Kuna Wakati Kwenye Maisha Yetu Ambapo Tunamsahau Mungu Na Kufanya Mambo Yetu Bila Kumshirikisha. Ni Vyema Kufahamu Kuwa Safari Yetu Bila Mungu Haitaisha Salama. Hakikisha Kila Uendapo Mungu Awe Mbele Yako, Hutajikwaa Wala Kuanguka, Na Utafika Salama.
Kuna Yule Rafiki Huwa Yupo Muda Wowote Ukimuhitaji, Unamuelezea Changamoto Zako Anazibeba Kama Zake Na Anakushauri Bila Kusita, Na Hakutangazi Kwa Wengine. Hakikisha Kwa Gharama Yoyote Humpotezi, Rafiki Wa Hivyo Hapatikani Kirahisi.
Tunabeba Mambo Mengi Sana Moyoni, Tuombeane Na Kutendeana Wema Kila Wakati, Ni Ngumu Kujua Mtu Anapitia Mambo Gani Kama Hatutakuwa Watu Wa Kushirikisha Wengine Kwenye Matatizo Yetu Na Kama Hatutakuwa Watu Wa Kuyapokea Matatizo Ya Wengine Kama Matatizo Yetu. Depression Is Real.
Kuna Swali Unaweza Kuuliza Na Ukapewa Majibu Tofauti, Inategemea Tu Ni Nani Anauliza Hilo Swali. Mfano Mzuri Wa Maswali Yenye Majibu Tofauti Ni Kama โUpo Wapi?โ Na โUna Mchumba?โ.
Dada Yangu Hakikisha Bidhaa Yako Ina Thamani Sawa Na Bei Unayouza, Bidhaa Haina Matunzo Na Unaiuza Bei Kubwa Hutapata Wateja, Watabaki Kuulizia Bei Tu Kwako Ila Wanakwenda Kununua Kwingine Kwenye Bei Inayoendana Na Thamani Halisi Ya Bidhaa. Shusha Bei, Na Expire Date Inakaribia.
Mwenzako Ameshakuonyesha Dalili Zote Kuwa Mahusiano Yenu Yamefika Mwisho, Halafu Wewe Hutaki Kukubali Matokeo, Unaendelea Kusubiri Ukiwa Na Imani Kuwa Labda Atabadilika Baadae, Unapoteza Muda, Nguvu Na Pesa Kusubiri Jua Liwake Usiku. Amka Usingizini Kumeshakucha.
Wakati Unasubiri Abadilike Ili Uolewe Naye, Usiache Kuangalia Pembeni Pia, Usiache Kutoa Namba, Unaweza Kuta Huyo Unayemsubiri Ni Daraja Tu La Wewe Kumfikia Yule Wa Ndoto Yako.
@jemedarisaid Wewe Ni Boss Wa JKT Tanzania, Muda Kama Huu Ulitakiwa Kuwa Unaiandaa Timu Yako Ili Ifanye Vizuri Kwenye Ligi, Kuacha Majukumu Yako Na Kufuatilia Majukumu Ya Timu Nyingine Ndio Baadae Mkifungwa Mnasema Timu Pinzani Imenunua Mechi๐
Shida ya kua BROKE ile hali unajiskia kutokua na lolote la kufanya ndio inakumaliza.
Age inasonga hujioni ukitoboa umefulia, hadi mahusiano yanakua magumu bila sababu.
Na inakuja na hali ya unyonge hata ukiitwa kutoka unahofia kua mnyonge. Ogopa sanaaa
Kitu Cha Muhimu Kukifanya Kwa Mpenzi Wako Ili Awe Mgumu Kufanya Maamuzi Ya Kutaka Kukuacha Wakati Wowote Ni Kwa Kumuonyesha Kuwa Unaweza Kuishi Bila Uwepo Wake, Hata Kama Anajua Unampenda Sana.
@Elparton112 "Shule Ya Sekondari Mazengo Na Baadae Chuo Cha Ufundi Mazengo", Usahihi Ni Kwamba Hicho Ni Kitu Kimoja Kikiitwa "Shule Ya Sekondari Ya Ufundi Mazengo"
Ukiyumba Kimaisha Unakimbiwa Hadi Na Wale Uliotegemea Ndio Watakaokushika Mkono. Marafiki Watakuvumilia Watakuchoka Wataondoka, Ndugu Nao Dharau Zitaanza, Ikifika Kwa Mpenzi Wako Kukuacha Ndipo Unapogundua Kuwa Umepoteza Kila Kitu. Tupambane Wanangu, Mungu Yupo, Atatuheshimisha.
Amka Ukapambane, Usilale Ukisubiri Kusaidiwa, Usilale Ukisubiri Bahati, Misaada Huwafuata Wanaojishughulisha. Bahati Huenda Kwa Wasio Wavivu, Pesa Imekuwa Ngumu Sana, Utasaidiwa Ukionyesha Juhudi, Wape Sababu Ya Kukunyanyua Zaidi Kwa Kuanza Hata Na Hicho Kidogo Kwanza.
Kuna Haka Katabia Ka Hawa Watu Wetu Maarufu Mitandaoni, Kabla Hajawa Maarufu Atamfollow Karibu Kila Mtu Kwenye Social Medias, Jina Likishakuwa Kubwa Anamu-Unfollow Karibu Kila Mtu, Natamani Kujua Ni Kwanini, Ni Kulinda Brand Au Ndio Fasheni!?
Ulimwengu Umewafundisha Vijana Wengi Kuwa Wafanyabiashara Ambao Mwanzoni Hawakuwa Hata Na Ndoto Za Siku Moja Kuja Kuwa Wafanyabiashara. Wakati Ukipanga Yako Ulimwengu Nao Unakupangia Yake, Ndoto Yako Ikikukataa Nenda Na Ndoto Uliyopangiwa Na Ulimwengu, Cha Msingi Ni Mafanikio Tu.
Kuna Wakati Ni Bora Usimchunguze Ili Usijue, Kuna Mengine Ukiyachunguza Ukayajua Siku Hiyo Hiyo Maisha Yako Yanabadilika, Furaha Inaondoka Huzuni Inapiga Hodi, Uamuzi Ni Wako.
@GIVENALITY Nadhani Kitu Cha Msingi Mngewaomba Kwanza Msamaha Washabiki Wenu Waliotoka Mbali Na Wengine Kupata Ajali Kwa Ajili Ya Timu Lakini Matokeo Yake Mmewasononesha Zaidi Kwa Kufungwa Nyumbani, Safisha Kwanza Nyumbani Kwako Kabla Hujaanza Kulalamika Jirani Yako Mchafu!
Rafiki Akishindwa Kukusaidia Haimaanishi Kuwa Ameamua Tu Kutokukusaidia, Wengine Wanapitia Changamoto Ngumu Kukuzidi, Ni Vile Tu Hawajaamua Kukushirikisha, Na Hawajakushirikisha Wakiogopa Kukuongezea Mzigo. Kukasirika Kisa Hujapewa Msaada Ni Ubinafsi. Usinunie Watu, Jipambanie.