KARIBU NYUMBANI!
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara katika Tarafa za Ndago na Mgongo siku ya Jumamosi, Juni 13, 2026.
@mwigulunchemba1
Hongera Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha RUDN nchini Urusi.Hii ni uthibitisho wa mchango wako katika elimu,diplomasia na maendeleo ya Taifa.Tunajivunia kuona Nchi ikiendelea kung'ara Kimataifa
Nimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mhe. Agnes Nasania aliyekuwa Diwani Kata ya Shelui,kilichotokea Mei 30,2026 baada ya kuugua ghafla,Ninatoa pole kwa,familia ya Marehemu,ndugu,jamaa na marafiki.
"Mungu azidi kuwafariji wafiwa
Twiga akivuka barabara eneo la Mingela akitoka katika msitu wa Sekenke Tulya akielekea ziwa Kitangiri 1987.
Kutokana na uharibifu wa mazingira wanyama hao wamehama na hawapo tena katika msitu huo.
Juhudi ya Serikali kwasasa ni kulinda msitu huo.
#IrambaNkulu
Nimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Daudi Amos Mtoto wa katibu wa Mbunge Jimbo la Iramba Magharibi kilichotokea Mei 4,2026 baada ya kuugua kwa muda mfupi,Ninatoa pole kwa,familia ya Marehemu,ndugu,jamaa na marafiki.
"Mungu azidi kuwafariji wafiwa
Juni 15–21, 2026, Iramba kuwa mwenyeji Sekenke Marathon yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii
Mratibu wa shughuli za Jimboni na Msaidizi wa Waziri Mkuu, Christopher Hole, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wadau kushirikiana kuhakikisha mafanikio ya tukio hilo.
TUNAKUTAKIA TAFAKARI NJEMA YA IJUMAA KUU
Na iwe siku ya kutafakari, upendo na unyenyekevu, tukikumbuka sadaka ya Yesu Kristo kwa ajili yetu.
Amani, baraka na faraja viwe juu yako na familia yako.
#IjumaaKuu
KAMBI YA HUDUMA ZA MACHO BURE ��️
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA imeandaa kambi maalum ya huduma za macho:Uchunguzi,Upasuaji,Miwani naDawa
📍 Hospitali ya Wilaya ya Iramba
📅 4–6 April 2026
Huduma zote zitatolewa BURE!
EID MUBARAK
Mkuu wa wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda anawatakia waislamu wote na Watanzania kwa Ujumla Sikukuu njema ya Eid al Fitr, Tusherehekee kwa amani na utulivu.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Nazael Madede, Aliyepotea Machi 9 na kupatikana Machi 11 akiwa amefariki kwa ajali ya gari. Natoa pole kwa familia ya Marehemu,ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.
KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA WILAYA (DCC)
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleiman Y. Mwenda, anatarajiwa kuongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kitakachofanyika Ijumaa, Machi 6, 2026 saa 9:30 Alasiri katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.