SHAABAN NA NGUGI - Dizasta Vina ft. Kaa La Moto
Oyaaaaa!! Shaaban na Ngugi, si ile track ya kuweka tu speaker ikalia halafu unaendelea na shughuli zako.
Hii ni ile ngoma ambayo ukikaa chini ukaipa sikio, unaanza kugundua layers zake moja baada ya nyingine.
Yaani Vina na Kaa La Moto wamechukua kalamu ya fasihi, wakaichomeka kwenye microphone, halafu wakaiachia ipige freestyle ya maisha.
Kwanza kabisa, title yenyewe ina uzito. Shaaban Robert na Ngugi wa Thiongโo si majina ya kubahatisha. Hawa ni watu wa kalamu, watu waliotumia lugha kama silaha ya kufikiria, kuhoji jamii na kumzungumzia Mwafrika.
Sasa Vina na Kaa wameichukua hiyo spirit na kuipeleka kwenye rap. Ni kama kizazi cha vitabu kimekutana na kizazi cha mic.
Vina kwenye hii track anaonekana kama kawaida yake ni architect wa story. Hajaanza kukimbizana na punchline kila baada ya sekunde mbili.
Yaani ana build scene, anaweka picha, anaunganisha dots na anakupa muda wa kutafakari. Hii ndiyo strength yake kubwa, niseme ni conceptual writing.
Unasikia kama anasimulia story lakini nyuma ya hiyo story kuna thesis. Yaani kuna kitu anataka ukifikirie, uumize ndonga na hapa ndipo Vina huwa anakuwa tofauti na rapper anayejua tu kurusha mistari.
Vina anajua kuandika wimbo kama screenplay. Kuna setup, kuna development, kuna payoff.
Anaweza kuanza kwenye kitu kidogo halafu akakufikisha kwenye idea kubwa bila hata kugonga breki.
Lakini sasa Kaa La Moto anaingia... Hapo ndipo moto unawashwa si kitoto.
Kaa hana ile delivery ya kuomba nafasi, yaani naingia kwenye beat kama tayari ni kwake.
Yaani kuanzia Cadence yake, pocket yake, articulation yake na projection yake vinafanya verse yake iwe na character tofauti kabisa.
Yaani unahisi rapper yupo ndani ya beat, sio kwamba beat ipo chini yake. Pia Kaa ana kitu kingine muhimu sana kwenye hiphop niseme ni presence.
Kuna rappers wanaandika mistari mizito lakini wakifika kwenye mic, moto unakufa kwa Kaa ni tofauti.
Huyu mwamba anachukua mstari, anaupa pressure, anauweka kwenye pocket, halafu anauacha uanguke. Na hapo ndipo delivery inakuwa sehemu ya lyrics.
Naweza sema Kaa hakariri verse, anaishi verse na hiyo ndio sababu verse yake inaweza kukufanya urudishe ngoma nyuma hata kama umeshaisikia mara tatu.
Kwenye beat, hawa wawili wamepata nafasi ya kuonyesha tofauti zao. Tempo ikiwa juu, bado hawajakimbia ovyo oyaaaa wametulia kinyama.
Wanajua breath control, wanajua pauses, wanajua kusisitiza neno na wanajua kuacha nafasi beat ipumue. Hiyo ndiyo tofauti kati ya nimeandika mistari mingi na nime master rap performance.
Kuna pia ile technique ya switching cadence, yaani kubadilisha flow bila kupoteza pocket. Hapo ndio unagundua kuwa rap sio maneno pekee ila ni rhythm, timing, emphasis, tone na attitude.
I went to Tanzania as a Kenyan and quickly discovered two things, X is restricted and Arusha is nothing like what I expected. From chips mayai and serious minji culture to 1,000 TSh stage fares here are a few things that caught me off guard.๐งต๐ฐ๐ช๐น๐ฟ
Usiweke kikomo cha maombi yako kwa sababu unafikiri wewe ni mwenye dhambi au hustahili.
Hauombi kwa sababu ya wewe ulivyo; unaomba kwa sababu ya Mungu alivyo na rehema na upendo wake kwako hauna mwisho.