Ni nani hasa ambae anakwamisha mchakato wa amani kati ya Israel na Palestina?
May 20, 1948 UN ilimteua Count Folke Bernadotte kuwa mpatanishi mkuu katika mgogoro wa huu.
Bernadotte aliuawa Sept 17, 1948 na kundi la kiyahudi la Lehi ambalo lilikuwa linapinga mapendekezo yake. 👇
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 229
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.
Mhe. Lissu : Shahidi apatiwe PGO namba 1 aya ya 25 Crimes are Actions defined by law yanayoitwa makosa ni matendo yaliyofafanuliwa na Sheria ya Upelelezi wa Polisi inabidi ufuate masharti ya sheria strictly.
Swali langu kifungu cha 38 (2)d kinataja tendo la kuvuruga uchaguzi ni kosa?
ACP Amin Mahamba : Hapana.
Shahidi kakubaliana na Mhe. Lissu kimtindo kuwa haijataja.
Mhe. Lissu: PGO namba 1 para 3 inasema kila Askari Polisi anawajibu wa kuheshimu Uhuru wa mwananchi kama ulivowekwa kwenye Katiba na Sheria na kwenda kinyume na haya haikubaliki, tafsiri iko sahihi au sio sahi?
ACP Amin Mahamba : Inategemea
Mhe. Lissu anarudia tena swali hilo hilo.
ACP Amin Mahamba anajibu hapa anajiumauma sana ni kweli tunatakiwa kuheshimu haki za raia imetoka kwa mbinde sana mdomoni mwake.
Mhe. Liss : Ibara ya 15 (1 kila mtu ana haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru kweli au si kweli?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli.
Mhe. Lissu; Kuna mahali umezingatia uhuru wangu kwenye maelezo yako polisi?
ACP Amin Mahamba : Hayapo ila aina ya kosa uliloshtakiwa nalo halitakiwi uwe huru, ninachotambua ulikuwa na haki.
Mhe. Lissu : Hao wenzio nilimalizana nao niko na wewe ulitambua haki yangu ya uhuru kwenye maelezo yako?
ACP Amin Mahamba : sikuweka
Mhe: Lissu : Ulizingatia Haki yangu ya uhuru wa kutoa maoni na fikra zangu kwenye maelezo yako uliyotoa polisi?
ACP Amin Mahamba : Ilizingatiwa
Mhe. Lissu anasoma hapa ibara inayoongelea haki ya mtu kutoa mawazo yake hadharan na kujumuika na watu...
Anasema Mwenyekiti wa chama alitoa mawazo yake alipokutana na watu wake hadharani ulizingatia haya?
ACP Amin Mahamba : Ulifanya makosa, uliitisha serikali.
Mhe. Lissu: Hayo maelezo ya kutisha serikali yako wapi? inaweza ikawa una shida ya akili
Shahidi : Kimyaaaa
Mhe. Lissu ; Ulizingatia kuwa nina haki ya kufaidi haki za kikatiba kutokana na ibara ya 29 na ukaweka kwenye maelezo yako?
ACP Amin Mahamba : Hapana sikuweka
Mhe. Lissu: Kama uliangalia video nilishambulia sana Tume ya Uchaguzi kuwa inapendelea CCM miaka yote na watumishi wanaohusika na Serikali, wanapendelea ccm pamoja na wizi wa kura..
ACP Amin Mahamba : Ndio ulisema
Mhe. Lissu : Nilisema kuwa Samia aliamuru wagombea wa upinzani waenguliwe kwenye uchaguzi wa Serikali za mtaa?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli, ulisema.
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 227
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shaidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.
Mhe. Lissu : Waeleze Waheshimiwa Majaji kama mimi nilidessiminate hiyo video mtandaon au kama nilipublish hiyo video mtandaoni?
ACP Amin Mahamba ; Ndio ni wewe.
Mhe. Lissu; Waeleze majaji kama nimeajiriwa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Sina uhakika na hilo.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji kama mimi ni mpiga picha wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : sina uhakika
Mhe. Lissu : Na wewe ndo ulikuwa mpelelezi wa kesi hii na huna uhakika na mambo na yote unayosema hapa?
