@EduTalkTz Wachina husema"Speak of Cao Cao,and Cao Cao arrives".
Wazungu husema"Speak of the devil"
Wazee uchaggani walisema"Kokumbuo Rumu shinga numba(Ukimkumbuka Chui,funga mlango)"
Waswahili wakasema"Ukitaja nyoka,shika kigongo".
Kesi fake ya Uhaini,wasishangae Wahaini wa kweli wakitokea
Mhe. Lissu Mungu kampa karama nyingi ambazo katika ulimwengu wa leo watu wa aina yake ni wachache sana.
Huyu tunatakiwa kukumbuka kumuombea kila siku kwenye sala zetu maana ni hazina kwa nchi yetu.
Sisi hatuna silaha za kutosha kumlinda ila tuna Mungu ambae tukiomba anasikia na anajibu.
Tukiomba Mungu ampe ulinzi hakuna silaha yoyote ya watesi wake ambayo itafanikiwa kumdhuru iwe sirini au hadharani.
#FreeTunduLissu
"Tuendelee kushikilia msimamo wa #NoReformsNoElection, kwa kufanya hivyo tutaiondolea CCM uhalali katika uchaguzi huu." Mhe. Susan Lyimo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema (BAZECHA)
Mkapa alimshitaki Lissu mara ya kwanza 2002.
Kikwete alimshitaki mara tatu.
Magufuli alimshitaki kwa kesi sita, alikamatwa mara nane.
Alichaguliwa Urais TLS akitokea kortini Kisutu.
Samia amemkamata mara 3. Sasa amempa uhaini.
Katika yote, hajawahi kutwa na hatia. FreeLissu
Hadi sasa CDM kinapambana na:
Mbogamboga
Artifical opposition
Genge la freeman
Polisi & dola
Hata hivyo, hayo makundi yote yataangukia pua.
Hiki ni kipindi muhimu mno. Wananchi wanafahamu nani tapeli, laghai na enabler wa uhai wa dola katili.
Tutashinda tusipozimia roho.
Hata katika kesi ya kwanza ya uhaini Tanzania, mwaka 1970, washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa saba na walikuwa wanaletwa Mahakamani na askari waliovaa kwa unadhifu. Hawakuficha sura zao kwa soksi.
Miaka 55 imepita, mwaka 2025, askari wa magereza wanamleta kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, mahakamani wakiwa wamevalia vitambaa kuficha sura na nyuso zao. Unajua ni kwanini?
James Hadley Chase anasema “the guilty are afraid” - wenye hatia wanayo hofu). Hofu ya uovu. Wanaogopa macho ya watu baada ya kuvua sare za magereza. Wanatakiwa kuishi na binadamu wengine mtaani.
Hata wao, hao askari magereza, wanajua kwamba, Tundu Lissu sio mhaini. Wao wanatekeleza maelekezo ya watawala tu. Wanaficha sura zao kwa kuwa wanajua UMMA unawashangaa. Wakijulikana, watachekwa.
Miaka 55 iliyopita, kesi ya kwanza ya uhaini Tanzania ilipokuwa ikiendeshwa, askari hawakuficha sura kwa kuwa walikuwa na ushahidi na upelelezi ulikuwa umekamilika. Hawakuwa na sababu za kujiziba sura.
Kesi ya uhaini aliyopewa Tundu A.M. Lissu ni kesi ya kwanza Duniani kusikia mtu anayetuhumiwa kutenda uhaini yupo pekee yake; alikula njama mwenyewe; alipanga mwenyewe; tena alipanga uhaini YouTube.
Muda mrefu wengi wanafikiri nchi yetu inatawaliwa na chama cha siasa, wao wanakiita ‘CCM’. Wakati wengine wachache walishaanza kuhoji kama CCM ni chama cha siasa kabla mfumo wa vyama vingi kurejea….
