KAMPENI YA AFYA YA AKILI NI AFYA YAZINDULIWA RASMI
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Bi. Ziada Sellah amezindua rasmi Kampeni ya kitaifa ya Afya ya Akili ni Afya, yenye lengo la kuongeza uelewa juu ya afya ya akili nchini ili kuhakikisha kila mwananchi ana ustawi wa akili.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNMH, Dkt. Paul Lawala, amevitaka vyuo vikuu kuwa mabalozi wa afya ya akili, akizungumza UoI & RuCU wakati wa kampeni ya Afya ya Akili ni Afya Mkoani Iringa.
🎖️ UoI yatunukiwa tuzo ya mchango wa kitaaluma!
#AfyaYaAkiliNiAfya#MentalHealthAwarenessMonth
Wote mnakaribishwa kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani ambayo itakuwa tarehe 10 October 2024.
Fanya usajili wako wa kushiriki kupitia Link hii: https://t.co/gFr8DEg13w
Mimi nimeshajisajili nawe, Karibu Ujisajili ili tushiriki wote. Tena na Hakuna Kiingilio!
Meet Damas Mlaki @DamasMlaki, a neuropsychiatrist from Tanzania 🇹🇿 and #AtlanticFellow. He's driving efforts to improve dementia care by engaging stakeholders, boosting primary health care, and creating equitable interventions. @atlanticfellows@UCSFmac
https://t.co/x0eJ95X5Rb
Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Jijini Dodoma imesema zipo tabia nyingi kwenye Jamii ambazo Watu huzifanya zinazoashiria wana changamoto ya afya akili au magonjwa ya akili ikiwemo ku-bet, kunywa pombe na kutumia simu kupita kiasi, kutoridhika na kukosoa kila kitu, kuona kila Mtu ni mbaya na hakupendi, kutukana na kucomment vibaya mitandaoni, kuogopa kupanda ndege, lift n.k ambapo imesema Mtu akijiona na viashiria hivi anapaswa kuwahi Mirembe ili apewe ushauri au dawa badala ya kusubiri hadi apelekwe akiwa amefungwa kamba.
Akiongea na @AyoTV_ , Mtaalamu Bingwa wa Saikolojia na Afya ya Akili amesema “Kuhusu ku-bet Watu wanataka kuongeza kipato lakini Wataalamu wa Afya ya Akili tunajiuliza iweje Mtu afikirie maisha yake anaweza kumudu kwa kubahatisha?, Mtu huyu tunaanza kutilia mashaka akili yake, Mtu anachukua hela ya ada, mshahara wake wote kwenda kubet, kubobea kwenye ku-bet ni uraibu (addiction) na hawa pia tunawahudumia kama Warahibu wa dawa za kulevya”
“Pombe kupita kiasi ni tatizo mpaka Mtu akikosa pombe anatetemeka, Mtu kupata furaha kupita kiasi na akiwa na hela ananunua hata asivyohitaji na kutoa ofa kwelikweli ni tatizo, kuna Mtu kila Mtu ni mbaya anaona kila Mtu hampendi ofisini hadi nyumbani, una haja ya kuchunguzwa”
“Magonjwa ya akili yanazidi 300, kuna magonjwa ya wasiwasi ikiwemo Mtu ghafla anapata mshtuko moyo, kuogopa kusimama mbele za Watu kuzungumza, kuna Watu wanaogopa kupanda lift au kukaa vibaraza vya maghorofa pekee yao, uoga kupanda ndege, Mtu akipoteza hali ya kupenda vitu alivyokuwa akivipenda siku za nyuma mfano outing na ghafla anajitenga au kujiona hana thamani na hata kufikiria bora kufa, huu ni ugonjwa wa akili”
“Mtu anapojiona ana changamoto ni vizuri akaja Mirembe kuliko kufikiria wewe ni mzima ukabaki Mtaani halafu ukaletwa siku umefungwa kamba, kuhusu ubalozi tunatumia Watu wenye ushawishi kama Mh. Jokate ambao afya zao za akili zipo vizuri ili watusaidie kupeleka elimu kwenye Jamii kwahiyo sio kweli Mtu tunayemtumia akawa ana tatizo na hata walio-comment vibaya kuhusu ubalozi wa Mh.Jokate nao wanafaa kuchunguzwa afya yao ya akili, lindeni afya zenu za akili”
#MillardAyoAUPDATES
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga fedha katika Bajeti ya Mwaka 2024/25 kwa ajili ya kujenga chuo kikubwa na cha kisasa cha Afya - Mirembe cha uuguzi na ukunga kitakachokua na vifaa vya kisasa ambacho kitatoa wataala wa kutosha katika Sekta ya Afya.
Waziri @ummymwalimu amesema hayo leo Juni 12, 2024 alipofanya ziara katika chuo cha Afya - Mirembe kwa kujionea hali ya chuo hicho pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa chuoni hapo.
"Serikali imeona ipo haja ya kuongeza idadi ya wataalam wa Afya ya akili nchini Tanzania kwa kujenga Hospitali kubwa pamoja na kuanzisha kozi ya mafunzo ya diploma ya juu ya uuguzi katika afya ya akili ili kuboresha upatikanaji wa wataalam wa afya nchini ambapo wanafunzi watakao soma kozi hiyo kunufaika na mikopo kutoka Bodi ya Mikopo Tanzania." Amesema Waziri Ummy
"Lengo letu ni kuhakikisha tunazalisha wataalam wa Afya ikiwemo wauguzi na wakunga wenye sifa pamoja na ujuzi walio pikwa wakapikika na wanaozingatia maadili ya kazi." Amesisitiza Waziri Ummy
Tamasha is a fellow-led intergenerational, Intercultural, interdisciplinary and international arts and health festival of the Global Arts in Medicine Fellows across the world. ‘Tamasha’ is a Swahili word for festival and we are delighted about its activation by GAIMF Cohort 6
GSAHW 2023 INTERNATIONAL CONVENING Registration is Live!
Join us for one week on arts & health engagement,scientific research emerging innovative solutions to health care in the global south
Sept. 23-30
Register for the online & on-site event via https://t.co/eoCLBiXvrG