MO29 ni siku ya kuutafuta uhuru wetu sisi wenyenchi kutoka mikononi mwa genge la watekaji,watesaji,wapoteza watu, wezi, mafisadi,wabambika kesi,wahujumu uchumi,waporaji/wauza rasilimali zetu, madikiteta uchwara, na wahatibu nchi
The Time Has Come
The Time is MO29
HATUNUNUI HOFU
AMETEKWA! AMETEKWA! AMETEKWA!
Naomba kushare nanyi huu ujumbe kama nilivoupokea.👇👇👇
Huyu anaitwa Rodrick Kakwaya ni Mwalimu wa Usevya Secondary iliyopo Mkoani Katavi na Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe lakini pia aliwahi kuhudumu kama Makamu Mkuu wa shule akiwa hapo Usevya Sekondari.
Mwalimu huyu alitekwa siku ya Tarehe 30 Septemba mida ya usiku katika makazi yake hapo Usevya,nyumba wanazoishi walimu hazipo mbali na shule,hivyo alitekwa kama alivyotekwa Mdude Nyagali mbele ya mke wake na watoto.
Mwalimu Kakwaya alikuwa Mwanaharakati na Mtetezi wa haki za Binadamu na msimamo wake haujawahi kuyumba tangu nimfahamu.
Taarifa hii nimeipata jana kutoka kwa mtu niliyesoma naye na nikajaribu kufanya mawasiliano huko Usevya ili nipate uthibitisho na nimethibitishiwa kwamba taarifa hii ni ya kweli na Ndugu wameenda vituo mbalimbali vya Polisi lakini mpaka sasa hawajafanikiwa kumpata Ndugu yao mpaka sasa.
Nimearifiwa kwamba Mwalimu Kakwaya alikuwa Mkosoaji wa Mfumo hususani katika Magroup ya WhatsApp.
Huyu ni Mwalimu wangu alinifundisha wakati ule nasoma Advance pale Usevya hivyo namfahamu vizuri hajawahi kuwa na shida na mtu,ni Mwalimu mpole sana asiye na makuu,Mwanafunzi yeyote aliyesoma pale Usevya anaweza kukubaliana na hili lakini hata mtu anayeishi yale mazingira anaweza kuthibitisha hili jambo hivyo kosa lake ni kutoa maoni yake kuhusu mfumo.
Hakuna kosa linalostahili adhabu ya kutekwa,Tanzania ni yetu sote,tujifunze kuwa na uvumilivu wa kisiasa.
Ujumbe wa Mwenyekiti Tundu Lissu (Sehemu ya Kwanza)
“Ndugu zangu,
Kwa wiki kadhaa sasa nimewekwa kwenye total isolation — upweke wa kulazimishwa. Wale wafungwa wenzangu waliokuwa nami kwenye selo moja, ambao walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, wametolewa wote; nimeachwa peke yangu.
Selo yangu sasa imewekwa kamera za ufuatiliaji (CCTV) zinazorekodi kila kitu ninachofanya, hadi wakati ninapokojoa au kubadilisha nguo. Sina faragha yoyote tena. Hili si suala la usalama bali ni kudhalilishwa kwa utu wangu kama binadamu.
Naomba jambo hili lipigiwe kelele kwa nguvu zote, kwa sababu ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu na ni kosa kisheria chini ya Kanuni za Umoja wa Mataifa za Matunzo ya Wafungwa (Mandela Rules), ambazo zinasema wazi kuwa:
• Utu wa binadamu unabaki kuwa wa heshima hata akiwa gerezani (Kanuni ya 1),
• Upweke wa muda mrefu au unaomnyima mfungwa mawasiliano ni ukatili na mateso (Kanuni ya 43 na 44).
Pia ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 12 na 13, zinazolinda hadhi ya mtu na kumzuia kuteswa au kudhalilishwa.
Niko tayari kuvumilia hali yoyote kwa ajili ya imani yangu katika haki na uhuru wa watu wetu, lakini udhalilishaji wa utu wa binadamu hauwezi kukubalika — si kwangu tu, bali kwa yeyote anayebeba jina la mwanadamu.”
🗣Dikteta Kashusha Karibia VPN zoote Usiku wa Kuamkia leo...
Tafadhari Msitaje Majina ya VPN maana Wahuni wakiona tu Wanashusha...
ni Vyema Umfate mtu Direct umuombe Kuliko Kutaja...
Just Imagine Kwenye VPN kumi nilizo nazo 3 tu ndio zinafanya Kazi...
Tarehe 29, Tusiogopee ✊
Tatizo sio LULU bali kile alichokuwa akipigania; hivyo dawa sio kumtisha, kumpa ujumbe asome au kumbonga akae pembeni. Ili kumalizana na watu wa aina hii ni kushughulikia kile wanachosimamia ambacho ndicho wananchi wanachotaka. Sasa Lulu amekaa pembeni kaibuka huyu mkali zaidi.
FREE JOHN HECHE NOW…!!
