Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Baba wa Taifa la Namibia Dr. Sam Nujoma ambaye amefariki dunia February 8, 2025, akiwa na umri wa miaka 95.
Rais Dkt. Samia amesema Nujoma alikuwa ni Mpigania uhuru, Mwanaukombozi na Rafiki mzuri wa Tanzania na wakati wa mapambano ya kuupata uhuru wa Namibia aliwahi kuishi Tanzania.
“Kwa niaba ya Serikali na Watanzania natuma salamu zangu za rambirambi kwa Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba, Mke wa Nujoma, Kovambo Nujoma, Watoto wa Marehemu, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Wanachama wa SWAPO”
#MillardAyoUPDATES