Unapitia wakati mgumu kiuchumi japokuwa kila siku unapambana?, ndugu usikate tamaa kama unapambana na mambo ni magumu hivo vipi ukiacha?
Au kata tamaa tu ukitaka kama unae mtu wa kukuletea mkate mezani, sisi wenzio kukata tamaa mwiko
“Tanzania hakuna uhaba wa kazi, kuna uhaba wa ajira. Wengi wenu hamtaki kufanya kazi, mnataka kuajiriwa, mkishapata hizo ajira mnabweteka hamfanyi kazi” Mchungaji Dkt Kimaro.
#MeiMosi
HERI YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI
Mungu wetu ni mtenda kazi, na sisi inatupasa kutenda kazi.Ndio maana kuna laana kwa wafanyao kazi kwa ulegevu (Yer 48:10).
Ukiwa mchapa kazi, unafanyika baraka kwa dunia.
Ninakuombea Mungu abariki kazi ya mikono yako,na uwe nuru kwa wengi.
Kutoka 33:14 “Bwana Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha”
Ninakuombea wiki hii, uso wa Mungu uende pamoja nawe, naye akakupe raha na kufanikiwa sana katika kazi za mikono yako na maisha yako kiujumla.
Mungu akubariki
NUKUU YA LEO: “Mafanikio ni bahati. Kadri unavyojituma kwenye ubunifu, kutafuta maarifa, uthubutu na uvumilivu ndio bahati yako inaongezeka.” - Ruge Mutahaba
Ukiwa mwenye haki, Kila utendalo litafanikiwa na utazaa matunda yako kwa wakati na wala hautanyauka (Zab 1:3)
Asubuhi ya leo ninakuombea Baraka za Mungu ziambatane nawe, na nguvu zake zikutenge na kila mauti katika maisha yako na kazi za mikono yako.
Akupe kustawi sana. Amen
Unapoianza wiki yako Mpya siku ya leo, ninakukumbusha, kuongeza thamani kila iitwapo leo. Wewe sio wa kawaida, usifanye vitu kikawaida kawaida, Add Value! Hakikisha unapanda bei
Mungu na akubariki sana