengine kama walivyotakiwa na Mahakama.
Katuga: Jana tulisema tutakuja na shahidi mmoja then twende kuargue application yetu, hatujaweza kuja na mashahidi wengi ili tupate muda wa kutosha kwasababu yeye alisema ana-objection.
Mahakama: Nadhani twende break fupi kwanza ili tukirudi tuendelee na huyo shahidi halafu tukimalizana nae mambo mengine yatafata.
Part 2014 itaendelea tukirudi.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 212
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P9
Mhe. Lissu: Shahidi umesema tarehe 4 april 2024 ukiwa na jamaa zako nyumbani kwako, “Tukawa tunajadili kauli ya Mwenyekiti kwamba tukichafue, ni kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Umewataja hao jamaa zako wakati unatoa ushahidi?
Shahidi wa kificho P9 : Hapana.
Mhe. Lissu: Wakati tunazungumza jamaa yangu akaniomba namba yangu ya simu, jamaa ambaye simfahamu, unakumbuka hayo maneno?
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nakumbuka.
Mhe. Lissu: inawezekana mtu usiyemfahamu kuwa jamaa yako, hiyo inaingia akilini!
Shahidi wa kificho P9: Inawezekana.
Mhe. Lissu; Na jamaa yako ambaye humfahamu akakuomba namba yako ya simu na ukampatia? Inaingia akilini?
Shahidi wa kificho P9 : ndio inaingia akilini.
Mhe. Lissu: ndivyo ulivyofundishwa na mapolisi.
Mhe. Lissu: Kwa vile unafanya kazi ya fundi umeme kwa malipo, una leseni ya biashara?
Shahidi wa kificho P9: Sina leseni ya biashara kwasababu sina ofisi
Mhe. Lissu: Una TIN number?
Shahidi wa kificho P9: Ndio
Mhe. Lissu: Umeionyesha?
Shahidi wa kificho P9 : hapana kwasabb haijahitajika.
Mhe. Lissu: Tarehe 5 April 2024 siku ambayo unakamatwa, unasema ulipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mteja, na ukasema tulipoonana akajitambulisha kuwa ni afisa wa polisi na akanionyesha kitambulisho chake, waambie waheshimiwa majaji kama unakumbuka jina la icho kitambulisho?
Shahidi wa kificho P9: Nakumbuka ni Vicent
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama hilo jina lipo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9: Halipo.
Mhe. Lissu: Hiyo tarehe 5 April 2024 uliandika maelezo kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: Na maelezo ya siku hiyo yalihusu uchochezi na kuzuia uchaguzi, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9: Kweli
Mhe. Lissu: Waambie majaji hiyo tuhuma ya uchochezi na kuzuia uchaguzi imeishia wapi?
Shahidi wa kificho P9 : Sijui
Mhe. Lissu: Waeleze majaji tangu tarehe 5 april 2024 umepelekwa Mahakamani kwa tuhuma hizo?
Shahidi wa kificho P9 : sijawahi kupelekwa
Mhe. Lissu: Waeleze majaji ulipoitwa polisi kwa mara ya pili 22 april 2025 kama ulielezwa tuhuma za uchochezi na kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa kificho P9: Ndio nilielezwa.
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako shahidi halafu tuonyeshe wapi uliuzwa juu ya tuhuma hizo
Shahidi wa kificho P9: Mimi nilieleza lakini wao hawakuandika.
Mhe. Lissu: Imekula kwako kwasababu wanasema haya ni maelezo yako.
Mhe. Lissu: Wewe ni shahidi kwenye kesi dhidi yangu, kweli si kweli.?
Shahidi wa kificho P9 : kweli
Mhe. Lissu: Na ndio maana umekuja kutoa ushahhidi jana na leo, kweli si kweli.
Shahidi wa kificho P9 : kweli.
Mhe. Lissu: Nikisema walikukamata tu ili uje kutia ushahidi dhidi yangu nitakua nakosea??
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sifahamu.
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama unajua kuwa hakuna kosa la kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa kificho P9 : ni kosa.
Mhe. Lissu: waambie majaji ni kwa mujibu wa sheria gani?
Shahidi wa kificho P9 : mimi sio mwanasheria.
Mhe. Lissu: ni sheria gani.
Shahidi wa kificho P9 ; Mimi najua kuzuia uchaguz kwa njia ya vurugu ni kosa lakini sheria gani sijui
Mhe. Lissu: Kama hujui sema sijui, sio kuleta ujuaji tu.
Mhe. Lissu: Kwani mimi nimeshatakiwa kwa kosa la vurugu.
Shahidi wa kificho P9 : umeshtakiwa kwa uhaini.
Mhe.Lissu: Shahidi ulikujaje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P9: Nilipanda bus
Mhe. Lissu: Nani alikwambia uje kutoa ushahidi
Shahidi wa kificho P9 : Nililetewa wito
Mhe. Lissu: nani alikuletea?