Mhe. Lissu : Ni kweli hio video ya ilichukuliwa na P1 mfanyakazi wa jambo tv?
ACP Amin Mahamba ; Sio kweli.
Mhe. Lissu : Taratibu wewe Afande, Ni kweli au si kweli kwamba kwenye maelezo uliyoyasoma ulisema P1 alikuwa anarusha video mubashara kupitia camera yake ya Sonny Ericsson?
ACP Amin Mahamba : Ndio ni kweli.
Mhe. Lissu : Waeleze Majaji kama ni kweli kwenye maelezo ya P1, yeye ndiye aliyehifadhi na kurusha mubashara video kwenye Mtandao wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli
Watu 😂😂😂😂😂 Shaidi kakataa kona, amekubali Penalty.
Mhe. Lissu ; Ulisoma maelezo ya George Bagyemu?
ACP Amin Mahamba : Ndio nilisoma.
Mhe. Lissu : George Bagyemu alisema kwenye maelezo yake aliyojiandikia mwenyewe kama wewe kuwa video ilirushwa na kurekodiwa na Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli
Mhe. Lissu : Mashaidi P1 na P2 walipewa maelekezo ya kucover Mkutano wangu na John Marwa?
ACP Amin Mahamba : Ndio
Mhe. Lissu : Waeleze Mahakama kwamba John marwa alipewa mualiko na
Mkurugenzi wa habari Chadema mimi ndio Mkurugenzi wa habari?
ACP Amin Mahamba : Hilo sijalifanyia kazi
Mhe. Lissu : Nimekaa mahabusu mwaka na miezi 4 kwa kosa ambalo wamemfanya Jambo tv, Waeleze Majaji kama huu ndio utendaji wa Jeshi la Polisi la Tanzania?
ACP Amin Mahamba : Waheshimiwa Majaji mshtakiwa ananipitisha kwenye maelezo ya P1 na P2
Huyu Polisi anaongea kwa dharau sana hapa
Mhe. Lissu anamkatisha anamjibu lissu majaji wanamtuliza Shahidi
Mhe. Lissu : Anarudia tena maswali yake na anaongeza kuuliza kama John mnyika alihojiwa?
ACP Amin Mahamba : Hapana
Mhe. Je Golugwa alihojiwa ili waseme?
Mhe. Lissu Je Mkurugenzi wa habari wa CHADEMA alihojiwa?
ACP Amin Mahamba ; Hao wote ni sehemu yako siwezi kuwahoji.
Mhe. Lissu: Mwenyekiti wa Chama anawajibika kijinai kwa Makosa ya kijinai ya watu wengine?
ACP Amin Mahamba : Umeshtakiwa kama lissu sio Mwenyekiti.
Afande anakimbia kujibu swali hapa 😂
Mhe. Lissu : Je Mwenyekiti wa Chadema anawajibikia kijinai kwa kosa ambalo umelitenda wewe au kwa makosa ya watu wengine?
ACP Amin Mahamba : Huwajibiki
Mhe. Lissu : Nawajibika au siwajibiki?
ACP Amin Mahamba : hauwajibiki
Mhe. Lissu :Turudi kwenye maneno niliozungumza, Waeleze majaji kuwa ni kweli au si kweli hotuba ilikuwa inahusu shida ya Uchaguzi Mkuu kwa mujibu wa Lissu?
ACP Amin Mahamba : Kweli
Mhe. Lissu : Maswala yaliyopo kwenye uchaguzi ni maswala yaliyoko kwenye katiba ya nchi na taratibu za nchi?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli.
Mhe. Lissu : Kwa katiba hii mtu anaetaka uchaguzi usifanyike kwa katiba hii amefanya kosa?
ACP Amin Mahamba : hapana sio kosa.
Mhe. Lissu : Unajua sheria ya uchaguzi na kuna kosa linaloongelea kuvuruga uchaguzi?