Ukisoma ‘The State and the Working People in Tanzania’, kilichohaririwa na Prof. Issa Gulamhussein Shivji na kuchapishwa mwaka 1987, utagundua kuna wasomi walishaanza kuhoji uhalali wa CCM.
Watu timamu walishaanza kuhoji kama kweli CCM ni chama cha siasa. CCM siyo chama cha siasa tena. Ndiyo maana kinaogopa kushiriki uchaguzi na wanapora mchakato wa uchaguzi hata wa vijiji na vitongoji.
Chama cha siasa kimewekwa madarakani na nguvu ya kura za wananchi, hakiwezi kuogopa wapinzani wake na kutumia njia za uongo kuzuia wasifanye shughuli za kisiasa. Hicho chama hakifanyi tena siasa..
Chama kinachofanya siasa hakiwezi kumshikilia gerezani siku zaidi ya 112 kwa uhaini usiokuwa na ushahidi kiongozi mkuu wa chama cha upinzani miezi michache sana kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Chama cha siasa huongoza kwa hoja za kisiasa, sio kwa bunduki, mizinga na mabomu na magereza. Chama cha siasa hushinda mijadala ya kisiasa kwa kutumia ushawishi wa nguvu ya hoja za kisiasa na kiitikadi.
Chama cha siasa kinakwenda kwa wananchi kuwashawishi wakiunge mkono kwa falsafa na itikadi zake, hakijifichi nyuma ya vyombo vya ukandamizaji vya na kuwatisha wananchi. Hutumika nguvu ya hoja…
Chama cha siasa kilichofilisika, ambacho hakiwezi kuuza sera kwa umma, ambacho kinategemea kupora mchakato wa uchaguzi kinaanzisha vyama vya mfukoni vitashiriki uchaguzi kuwapa uhalali wa kisiasa…..
Zamani sana, CCM walikuwa wanatuita wapinzani, hususani CHADEMA, vyama vya msimu vinavyosubiri uchaguzi ndio tufanye kazi ya siasa. Sasa hivi wao ndiyo wanatukataza kufanya kazi ya siasa, wametuzuia...
MaCCM sasa ndiyo chama cha msimu. Hakkwezi kufanya siasa. CHADEMA ndiyo chama cha siasa. MaCCM yanamshtaki Tundu Lissu kwa uhaini ambao hakuna ushahidi na hawataki kupeleka ushahidi wao…
Hawataki kesi iende Mahakama Kuu kwa kuwa hawana ushahidi na vielelezo kuthibitisha tuhuma zao za uhaini ambao ulitokana na askari wao kupiga doria mtandaoni na kusikia maneno ya Tundu Lissu, YouTube….
Agenda ya UMMA ni #NoReformsNoElection, imepokelewa na kueleweka ipasavyo. Hii ndiyo agenda ambayo inafanya CCM na DOLA yao wanaishambulia CHADEMA, viongozi na wanachama wake wote.
Tukishinda vita hii ya sasa, ni kwa hakika, watesi wetu hawatakuwa na silaha nyingine yoyote itakayokuwa imebaki. Tutashinda. Hatua zote hizi ni kuwaogopesha wafuasi wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla…
Hasta la Victoria Siempre.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Mchungaji unapaswa kumuogopa Mungu na si serikali. Huu ni msiba, si mkutano wa chama tawala. Ni mahali pa kutoa pole na kuenzi maisha ya Albert na kuzungumza kwa uhuru. Umechagua kufunga midomo ya wafiwa, lakini Mungu hawezi kufungwa. Kilio cha watu wa Mungu hakiwezi kunyamazishwa na kofia ya uchungaji iliyogeuzwa kuwa kifuniko cha unafiki.Kama mchungaji huwezi kusimama upande wa waliodhulumiwa, basi ni heri ukae kimya kuliko kutumika kama kipaza sauti cha watesi.