Shahidi wa kificho P9 : aliniletea Mwenyekiti wa serikali za mtaa.
Mhe. Lissu: anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P9 : Siwezi kukutajia kwasababu za kiusalama.
Katuga: sisi tunapinga hilo swali kwasababu za kiusalama. Kwahyo tunaomba hilo swali asiulizwe.
Part 213 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 211
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross examination Shahidi wa kificho P9
Mhe. Lissu: Waambie majaji kama tutafanya vurugu na kuuvuruga uchaguzi huo kama yapo kwenye maelezo yako…nasubiri jibu shahidi!
Shahidi wa kificho P9: Hayapo
Mhe. Lissu: Uliendelea kusema, alisema lazima tukichafue, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : kweli.
Mhe. Lissu: hayo maneno yapo au hapo.
Shahidi wa kificho P9 : sasa mbona unarudia maswali. hayapo.
Mhe. Lissu: Twende kwa yaliyotokea 22 April 2025, ulisema siku hiyo ulipigiwa simu na polisi kwenda Kituo cha Polisi Mwanjelwa.
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa soma pale palipoanzia na leo Tarehe 22 April 2025 mpaka nitakapokwambia basi…
Shahidi wa kificho P9 Anasoma…
Mhe. Lissu: Kwenye hiyo sehemu kuna sehemu kumeandikwa kituo cha polisi Mwanjelwa.?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli haijaandikwa
Mhe. Lissu: Na ukasema ulipofika walisema wanataka kukuhoji tena kwa matukio yaliyokuleta hapa.
Shahidi wa kificho P9: Kweli.
Mhe.Lissu : Waambie kama hayo maneno yapo kwa tukio lililokuleta hapa.
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana, ulisema nilihojiwa na mtu mmoja na mwingine alichangia kwa kuniuliza maswali mbalimbali, waeleze majaji kama hayo maneno yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Niliona clip ya Tundu Lissu ndio nikaanza, waeleze hayo maneno kama yapo katika maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9 : hayapo.
Mhe. Lissu: Sijamalizana na wewe, nataka ukitoka hapa ukawaeleze Mapolisi kwamba kule hakufai!
Watu wanacheka: 😂😂😂😁
Mhe. Lissu: Ulisema mimi kama mwananchama wa CHADEMA nilishawishika na kwamba nitafanya uasi, hayo maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P9: Yapo.
Mhe. Lissu: Sasa nataka uwaambie majaji kwamba wewe ni Mwanachama wa CHADEMA au sio?
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sio mwanachama wa CHADEMA.
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako na ushahidi wako wa jana, ulisema mwaka 2024 ulivutiwa na sera na kuamua kuwa mwanachama wa CHADEMA, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 :Kweli.
Mhe. Lissu: waambie majaji wafuasi wa CHADEMA huwa wanaandikishwa wapi.
Shahidi wa kificho P9: sifahamu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama wafuasi huwa wanatambulishwa wapi.
Shahidi wa kificho P9: Sijui
Mhe. Lissu: Waeleze kama huwa wanaalama usoni?
Shahidi wa kificho P9: Hapana
Mhe. Lissu: Na ulisema baada ya kuwa mfuasi ulishiriki katika matembezi ya amani, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa kama ulijiandikisha sehemu yoyote?
Shahidi wa kificho P9 : Hapana
Mhe. Lissu: Sasa shahidi hukuwahi kujiandikisha popote, huna alama yoyote kuwa ni mfuasi wa CHADEMA, waeleze majaji wataamini vipi kwamba wewe ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sijui hilo ni suala la amani.
Mhe. Lissu: Unasema tulihamasishwa kushiriki kongamano la vijana lililopangwa kufanyika Mbeya, waambie kama uliwahi kupewa mualiko wowote hata wa simu?
Shahidi wa kificho P9 ; hapana sikupewa mualiko wowote.
Mhe. Lissu: kama kiongozi wa chama aliwahi kukufata ili kukupa taarifa ya kongamano.
Shahidi wa kificho P9 : hawakunifata.
Mhe. Lissu: Kama hawakukufata inamaana hawakujui.
Shahidi wa kificho P9 : Sio lazima wanijue wote.
Mhe. Lissu: Kwa maelezo yako ya ushahidi ya jana, umesema ulisoma VETA Mbeya kati ya 2008-2010 ulipohitimu, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama umewasilisha cheti cha kuhitimu?
Shahidi wa kificho P9 : sijawasilisha kwasababu hakina umuhimu.
Mhe. Lissu: wataaminije? Kwasababu maneno matupu hayavunji mfupa.
Mhe. Lissu: Umesajiliwa kama fundi umeme wa majumbani na viwandani.
