Mafanikio ya Mtu hayategemei Maoni,Chuki,Wivu au kibali cha Watu wengine.Kubali kwamba kila Mtu ana Safari yake
Mafanikio ya Mtu mwingine hayahitaji Ruhusa yako,na Baraka za Mungu hazitolewi kwa kura za Watu
Watu watafanikiwa tu iwe unawapenda au huwapendi
Mungu si Mjomba wako.
“Kuna wakati utashinda na kuna wakati utashindwa
kuna wakati utaheshimiwa na kuna wakati utadharauliwa
kuna wakati utaaminiwa na kuna wakati utasalitiwa
kuna wakati utafurahi na kuna wakati utaumia
kuna wakati utasifiwa na kuna wakati utakosolewa
kuna wakati utaambiwa ukweli na kuna wakati utadanganywa
kuna wakati utapatia na kuna wakati utakosea
kuna wakati utapata faida na kuna wakati utapata hasara
Na hayo ndio maisha.”
Kuna Wakati kwenye Maisha unaweza kujihisi Umechoka sana sio kwasababu Umefanya kazi nyingi ni kwasababu Umebeba Vitu vingi unatabasam sehem ambayo ulitakiwa kulia📌