ACP Amin Mahamba : Sina uhakika sana na sheria ya uchaguzi.
Mhe, Lissu: Mimi nina uhakika sheria ya uchaguzi haina kosa la kuvuruga uchaguzi na mmelisema kama kosa la uhaini, mimi nitasema sio kosa la jinai wewe unasemaje?
ACP Amin Mahamba : makosa na sheria ziko nyingi
Mhe. Lissu : Tutaenda huko kote apewe penal code s.39(2) d asome kama hilo kosa linasema kuzuia Uchaguzi au kuhamasisha watu kutofanya uchaguzi ni kosa?
ACP Amin Mahamba : Nikitafasiri hii sheria...
Mhe. Lissu anamwambia kutafsiri sheria ni kazi ya Wanasheria sio mapolisi.
Watu wanacheka: 😂😂😂
Part 228 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 11, 2026
Last time tuliishia Part 225 so leo tunaendelea na-;
Part 226
Jana Shahidi wa upande wa Jamhuri ACP Amin Mahamba alianza kutoa ushaidi wake na leo Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross-examination.
Mhe. Lissu : Unaweza kuiambia Mahakama kwamba ulifufuka lini?
ACP Amin Mahamba : Sijaelewa
Mhe. Lissu : Mke wa Amin Mahamba anasema kwamba Amin Mahamba alifariki, sasa iambie Mahakama ulifufuka lini?
ACP Amin Mahamba : Huyo Amin Mahamba anaetajwa sio mimi.
Mhe. Lissu : Kwahiyo ni ushahidi wako kuwa huyu Amini Mahamba ni mwengine sio wewe?
ACP Amin Mahamba : Ndio ni mwingine tena yeye ni mstaafu na wanasema alishariki kweli kama unavosema.
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama ulimshirikisha RSO kwenye upelelezi wako?
ACP Amin Mahamba : Sikumshirikisha
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama ulimshirikisha afisa yoyote wa TISS.
ACP Amin Mahamba : Sikumshirikisha
Mhe. Lissu: Unafahamu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa?na kama uliishirikisha kamati ya ulinzi ya mkoa wa Dar es salaam?
ACP Amin Mahamba :Naifahamu na sikuwaashirikisha
Mhe. Lissu : Ulishirikisha ikulu?ofisi ya VP au Waziri mkuu?
ACP Amin Mahamba : Sikuishirikisha na sikuwaambia lolote.
Mhe. Lissu : Ulishirikisha ofisi ya DPP ndio nilishirikisha kanda maalum NPS.
Mhe. Lissu :Ulimshirikisha nani?
ACP Amin Mahamba: Incharge Mayenga
Mhe. Lissu : Umesema kokote kwenye nyaraka yako?
ACP Amin Mahamba : Sijasema na sijamtaja
Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa sheria ya NPS mwenye jukumu la kuratibu upelelezi ni DPP na Mastate Attorney wake.
Waeleze ni DPP yupi au State Attorneys yupi?
ACP Amin Mahamba : Kimya
Mhe. Lissu : Jibu swali wewe Polisi
ACP Amin Mahamba : Sijaelewa swali.
Mhe. Lissu : Swali langu linahusu nani aliecordinate upelelezi?
ACP Amin Mahamba : Ni DPP Mwenyewe, aliteua mtu nilisema jana kuwa sijui jina lake alitoka ofisi ya DPP Dodoma na nilisema ana jina la kibantu nimesahau.
Mhe. Lissu : Tutaenda kwa DPP Mwakitalu atupe hilo jina tuko kwenye serious matters.
😂😂😂 inachekesha sana maana jamaa hajui jina la mpelelezi ambae alishirikiana nae kufanya upepelezi pamoja na kufungua faili la kesi hii.
Mhe. Lissu : Umesema wewe ni mpelelezi wa muda mrefu umewahi peleleza kesi ya kisiasa?
ACP Amin Mahamba : Sijawahi
Mhe. Lissu : Kesi ya uhaini ni kesi kubwa sana ni highest in the land kwahiyo hujawahi kabisa na hii ndo kesi ya kisiasa ya kwanza.??
