Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na viongozi mbalimbali kwenye hafla ya uapisho wa Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2026.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye picha na Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2026.
Timu ya mpira wa volleyball ya wanawake ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeibuka mshindi wa tatu katika mashindano ya SHIMISEMITA2026 baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Kahama MC.
Ujenzi wa bwawa kubwa la kuhifadhi maji ya mvua pamoja na mtaro wenye urefu wa zaidi ya kilomita 3.6 umeanza kutekelezwa katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane wa Dkt. John Malecela, hatua inayolenga kudhibiti mafuriko katika eneo la Nzuguni na kuyageuza maji hayo kuwa fursa.
Jiji la Dodoma limetakiwa kuandaa orodha ya maeneo yote yaliyotolewa vibali vya uchimbaji wa madini ya ujenzi. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri katika kikao cha maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua za El Nino.
Timu ya Mpira wa Mikono ya Wanaume kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetwaa ubingwa wa mashindano ya SHIMISEMITA yanayofanyika jijini Mbeya, baada ya kuicharaza Halmashauri ya Wilaya ya Geita magoli 9-6 katika mchezo wa fainali.
Wataalamu wa afya kutoka Kituo cha Afya Kizota wamefika katika Shule ya Msingi Kizota, Kata ya Kizota, Jiji la Dodoma, kutoa chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 0 hadi miaka 10 ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo na madhara yake.
Timu ya Mpira wa Pete ya Watumishi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanza kwa kishindo mashindano ya SHIMISEMITA baada ya kuichapa Timu ya Halmashauri ya Mondalu DC kwa magoli 52–6 katika mchezo uliochezwa leo Uwanja wa Shule ya Sekondari Mbeya.
Ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania,Gerson Msigwa katika Soko la Wazi la Machinga ambalo ni moja ya mradi unaosimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
WAZIRI NANAUKA ATEMBELEA BANDA LA JIJI LA DODOMA SABASABA, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba na kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali