5. UVUMILIVU NA UTHUBUTU
Kilimo kina changamoto zake kama mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa, magonjwa, au kushuka kwa bei ya soko
Usiingie kwenye kilimo ukitegemea kupiga hela tu, inahitaji ujenge nidhamu, ujifunze kutokana na makosa ya msimu wa kwanza.
MTAJI WA AKIBA
Wakulima wengi wanahesabu mtaji kuwa ni kukodi/kununua shamba, mbegu, na mifumo ya umwagiliaji.
Kuna gharama zaidi kama vile, mafuta ya pampu ya maji, vibarua wa kupalilia, kupiga dawa na ununuzi wa mbolea. Hakikisha una mtaji wa akiba wa kuendesha shamba.
@Nalimasaumu Zingatia mwenendo wa bei sokoni katika mwaka. Hivyo, utapanda kitunguu ukikusudia uvune wakati ambapo bei zinakuwa nzuri sokoni ili kuepuka hasara.