ACP Amin Mahamba : Sijawahi hii ndio ya kwanza
MheZ Lissu : Umewahi peleleza kesi ya mtu alikuwa mbunge na kiongozi wa Chama kama lissu?
ACP Amin Mahamba :Sijawahi
Mhe. Lissu : Umesema kitengo chako kinashugulika na makosa ya mtandao
ACP Amin Mahamba : Ndio
Mhe. Lissu: Ushapeleleza kesi ya cybercrime?
ACP Amin Mahamba : Ndio nimewahi.
Mhe. Lissu : Kesi gani shahidi?
ACP Amin Mahamba ; Nakumbuka nikiwa RCO Kinondoni
Naona kasita kama dakika 5 hivi then akasema kesi ya Mbowe na Mzee wa karatu Slaa
Mhe. Lissui : Waeleze ilikuwa inahusu nini na iliishaje?
ACP Amin Mahamba ; DPP hakuwa na interest ya kuendelea na kesi ikaisha hewani.
Mhe. Lissu : Una kesi zingine zaidi ya hizi kwenye cybercrime?
ACP Amin Mahamba ;Hapana
Mhe. Lissu: kwahiyo hauna kesi nyingine zaidi ya hiyo iliyofutwa?
ACP Amin Mahamba : Ninazo nyingine nyingi siwezi kuzikumbuka nikiwa RCO na OCCID.
Mhe. Lissu : Kwahiyo jana kweye ushahidi wako unasema mimi ndie niliechapisha video yangu hapa mtandao wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ndiyo nilisema.
Mhe. Lissu ; Unafahamu maana ya neno kuchapisha mtandaoni?
ACP Amin Mahamba : Ndio nafahamu lakini sheria ambayo imetumika kukushitaki sio Cybercrime.
Mhe. Lissu : Waeleze waheshimiwa majaji kama mm ndie nilisambaza video za YouTube kwenye mtandao wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ndio ni wewe ulisambaza hizo video.
Part 227 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Lissu aendelea kumuhoji shahidi
Shahidi anapewa hati ya kiapo
Lissu: Ni yenyewe si ndio?
Shahdi anakagua
Lissu: Kesi ya uhaini sio rahisi haijawahi kuwa rahisi, ni kiapo chako kweli si kweli
Shahidi: Ni kweli
Lissu: Kuna mahali popote umesema shahidi alitishiwa kupigwa Shahidi: Ipo
Lissu: Isome tafadhali.
Shahidi: Naona hii hapa “body harm”
Lissu: Body harm inaweza kuwa na namna nyingi, je, kwenye kiapo chako kuna mtu alipigwa aliambiwa tutakuua tutachoma nyumba tutashambulia familia yako?
Shahidi: hiyo haipo
Lissu: Sasa shahidi kuhusiana na hii habari ya mashahidi kutishiwa, waliletwa mashahidi niliwauliza swali je ulitishiwa kupigwa, ndugu zako au kudhuriwa wote walisema hapana sasa wewe unadai walitishiwa Je mahakama ifuate ushahidi wa nani?
Shahidi: Wakwangu
Lissu: Shahdi angalia hicho kielelezo chako mwanzo kabisa... Makazi Goba njia Nne kata ya Matosa waeleze majaji kama kweli si kweli Goba iko halmashauri ya manispaa ya Ubungo.
Shahidi: Sijui
Lissu: Hujui, Goba iko manisapaa ya Ubungo?..nataka nimsomee shahidi aelewe maeneo.
Anamsomea maneo yote ya ubungo.
Lissu: Waeleze majaji wewe umeandika kata gani
Shahidi: Kata ya matosa.
Lissu: Shahidi twende kwenye kielezo D15 waeleze majaji nani ameandika hayo maelezo.
Shahidi: Nimeandika mwenyewe.
Lissu: Hayo ni maelezo waeleze majaji kama shahidi ana uwezo wa kujiandikia maelezo yake mwenyewe kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai.
Shahidi: Shahidi yeyote maelezo yake yanachukuliwa na afisa wa polisi.