Kama nchi imewashinda kuiongoza kwa HAKIna KATIBA, semeni tujue moja… Ila sio kwa INCOMPETENCE na UONEVU huu wa Raia ambao sio tu wana exercise haki zao bali mnapaswa kuwalinda!
Tujuzeni kama tunaongozwa na utawala wa KIIMLA au kama Tanzania ni POLICE STATE!!
Serikali na Vyombo vya Usalama ndio chanzo cha kuleta Taharuki nchini alafu ndio wa kwanza kuhubiri kuhusu AMANI (wakati msingi wa Amani ni HAKI). Wananchi hawapewi taarifa kwa wakati, Wananchi wanatekwa, hakuna usalama wa Wananchi na Mali zao… Wananchi wanauwawa, na hakuna ufuatiliaji, mrejesho, wala matokeo ya hitimisho!! Na Viongozi wa Upinzni wanawekewa zengwe na Usumbufu usio na kichwa wala miguu…
#FreeHECHE #Now
Lugha za kiCAG kuna wakati zinataka D mbili
Lazima kufukuze kwanza KICHECHE kwa usalama wetu kisha ndio tukae kutengeneza mambo
Tatizo la dharura kwa sasa ni kicheche kinapita sana na kuku
sasa wewe ifike 29 ubaki ndani
Kwenye msafara wa Samia kwa mujibu wa hii clip kuna magari yamebeba pesa nyingi sana , nyingi
Wanafanya uharifu wa cyber kuna watu wana mifumo ya kuingilia simu za Watu , mtu amelipia mabilioni ya pesa hili apate mawasiliano ya simu ya mkewe
Wanafanya udufuzi wa masimu kama hawana akili nzuri
Jeshi mpo? Mjue na nyie mnadukiliwa na hawa wahuni kama sisi
Nilipokuwa nakula leo, mhudumu alinijia akaniambia kwa hisia, “Mh, tafadhali mpe Lissu hii pesa, anunue maji ya kunywa.” Niliguswa sana!
Vitendo vidogo kama hivi vinatukumbusha kuwa bado kuna watu wenye mioyo safi. Tujali, tupende, tusambaze wema.
UJUMBE WA MATESO KUTOKA KWA MH. TUNDU LISSU AKIWA GEREZANI UKONGA.
“Ndugu zangu,
Kwa wiki kadhaa sasa nimewekwa kwenye total isolation “upweke wa kulazimishwa”
Wale wafungwa wenzangu waliokuwa nami kwenye selo moja, ambao walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, wametolewa wote nimeachwa peke yangu.
Selo yangu sasa imewekwa kamera za ufuatiliaji (CCTV) zinazorekodi kila kitu ninachofanya, hadi wakati ninapokojoa au kubadilisha nguo.
Sina faragha yoyote tena. Hili si suala la usalama bali ni kudhalilishwa kwa utu wangu kama binadamu.
Naomba jambo hili lipigiwe kelele kwa nguvu zote, kwa sababu ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu na ni kosa kisheria chini ya Kanuni za Umoja wa Mataifa za Matunzo ya Wafungwa (Mandela Rules), ambazo zinasema wazi kuwa:
•Utu wa binadamu unabaki kuwa wa heshima hata akiwa gerezani (Kanuni ya 1),
•Upweke wa muda mrefu au unaomnyima mfungwa mawasiliano ni ukatili na mateso (Kanuni ya 43 na 44).
Pia ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 12 na 13, zinazolinda hadhi ya mtu na kumzuia kuteswa au kudhalilishwa.
Niko tayari kuvumilia hali yoyote kwa ajili ya imani yangu na msimamo wa wananchi katika haki na uhuru wa watu wetu, lakini udhalilishaji wa utu wa binadamu hauwezi kukubalika, si kwangu tu, bali kwa yeyote anayebeba jina la mwanadamu.
#REPOST UJUMBE UFIKE MBALI
KIPEPERUSHI CHA UDSM kimepata majibu kutoka kwa UDASA.
“Hakuna mahala popote Tamko la UDASA limesema kilichosemwa na UDASA ni msimamo wa UDSM wala viongozi wake ambao ni wanachama wa UDASA”
Soma tena hapo juu. Kuna nondo MBILI hapo hawa jamaa kweli ni wasomi sana. Yani WAMEMPASUA ANANGISYE Makamu wa chuo na kipeperushi chake kaonekana kweli ana uprofesa wa “JALALANI” kama alivyosema KABUDI.
Asante sana UDASA kuendelea kusimama upande wa wananchi zama hizi za giza hakika TUTAWAKUMBUKA na heshima yenu kutoka kwetu mmeipata.
Huyo KIBAKA ANANGISYE kiufupi sana kaambiwa AACHE SHOBO.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Baada ya tarehe 29.10.2025 maandamano kufanikiwa, Warioba atakua rais wa Mpito amalizie kazi aliyoianza kuweka nchi hii katiba mpya na kuandaa uchaguzi wa kwanza wa kweli wa vyama vingi!