Yesu hakuwa mpatanishi wa uonevu alikuwa na hasira dhidi ya wanafiki, akawafukuza hekaluni kwa sababu waligeuza ibada kuwa biashara. Wewe umegeuza msiba kuwa jukwaa la kuzima harakati. “No Reforms, No Elections” si matusi ni wito wa haki. Ni kilio cha watu wanaotaka katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, uhuru wa maoni na haki ya kuchagua viongozi wao kwa amani. Ningekuwepo hapo msibani ningekuambia acha kuongea kama mtu MPUMBAVU asiyejua maandiko.
Ntobi acha UJINGA ukikwisha elimika zamani tena CPA holder unakuwa na mambo ya kipuuzi namna hii?
Amekuwa Mwenyekiti wa chama for twenty five (25) years he knows everything ndani ya Chama he’s a live central committee member haya yote ambayo CDM wanayapitia kwanini akae kimya?
Kindles kushupaza shingo kwa UBISHI kuhusu hili la MWAMBA kutelekeza CDM na kusababisha maumivu yote wanayopata CDM basi utakuwa umevuka level ya UJINGA na sasa wewe ni MSHENZI!
Kwa Gen Z,wanachama, wapenzi na wafuasi wapya TUIJUE CHADEMA kwa pamoja.
Tuifaham historia ya CHADEMA.
Tuelewe kwanini tunasema CHADEMA NI IMANI.
Tuwafikishie na salamu wanaohisi CHADEMA itakufa kuwa CHADEMA IMEJENGWA, HAIKUIBUKA KAMA MRADI 📌
@ChademaTZ2#NoReformsNoElection
Tukiwa Igunga wakati wananchi wanachangia tone tone, pamoja watu kuwa wengi wanasukumana mwishoni alikuja mzee mmoja wa umri mkubwa ambae kwa makadirio ana miaka 90+.
Huyu mzee akatoa sh 2,000 ambayo alikua ameifunga kwenye karatasi na ilikua pesa pekee.
Tukio hili liligusa sana hisia zangu maana ukimuona yule mzee ni kama alitoa kila kitu alichokuwa nacho.
Najua kuna wengi na mama mwingine pia alitoa hivyo tukiwa Serengeti.
Kisa hiki nakifananisha na ule mfano wa yesu kwenye biblia akimzungumzia mama alietoa kila kitu.
Huyu mzee alinigusa sana ikabidi nimpe sh 100,000.
Tunawashukuru sana Watanzania kwa jinsi mnavyojitolea kupigania mabadiliko.
Asanteni sana wote.
#NoReformsNoElection
Tafadhali mwimbaji mkuu wimbo huu awasiliane nami.
Nimesikiliza nyimbo tatu mpaka sasa za #NoReformsNoElection lakini kwangu huu mpaka sasa ni wimbo bora kuliko zote.
https://t.co/w2mzejrnQo
Ikiwa kuna wimbo mwingine wa #NoReformsNoElection naomba link yake iwekwe hapa pia.
Nishukuru wasanii wote mnaotumia nguvu ya sanaa anuai katika mapambano ya kuhakikisha #BilaMabadilikoHakunaUchaguzi .
Zaidi ya nyimbo ni kazi ipi ya sanaa imekuvutia zaidi kwa namna ilivyofikisha ujumbe wa mabadiliko na haki mintaarafu kuwezesha #Tanzania inakuwa na uchaguzi huru na haki?
Nakuombeni mlio na BUSARA mmuambie huyu Sheikh Makanzu akae KIMYA. Asiingilie DINI ya wenzetu wala asiwaambie cha kusema Makanisani mwao.
Sijawahi kumsikia Padre wa Kikatoliki kuwambia Waislamu salaam za Eid zitolewe vipi!
Huu UCHAWA utatuweka pabaya!
Tito Magoti, Human rights lawyer: The East Africa community needs a new dawn where our voices are heard. In Tanzania, the situation is alarming. As citizens we need to go to the streets and ensure that we retain our position in the governance of the country
#CitizenWeekend