Msamaha hauimaanishi kwamba kilichotokea hakikuwa kibaya. Unamaanisha kwamba umeamua kutoruhusu maumivu ya jana yaendelee kutawala maisha yako ya leo. Unaweza kusamehe na bado ukaweka mipaka.
Kuna tofauti kubwa kati ya kuzeeka na kukomaa. Miaka inaweza kuongezeka bila hekima kuongezeka. Ukubwa wa mtu haupimwi kwa umri wake, bali kwa uwezo wake wa kujifunza, kusikiliza, kukubali makosa, kurekebisha kasoro na kuwaheshimu wengine.
Wakati mwingine sala yenye nguvu zaidi si ile yenye maneno mengi, bali ni moyo unaosema: Ee Mungu, sijui kesho yangu itakuwaje, lakini ninaamini hutaniacha. Imani ni kuendelea kujishikamanisha na Mungu hata pale ambapo hujui kwa hakika njia inayofuata.
Usisubiri upate kila kitu ndipo uanze kufurahia maisha. Kuna watu walikuwa wanatafuta maisha mazuri mpaka wakasahau kuyaishi kabla ya kufa. Thamini siku uliyonayo, watu ulio nao na nafasi uliyopewa.
Tusiharakishe au kulazimisha maisha kwa sababu ya kuona wengine wamefika kabla yetu. Kila mtu ana majira yake, safari yake na changamoto zake. Hata maua huwa hayachanui yote kwa wakati mmoja, lakini kila moja lina uzuri wake na linachanua kwa wakati wake!
Usipime thamani ya maisha yako kwa kile ambacho bado hujakipata. Kuna mengi uliyonayo leo ambayo wenzako wanayatamani. Shukrani haimaanishi kwamba huna ndoto kubwa. Shukrani inamaanisha unathamini ulichonacho wakati unaendelea na safari ya kuelekea unakotaka kufika.
Wakati mwingine Mungu hacheleweshi majibu ya maombi yako; anakutengeneza ili uwe tayari kuyapokea. Usikate tamaa kwa sababu mlango haujafunguka leo. Endelea kuomba, kufanya kazi na kumtumaini Mungu.
Ni siku mpya tuanaianza kwa Ishara ya Msalaba kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina. Ulinzi wa Mungu uwe pamoja nasi katika siku hii ya leo🙏💒
"Ufalme wa mbinguni utafanana na mtu atakaye kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.
Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.
Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano, tazama talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na uaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili, tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema mtumwa mwema na uaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wakeo.
Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; bali nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na ulegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
Basi mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele, lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno." (Mt. 25:14 – 30)
Neno la Bwana.
~Sifa kwako Ee Kristo.
Tujiandae kwa Ibada ya kesho.
Novemba 15, 2026, DOMINIKA YA 33 YA MWAKA 'A'.
SOMO 1: Mith 31:10-13, 19-20, 30-31
WIMBO WA KATIKATI
Zab 127:1-5
SOMO 2: 1Thes 5:1-6
INJILI: Mt 25:14-30.
Maandalizi mema & Dominika njema🙏
Kuna wakati utajikuta unafanya kila uwezalo, lakini mambo bado hayaendi kama ulivyotarajia. Usikate tamaa. Si kila ukimya ni kukataliwa, wala si kila kuchelewa ni kushindwa.
Wakati mwingine maisha yanakufundisha subira kabla hayajakupa kile ambacho umekuwa ukikiomba.