๐ก๐๐๐๐จ ๐ช๐๐ญ๐๐ฅ๐ ๐ ๐๐จ๐จ ๐๐๐จ๐ก๐๐จ๐ ๐๐ข๐ก๐๐๐ ๐๐ก๐ข ๐๐จ๐จ ๐๐ ๐๐๐ฆ๐๐ฌ๐๐ก๐ฆ๐ ๐๐ ๐ฏ๐ฎ ๐๐ ๐ก๐๐ ๐ฅ
Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua Kongamano Kuu la Mwaka la Kisayansi la 32 katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambalo limewakutanisha watafiti 516 kutoka nchi mbalimbali.
Dk. Biteko amemwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ambapo amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na mchango wa tafiti za kisayansi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisayansi zinazochangia kuchochea maendeleo ya nchi.
โโSerikali inayoongozwa na Rais Samia inaamini katika tafiti za kisayansi na inaamini pia kuwa hakuna maendeleo bila utafiti na hivyo ili kupata mafanikio ni lazima tufanye utafitiโโ, amesema Dk. Biteko.
Amesisitiza โโKama mnavyofahamu kupata maendeleo ya mahali popote ili matokeo yaonekane lazima kuwe na utafiti wa kisayansi na uweze kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali kwa hivyo maendeleo yoyote bila utafiti yatakuwa ni maendeleo ya kubahatisha, na kama ni ya kubahatisha kutakuwa na kukosea kwingi matokeo yake kutakuwa na matumizi ya rasilimali nyingi zaidi kabla ya kupata jibu sahihi jambo ambalo lingeepukika, hivyo wataalamu hawa wako hapa kujadili tafiti mbalimbali katika sekta ya afya mfano chanjoโโ.
Aidha, Dk. Biteko amesema kuwa Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya afya na itaendelea kuunga mkono tafiti za kisayansi huku akiziasa taasisi za utafiti kushirikiana katika tafiti kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali ili kuchangia maendeleo ya nchi.
Sambamba na hilo, Dkt. Biteko amesema Serikali imewekeza vya kutosha kwenye utafiti katika sekta ya afya ili kuwa na ugunduzi wa ndani ya nchi โPamoja na kwamba tunahitaji watu kutoka nje lakini na sisi wenyewe tunaweza kuwa na wagunduzi wetu wa ndani na tumeshaanza, unaweza kuona zipo dawa tunazalisha wenyewe na hata chanjo, ni lazima tuwe na tafititi zinazotusaidia wenyeweโ. Amesema Dkt. Biteko
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Molel amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanza kutoa kipaumbele katika masuala ya utafiti kwa lengo la kuwajengea uwezo watafiti wa ndani ya nchi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazohitaji utafiti wa kisayansi mara zitakapotokea.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya NIMR ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema kuwa Taasisi hiyo imekuwa na ushawishi mkubwa ndani na nje ya nchi kupitia tafiti zake mbalimbali inazofanya akitolea mfano utafiti wa matumizi ya dozi moja ya chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi
uliofanywa na NIMR mkoani Mwanza.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. John Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesem kuwa tafiti zinazofanywa na NIMR ni ulinzi tosha kwa mwanadamu, hivyo kuona mkutano mkubwa wa kisayansi unafanyika katika jiji la Dar es Salaam ni ishara njema ya kujali afya na ulinzi kwa watu wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla. Pia amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika Tafiti za Afya ya Mwanadamu.
Naye, Mkurugenz Mkuu wa (NIMR), Prof. Said Aboud amesema kuwa NIMR imekuwa ikiendesha makongamano kwa kushirikiana na wadau ambayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha sera za afya pamoja na kufanya maamuzi yanayosaidia kuboresha huduma za afya nchini.
Aidha Prof. Aboud amesema katika kongamano hilo watafiti wataketi kwa siku tatu, watawasilisha maada mbalimbali na kufanya majadiliano na mwisho wa siku watakuja na mapendekezo ambayo yatawasilishwa Serikalini kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma za afya.
Awali, Dk. Biteko ametembelea mabanda ya maonyesho ya utafiti ikiwemo vifaa vya maabara vya kupima magonjwa mbalimbali kama kifua kikuu, malaria na tafiti za dawa za tiba asili.
Something new, big & exciting is #ComingSoon! Watch out for a call for #PhD applications on the Sewankambo Training Program for Global Health Security in Africa. Check for updates on this via @IDIMakerere & THRiVE's socials & #website. BE THE FIRST TO KNOW!
#AcademicTwitter
Much appreciation to @NIMRMbeya, a Centre with a calm research environment, extensive collaboration networks, high-tech laboratory infrastructure and committed scientists ๐ฌ
I am indeed fortunate to be part of this team and to contribute to its success ๐
#Ndagafijo#Kaziiendelee
1/3 A huge congratulations to our very own Dr.Ruby Mcharo on achieving her PhD!Her dedicated research delved into estimating the prevalence & identifying risky behaviours pertaining to sexually transmitted infections(STIs) among young adults attending Higher Learning Institutions
#Congratulations Drs. @RoberoDK & @DorynRuby on graduating with doctorates of @kcmucotz. It's a prestigious degree that requires years of studying & researching. You've done a good job! THRiVE is proud of you.
Here's to the next chapter of your life.๐ฅ๐๐ฅณ
The Provost of KCMUCo congratulates all students who have graduated today and argue all students to work harder and take this event as the beginning of a great milestone and not a moment of relaxation.
@NNtinginya@EDCTP Thank you very much Dr. Nyanda, I have seen higher and above from the shoulders of the giants like you
I am grateful for your guidance and support
Thank you @edctp for the opportunity to attend and experience the 11th EDCTP Forum in Paris ๐จ๐ต
Indeed this is a celebration of the spectacular achievements of the program for two decades & beyond
The inspiration for young and mid-career scientists is beyond words
#edctpforum2023