Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Mussa Juma Assad, ameibua mjadala mitandaoni baada ya kutoa kauli kuhusu suala la vijana na mahusiano, akisema kijana anayepata kipato hapaswi kutumia fedha zake “kuhonga” mwanamke.
Prof. Assad alitoa kauli hiyo alipoulizwa kuhusu kijana anayepata kipato cha shilingi milioni moja kwa mwezi anatakiwa kutenga kiasi gani kwa ajili ya kuhonga, ambapo alijibu kuwa kijana huyo hapaswi kutoa fedha hata senti moja kwa ajili ya jambo hilo.
“Hatakiwi kuhonga kabisa, mtoto wa kike achukue hela kwa baba yake na kaka zake. Wewe kama mtu wa nje usitoe hela kwa mtoto wa kike,” amesema Prof. Assad.
Kauli hiyo imezua mjadala miongoni mwa wananchi, huku baadhi wakijadili nafasi ya fedha katika mahusiano ya sasa, wajibu wa mwanaume na mwanamke, pamoja na namna vijana wanavyopaswa kusimamia vipato vyao.
Wewe unaonaje kauli ya Prof. Assad? Je, vijana wanapaswa kuacha kabisa kutoa fedha katika mahusiano au kuna tofauti kati ya kuhonga na kumjali mwenza?
Weka maoni Yako na shirikisha wengine Taarifa hii.
Pamoja na kuwa Tanzania ina haki ya kuwa na mahusiano ya kirafiki na nchi yoyote duniani kwa kadri inavyowezekana, kwa maoni yangu safari ya kuelekea Moscow imefanyika katika wakati ambao si muafaka kisiasa na kidiplomasia.
Katika kipindi ambacho Marekani na Umoja wa Ulaya tayari wameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa nchini Tanzania, hususan baada ya matukio ya Oktoba 2025, malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wa upinzani, jambo la mwisho ambalo Tanzania ilihitaji ni kutuma ujumbe unaoweza kutafsiriwa kama kuhamisha mwelekeo wake wa kimkakati kutoka kwa washirika wake wakuu wa maendeleo kwenda Moscow.
Tatizo si kwenda Moscow.
Tatizo ni kwenda Moscow wakati Washington na Brussels wanaanza kuhoji mwelekeo wa kisiasa wa Tanzania.
Diplomasia sio suala la hisia; ni suala la muda, mazingira na maslahi ya taifa.
Ukweli ambao hatupaswi kuuficha ni kwamba kwa sasa Russia haiwezi kuchukua nafasi ya Marekani na Umoja wa Ulaya katika maendeleo ya Tanzania.
Takwimu zinaonyesha wazi:
Marekani imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika kipindi cha 2020–2025.
Umoja wa Ulaya umechangia takribani dola bilioni 3.2.
Russia imechangia karibu sifuri katika Official Development Assistance (ODA).
Haya si maoni. Hizi ni takwimu.
Wakati mwingine katika siasa tunajidanganya kwamba washirika wanaweza kubadilishwa kwa urahisi. Historia inaonyesha sivyo.
Marekani na Umoja wa Ulaya hawatoi fedha pekee.
Wamekuwa nguzo muhimu katika:
mapambano dhidi ya UKIMWI na malaria,
chanjo na mifumo ya afya,
elimu,
maji safi,
kilimo,
uwekezaji wa sekta binafsi,
teknolojia,
mafunzo ya wataalamu,
na upatikanaji wa masoko ya kimataifa.
Pengo litakalotokana na kupungua kwa ushirikiano huo haliwezi kuzibwa kwa picha za viongozi kukutana au mikataba michache ya kisiasa.
Mataifa hayajengwi kwa alama za kidiplomasia; yanajengwa kwa maslahi halisi ya wananchi.
Swali ambalo viongozi wanapaswa kujiuliza si kama tunaweza kuwa marafiki wa Russia.
Swali ni:
Je, Russia inaweza kuchukua mzigo wa afya, elimu, uwekezaji, biashara na maendeleo ambao Marekani na Umoja wa Ulaya wameubeba kwa miongo kadhaa?
Mpaka sasa, jibu la ukweli ni hapana.
Hatari kubwa zaidi si kupoteza misaada.
Hatari kubwa ni kupoteza imani.
Mataifa yanaweza kuishi bila misaada kwa muda fulani.
Lakini ni vigumu kuishi bila imani ya wawekezaji, masoko ya kimataifa, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo.
Fedha za dunia zina tabia moja:
Hukimbilia kwenye utulivu, uwazi wa kisiasa na taasisi zinazoaminika.
Ndiyo maana nchi yenye busara haiharibu madaraja kabla haijajenga mengine.
Na hata kama imeamua kujenga daraja jipya kuelekea Moscow, ni hatari kubomoa madaraja yaliyoiunganisha na Washington na Brussels kwa zaidi ya nusu karne.
Kwa sababu katika siasa za kimataifa, si kila rafiki mpya ana uwezo wa kuchukua nafasi ya rafiki wa zamani.
Na katika wakati ambao Tanzania inahitaji uwekezaji zaidi, ajira zaidi, teknolojia zaidi na masoko zaidi, taifa linapaswa kuwa makini sana lisije likachanganya uhuru wa kidiplomasia na kujitenga kidiplomasia.
Uzalendo wa kweli si kupiga picha na mataifa makubwa; uzalendo wa kweli ni kuhakikisha maamuzi ya leo hayaleti gharama ambazo wananchi wa kawaida watazilipa kesho.
Maisha yako ya leo ni matokeo ya MACHAGUO na MAAMUZI yako ya jana.
ZINGATIA haya mambo 13 yatakayo KUAMSHA na kukupa NGUVU ya KUKOMAA na kusaka MAFANIKIO na UTAJIRI wa kesho yako.
NAKAZIA! zingatia namba 3 ni muhimu sana!!
Thread/Uzi🧵⤵️
Baada ya kupitia zaidi ya 70+ success stories za watu waliofanikiwa, kuna mambo 15 yamejirudia tena na tena… na haya yameanza kubadilisha maisha yangu.
Thread/Uzi🧵⤵️
Kuna umri fulani ukifikisha unakua hauhitaji tena kuwa na marafiki wengi. Unahitaji clients, customers, connections, na confidence ya kupush malengo yako.
“Watu wanaenda mwezini, ule mwezi ni wa watu wote. Sisi pia tunataka tuwe na uwezo wa kwenda huko mwezini tuone kuna nini. Lakini tuko hapa Kyankwazi tunacheza ‘paka chini’ wakati wenzetu wako mwezini wanatungalia sisi huku chini kama sisimizi” Rais Museveni wa Uganda.
Netanyahu on Mojtaba Khamenei:
We eliminated the old tyrant. And the new tyrant, the new puppet of the Revolutionary Guards, cannot show his face in public.
Netanyahu on Mojtaba Khamenei and Naim Qassem:
“I believe there will be surprises, I must keep some of the combat fog at this press conference. What I can tell you is that we have the upper hand far more than we anticipated, and we will achieve all our objectives.”