Huyu hajui kwamba nchi wapinzani wa Apartheid ya Afrika Kusini ikiwemo TZ, walisusia Olimpic 1976, Montreal, km silaha ya kupinga ubaguzi kiasi kwamba Filbert Bayi akapoteza nafasi pekee ya kushinda dhahabu! Michezo ni siasa, siasa ni maisha!!!!!
Watu wanapiga kelele wanasema watanzania tumuunge mkono Nchimbi kwenye kudai katiba mpya, kwanini wasimwambie Nchimbi atuunge mkono sisi?
Maana yeye ametukuta tuko kwenye mapambano kitambo!
Picha hii ni ya mwaka 1998, nikiwa na Shyrose Sadrudin Bhanji mjini Arusha wakati tukihudhuria Semina ya Waandishi wa Habari za Michezo iliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), iliyofunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Wakati huo, Shyrose alikuwa mwandishi wa habari wa Daily News, nasi tulikuwa vijana wenye ndoto kubwa, tukijifunza, tukijenga uwezo na kuamini kuwa siku moja juhudi zetu zingezalisha matunda.
Leo, tunapoangalia tulipotoka na tulipofika, tunatambua kuwa mafanikio hayaji kwa bahati. Yanajengwa hatua kwa hatua, kwa nidhamu, uvumilivu na kujifunza kila siku.
Kwa vijana wanaochipukia sasa, msikate tamaa mkiona waliofanikiwa leo. Fahamuni kwamba hakuna aliyeibuka ghafla. Kila mmoja alianza mahali fulani, akapitia changamoto, akajifunza na akaendelea kusonga mbele.
Safari ni hatua. Endeleeni kujifunza, kufanya kazi kwa bidii na kuamini katika ndoto zenu. Siku moja nanyi mtakuwa ushuhuda kwamba mwanzo mdogo unaweza kuzaa mafanikio makubwa.
WANAOSEMA KUWA KWA SABABU SHAURI LA MHESHIMIWA LISSU LIKO MAHAKAMANI, HAKUNA ANAYEPASWA KUMSHAURI Mhe RAIS ALITAFUTIE UFUMBUZI WANAKOSEA. Hapa inabidi tuelimishane zaidi na kwa uwazi. Tusichanganye dhana mbili tofauti: uhuru wa Mahakama na wajibu wa Serikali.
Mahakama zina wajibu wa kutoa maamuzi kwa uhuru, bila kuingiliwa na mtu yeyote hata Rais. Huo ni msingi wa utawala wa sheria na lazima uheshimiwe.
LAKINI NI SERIKALI KUPITIA VYOMBO VYAKE NDIYO HUANZISHA NA KUENDESHA MASHITAKA YA JINAI. Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), mamlaka ya mashtaka yanaweza kupitia upya uamuzi wa kuendelea na shauri pale yanapoona kuwa maslahi ya umma au haki yanahitaji hivyo. Kwa hiyo, kumshauri mhe Rais ahimize Serikali yake kupitia upya uamuzi wa kuendelea na mashitaka ya jinai ambayo yanachukua muda mrefu au kuleta sintofahamu katika taifa si sawa na kuiamuru Mahakama iamue kwa namna fulani. Kusema vinginevyo ni kupotosha umma. Kuna wanaofanya hivyo kwa kutokujua. Kuna wanaofanya hivyo kwa hila ovu kama propaganda tu ya upotoshaji. Tusichoke kuelimishana.
Hata taarifa ya hivi karibuni ya Commonwealth Ministerial Action Group (CMAG) haikuitaka Mahakama imwachie huru Mheshimiwa Lissu. Badala yake, ilishauri suala hilo "lipatiwe ufumbuzi kupitia njia za kisiasa na kisheria." Hii inaonyesha kwamba hata katika demokrasia zilizoimarika, KUNA WAKATI SULUHISHO LA MIGOGORO YA KISIASA HUPATIKANA KWA KUTUMIA TARATIBU HALALI ZA KISHERIA PAMOJA NA BUSARA ZA KISIASA. Mimi ninaamini athari za kuendelea kumshikilia Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani kwa shitaka ambalo kwa mwaka mzima sasa halijakamilika mahakamani haisaidii taifa hili hata kidogo.
Mhe Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wassira (MTANI) kweli tulidiscuss. Kwa kuwa umeweka wazi maongezi yetu basi uniruhusu na mimi niongezee ufafanuzi for the record. Kwanza “tulikubaliana kutokubaliana”. Rai yangu kwa mhe Rais siyo shinikizo kwake wala kuingilia Mahakama. Silazimishi chochote kwani ninajua sina mamlaka hayo. Ni ushauri na ombi kwa uongozi wa Taifa kwa ujumla wake kwamba swala la Lissu na wengine wa aina hiyo likamilike. Serikali ndiyo inashitaki huko Mahakamani. Ikiondoa shauri, kama ilivyofanya mara nyingi huko nyuma kwa busara, tutapiga hatua ya mengine yanayotusubiri kuponya majeraha kwa kutenda haki, kuridhiana na kuweza kuandika Katiba Mpya katika hali ya kuaminiana. Mamlaka ya kuondoa shauri mahakamani iko chini ya mhe Rais na Serikali yake kupitia ofisi ya DPP. Ni kwa kutambua hilo ninajielekeza moja kwa moja kwa Mhe Rais. Na ninaendelea kufanya hivyo kwa unyenyekevu mkubwa. The stakes my MTANI are too high. The difference is that some can see the danger, others cannot. The burden of knowledge.
Pour rappel, la sélection haïtienne 🇭🇹 n'a pas eu le droit de jouer avec un maillot qui rappelait symboliquement la bataille de Vertières décisive avant l'indépendance du pays car la FIFA a jugé que cela était un "message politique"
C'est à la carte ou à la volonté de la Maison Blanche désormais la "politisation" à la FIFA...
Maridhiano mnayojadili ni kati ya nani na nani? CCM na CHADEMA? CCM iko Polisi, CHADEMA iko Ukonga. Sasa tufanyeje? Tuwafungulie CCM kutoka Polisi na CHADEMA toka Ukonga, ndipo tutapata fursa ya maridhiano ya aina yoyote!
Kwamba hawajui tofauti ya ‘documentary na coverage ya kawaida ya taarifa!? Kuna two sided and balanced story kwa documentary ? Yaani persona life experience inakuhitaji nini wewe @MsigwaGerson
#BBCAfricaEye profiles Tanzanian opposition leader Tundu Lissu as he fights treason charges, for which he could face the death penalty.
Watch the documentary, Tundu Lissu: A Fight Too Far? 🎥 https://t.co/s9pF5KAhXL
@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
Je vous prépare une très grosse enquête sur la mafia du football argentin demain matin 🇦🇷
Probablement l'un des plus gros scandales couverts par la FIFA ces dernières années d'ailleurs
The racist, dehumanising remarks against @KMbappe by Paraguayan Sen. Celeste Amarilla are despicable, regrettably not isolated.
States & sports organisations must prevent acts of racism & discrimination, and ensure independent and effective accountability. Social media must also prevent and address racial discrimination on their platforms.
https://t.co/TVawwmw3Qo
Tundu Lissu anashikilia rekodi ya kufunguliwa mashtaka mengi! Hakuna mashtaka dhidi yake yanayohusu kujinufaisha binafsi; yote yanahusu mawazo na msimamo wake kuhusu maslahi ya jamii pana! Ndiyo kusema huyu ni raia mwema tu aliyepewa na Mungu wake karama ya kutumikia ubinadamu!