Kuna watanzania hawakupenda mbinu za Mzee JPM kushinda chaguzi 2019 na 2020, lakini kwa CCM hiyo ndio mbinu pekee iliyobaki kama tunataka dola.
Rais Samia akitaka kubaki na dola na wabunge wengi lazima afanye kama JPM alivyofanya 2019/20 ingawa leo wanamtukana.
Serikali ni chombo cha wananchi walichokiunda ili kiwaletee maendeleo. Inapotokea chombo hiki kinakuwa mali ya familia fulani au kikundi fulani, maana ya serikali haipo tena.
Hadi leo hii utoaji wa taarifa za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 haujakamilika. Wazee ni wangapi, Watoto ni wangapi? Kata fulani ina watu wangapi? Bado haijulikani.
Walitaka kumtoa Uwaziri Mkuu Ndugu yangu Kassim Majaliwa ili wamuweke mtoto wao pendwa lakini mtoto haoneshi uwezo hata kwenye masuala madogo ya wizara.
Tatizo la wazee wa CCM hawawajengi vijana wao kiuongozi, wanaamini nafasi zao zina nguvu ya kuwapa vijana dola.
Deni la serikali ni kubwa sana. Ndani ya mwaka mmoja tumekopa Tsh. Trilioni 30 na hakuna cha maana kinachoonekana. Gharama ya maisha imeongezeka maradufu. Na bado hiyo mikopo italipwa na kodi za wananchi.
Wakati wa Mzee JMP sauti ilikuwa kubwa na mambo makubwa yalionekana. Sasa hivi tuna kelele nyingi na kinachofanyika hakionekani - pamoja na mikopo ya matrilioni.
Inasikitisha baadhi ya viongozi wa CCM na serikali sasa wanaonesha hadharani kupingana na Mzee JPM na kuchafua jina lake wakati akiwa hai waliufyata mkia.Hiki kiwango cha unafiki ni kikubwa mno.
Kama Rais wangu @SuluhuSamia anakubalika kwa kiwango kikubwa, kwanini wapambe wake hawataki wengine wachukue fomu ya urais 2025?
Kama anakubalika woga wa kushindana unatoka wapi?
Kwa kauli yake ile ya watu wazuri hawafi, na kutaja mifano ya Jakaya na Kinana, moja kwa moja kaka yangu Yusuph Makamba alimaamisha Waliokufa, akina Mzee JPM, Mzee Mkapa, Balozi Mahiga, Balozi Kijazi, Jaji Ramadani, nk walikuwa watu wabaya.
Kaka Makamba atafakari kuomba radhi.
CCM imerudi kumilikiwa na watu wachache ambao ndio wanufaika wakubwa wa Rasilimali za Taifa. Kuna kazi kubwa ya kufanya kukirudisha chama kwa wananchi.
Bila shaka mmeshuhudia wazee wa familia chache zinazotafuna nchi walivyojipambanua kule Dodoma. Wakatangaza na maazimio ya Mama agombee 2025 ili woanekane wanampenda sana - kumbe wanapalilia malisho ya familia.
Bado natafakari mkutano mkuu wa Chama chetu ulivyotawaliwa na majungu, uongo na fitina. Wengine wakadiriki kuonesha furaha yao hadharani kwa kifo cha Mzee wetu JPM.
Tatizo ni;
-umeme
-maji
-gharama za maisha.
Katikati ya hayo hakuna kuupiga mwingi.
Lakini tunaweza kuimba anaupiga mwingi ili watoto wetu waendelee kula.