#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 497
Jaji Nduguru anasema, pia tunasukumwa hivyo na kifungu cha 10 cha Kanuni ya adhabu kuwa nia ya mtu lazima iambatane na matendo ya dhahiri ya mshtakiwa na sio maneno tu.
Kwa mtazamo wetu dai kwamba upande wa utetezi walifanya kwa lengo la kushinikiza Serikali kufanya mabadiliko haimaanishi ni kuwa ni kuitishia Serikali ni msimamo wetu kuwa kesi ya upande wa mashtaka imeegemea zaidi katika maoni kuwa maneno ya mshtakiwa yalilenga kuitishia serikali.
Mahakama inaamua kuwa sio lazima provocative speeches zinaweza to constitute kosa kwa maana zinalenga kuhamasiha mabadiliko hivyo sio lazima ziwe kosa la jinai.
Hatujapata ushahidi wa moja kwa moja ukiachia ushahidi wa namba 1,2 na 16 ambao ni tafsiri zao, sisi tunaona kutokuwa na ushahidi tunasema kwamba maneno hayo sio kwamba yanapelekea uhaini.
Tunajua kuwa Serikali ina wajibu wa kusimamia uchaguzi, sheria na hivyo maneno yanayo desrupt election yanaconstitute kosa la uhaini.
Hoja ya tatu na ya mwisho ambayo ni ambayo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo ya kuchochea umma kuvuruga uchaguzo kwa lengo la kuitishia serikali.
Tukiangalia ushahdi wa Jamhuri hasa namba 1,2 na 16 ambao waliegemea kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na walisema kusambazwa kwa maneno hayo kulifanywa kupitia mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mshtakiwa na watu waliokuwepo kwenye mkutano huo, shahidi namba 17 alieleza kwamba matukio hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma kuhusiana na msimamo wa No reforms, No election.
Upande wa mashtaka wanaeleza kuwa kwa kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na mshtakiwa kukiri kuwa aliongea maneno hayo basi mahakama ione kuwa upande wa mashtaka umethibitisha publication hata kama hakuna picha mjongeo.
Upande wa utetezi ulieleza kuwa sio Lissu aliyesambaza maneno hayo, na kukosekana kwa video hakuna uthibitisho kuwa Lissu alichapisha.
Tunakubaliana na Lissu kuwa hakuna ushahidi kuwa yeye ndio alichapisha na kusambaza hayo maneno kwenye YouTube ya Jambo TV.
Kitendo cha kuonekana tu kwenye Jambo TV sio lazima kuwa Tundu Lissu ndiye aliyepandisha kwenye Jambo TV.
Tumeona kwamba upande wa mashtaka wamethibitisha kwamba kauli hiyo ilitolewa na mshtakiwa, na kuwa ilisambazwa na mshtakiwa alitoa hotuba hiyo katika umma sio kwa kificho hivyo kauli za mshtakiwa hazikuwa kauli za siri.
Mahakama hii inaona kwamba kauli hizo kupandishwa kwenye mtandao wa Jambo TV haimaanishi kuwa Lissu ndiyo aliyepandisha.
Hivyo basi kutothibitisha uhusika wa Lissu kuchapisha maneno hayo kwenye Jambo TV upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha element za kosa. Kwa kitendo cha kutokutolewa video clip does not defeat ushahidi wa mdomo ambao ulitolewa na shahidi wa 17 ambaye alikuwepo na mshtakuwa hapingi maneno hayo.
Kutokana na ushahidi uliopo, upande wa mashtaka hawajatupa ushahid kuwa Lissu alilenga kutenda kosa la uhaini.
Failure kuleta ushahidi hoja ya tatu inakuwa pia haina mashiko, treason per see kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) haijathibitishwa na kifungu hiki hakina minor offence lakini ni jukumu la ku evaluate ushahidi na kuona kama kuna kosa dogo.
Kwa mujibu wa kifungu cha 319(1-2) cha CPA kinaelekeza mahakama kwamba inaweza to substitute kosa pale ushahidi unapoonyesha kwamba kunaweza kuwa na kosa dogo.
Part 498 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
KUTOKA MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM
Siku ilishaanza mapema sana hapa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es salaam.
Ukumbi ulishajaa tangu saa 12 asubuhi lakini humu ndani wamejazwa askari kanzu na vipenyo wa kutosha kwenye kila Benchi ili wanachama wetu wakose pa kukaa.
Tofauti nan siku zote, leo jengo la Mahakama limesafishwa ni safi kuliko siku zote, na pale njee ya geti la Mahakama wanachama wengi wanaondolewa na kufukukuzwa toka saa moja asubuhi na kuambiwa ukumbi umekwisha kujaaa.
Saa saa mbili na robo Mchungaji Msigwa na Mzee Hashim, Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Unguja wamefanya maombi kwa niaba ya Dini zote.
Benchi ambalo huwa wanakaa viongozi wakuu wa Chama yaani Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Wajumbe wa Kamati Kuu leo limekaliwa na maaskari lote. Sijui watakaa wapi na nia yao ni nini?
Leo Wapo Mawakili kama 30 hivi humu ndani wa upande wa Mhe. Lissu. Wamekuja kuonesha solidarity na Wakili mwenzao yani Mhe. Tundu Lissu.
Mawakili waliopo kwa haraka haraka ninaowaona pale ni-;
1. Dr. Nshala
2. Mpale Mpoki
3. Jebra Kambole
4. Paul Kisabo
5. Edson Kilatu
6. Peter Madeleka
7. Maduhu William
8. Gaston Garubindi
9. Doris Kafuku
10. Nashon Nkungu
11. Sisty Masawe
12. Emmanuel Chengula
13. Deogratias Mahinyila
14. Emmanuel Ukashu
15. Matojo Cossotta
16. Hekima Mwasipu
17. Ikoti Lissu
Familia ya Mwenyekiti Lissu pia nao wamefika hapa Mahakamani, wakiongozwa na Dada ake lakini leo ni tofauti na siku zingine wako katika hali ya majonzi kwasababu ya msiba wa Mzee wetu Allute, nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu na awasaidie katika hili.🙏
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
As an American constitutional lawyer, I have personally litigated cases defending the rights to free expression and due process. These are fundamental principles of human liberty. For that reason, I am closely following the outcome of Tundu Lissu’s trial proceedings, and the broader implications for the rule of law.