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nimesjiliwa.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama umeleta hati ya kusajiliwa?
Shahidi wa kificho P9: Hapana.
Part 212 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 210
Anaendelea Mhe. Lissu na Cross Examination.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba shahidi apewe kielelezo D13
Mhe Lissu: Jana kwenye ushahidi wako uliulizwa unaishi wapi na ukasema unaishi katika Halmashauri ya Mbeya, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: Naomba uangalie maelezo yako, nenda palipo andikwa makazi usome pameandikwa makazi yako wapi?
Shahidi wa kificho P9: Pameandiwa Mwakibete.
Mhe. Lissu: Kwenye mstari wa kwanza kabisa sema palivoandikwa hapo? Kwamba unaishi?
Shahidi wa kificho P9 : Pameandikwa Mwakibete lakin nilihojiwa Mbeya.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kwamba haya maeneo huwa yanatangazwa kwenye gazeti la serikali na waziri wa TAMISEMI
Shahidi wa kificho P9 : sifahamu
Mhe. Lissu: Umeonyesha gazeti la Serikali linaloonyesha Mwakibete ni Mbeya,?
Shahidi wa kificho P9; Hapana.
Mhe. Lissu: unafikri unaandika andika tu unaingizwa chaka na mapolisi na wewe unaandika tu.
Mhe. Lissu: Uliulizwa unafanya shughuli gani na ulisema unafanya kazi ya fundi umeme na kazi zako unafanya katika Halmashauri ya Mbeya, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako unafanya kazi gani?
Shahidi wa kificho P9 : Mkulima
Mhe. Lissu: Kazi ni mkulima hapa unajifanya fundi umeme, lugha gongana.
Watu wanacheka: 😂😂😂😂
Mhe. Lissu: nyie Waha wa kigoma wajanja sana nyie na mimi napenda watu wajanja kama wewe.
Mhe. Lissu: Uliulizwa unakumbuka kitu gani kilikukuta 2024, ukasema nilivutiwa na sera za CHADEMA na nikawanafatilia matangazo, mikutano n.k haya sasa soma maelezo yako mjanja wa Jiji la Mbeya…😁
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji hayo maelezo uliyosoma hapo kama yapo na ulivyosema jana
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo
Mhe. Lissu : Uliandika kwa mapolisi wakakupuuza wakaandika ya kwao.
Mhe. Lissu: Katika matukio mengi uliyofatilia ulitaja matembezi ya yaliyoongozwa na Lissu yalianzia Uyole, na Heche Isanga, mwambie jaji kama Mhe. Heche yupo katika maelezo kayo
Shahidi wa kificho P9: Nilieleza ni Mnyika sio Heche.
Mhe. Lissu: Jana ulisema Heche alianzia Isanga, unataka niwasumbue majaji wakusomee ulichokisema??
Shahidi wa kificho P9: inawezekana nilikosea
Mhe. Lissu: Kazi yangu ni kukamata watu waongo kama wewe.
Shahidi wa kificho P9 : Hiyo unasema ww
Mhe. Lissu: ndio nasema.
Mhe. Lissu: Ulisema mnamo tarehe 3 April 2025 ukiwa nyumbani kwako wakati unaperuzi mitandao kupitia simu yako aina ya Samsung 8 pro, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : kweli
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako waeleze majaji kama kuna mahala popote ulikua unaangalia mitandao kupitia aina ya Samsung 8 pro.
Shahidi wa kificho P9: hayajaandikwa.
Mhe. Lissu: Asante, mmeuzwa na mapolisi.
Mhe. Lissu: Ulisema kwamba uliingia kwenye mtandao wa instagram na ili uweze kuimgia instagram lazima uwe na simu janja, account na bundle, hayo maneno yapo au hayapo.
Shahidi wa kificho P9 : hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana ulisema wakati unaingia kwenye instagram uliona video ya Tundu lissu na ukasema huo mtandao umeusahau.
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nimeusahau.
Mhe. Lissu: Kama umesahau inamaana, kwenye maelezo yako utakua umeandika.
Shahidi wa kificho P9: Sasa wewe unaniuliza mambo waliyoniuliza mawakili.
Mhe. Lissu: Jibu swali langu. Unanifundisha namna ya kukuhoji?
Shahidi wa kificho P9 : Ndio hakuna
Mhe. Lissu: Uliulizwa muonekano wa Tundu Lissu, ukasema alikua ukumbini alivaa kombati za kaki za chadema na tshirt nyeusi na bendera ya taifa na rangi za CHADEMA, kweli si kwei?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa waeleze waheshimiwa majaji kama yapo katika maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9 : Hakuna
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana uliulizwa alisema atauzuiaje ukasema tutafanya vurugu na kuuvuruga uchaguzi huo.
Shahidi wa kificho P9: Kweli
Part 211 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.