Lissu: Kwenye hayo maelezo aliyekupa onyo kama shahidi ni nani?
Shahidi: Nimetoa tamko
Lissu: Hilo tamko umelitoa mbele ya nani mbele ya afisa gani wa polisi?
Shahidi anajieleza
Lissu: Wewe si umesema ni polisi mimi mwanasheria
Lissu: Hilo tamko umetoa mbele ya nani?
Shahidi: Nimeandika mwenyewe
Lissu: Kuna sehemu ya saini ya mtoa maelezo hapo amesaini nani?
Shahidi: Mwenyewe
Lissu: Na hapo chini sehemu ya afisa aliyeandika maelezo
Shahidi: Nimesaini mwenyewe.
Lissu: Kwenye maelezo yako D15 umesema majukumu yako ni kulinda raia na mali zao.
Shahidi: Ndio
Lissu: Na ulisema uko kwenye kitengo x
Shahidi: Ndio
Lissu: Waleze majaji kama kazi za kitengo X ni pamoja na kulinda raia na mali zao
Shahidi: Ndio
Lissu: Unafahamu PGO
Shahidi: Ndio
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi apewe nakala yangu ya PGO sidhani kama wanayo.
Shahidi anapokea..
Lissu: Waeleze majaji kama hayo yaliyotajwa ni sehemu ya majukumu ya kitengo X kwenye kulinda raia na mali zao. Nimekuwekea alama order 6/8
Shahidi: Swali ni nini?
Lissu: Je, kitengo X kina wajibu wa kulinda raia na mali zao?
Shahidi: Ni sehemu ya majukumu yetu.
Lissu: Soma yote yako manne
Shahidi anasoma
Lissu: Waeleze majaji kama polisi kuna kitengo Y
Shahidi: Ndio kipo.
Lissu: Waeleze majaji kazi zake ni nini
Shahidi: Vyote vinalinda raia na mali zao kama jukumu letu polisi.
Lissu: Waeleze majaji kama umewahi kuwa RCO Singida.
ShahIdi: Sijawahi kufanya kazi Singida.
Lissu: Hujawahi, waeleze majaji katika Jeshi la Polisi kipindi ambacho umekuwa RCO maafisa wa polisi wanaoitwa Amini Mahamba ni wangapi kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2009, mtu anayeitwa Super intendent of Police, Amini Mahamba
Shahidi:Alikuwepo afisa kama huyo lakini alikua anaitwa Amini said Mahamba
Lissu: Waheshimiwa majaji hii ni muhimu iko kwenye kesi ya mahakama ya rufani mwaka 2007 anaidanganya mahakama chini ya kiapo
Lissu anamsomea hukumu ya kesi anayoitumia kama rejea.
Shahidi anakataa sio yeye anasema Amini huyo anayetajwa ni mtu mwingine.
Lissu: Tuendelee.. unasema kama kazi ya kitengo X ni kushughulikia usalama wa nchi, waeleze majaji kama ulimshirikisha Regional Security Officer
Shahidi: Hapana
Lissu: Waeleze majaji kama uliwashirikisha TIS.
Shahidi: Sikuwashirikisha
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kitu kinaitwa Kamati ya Ulinzi na Usalama na. kama uliijulisha kamati hiyo ya mkoa wa Dar es salaam....
ITAENDELEA....
REPOST
@swahilitimes Trump kushindwa na Iran kivita sasa anaanza kuwapangia wanasoka kioongozi wasiemtaka! tangia lini michuano ya World Cup ishindwe kufanyika eti sababu mtu fulani hayupo?
Lissu amuhoji shahidi kama alipewa jina la mwanachadema yeyote aliyekua hatarini kwa vitisho
Lissu: Waeleze majaji kama uliwasilisha hiyo barua
Shahidi: Ipo
Lissu: Ipo Mahakamani
Jajji: Shahdi embu jibu kama umeleta au hujaleta mawakili wa serikali watakuuliza baadae pia
Lissu: Kwa hiyo jibu ni lipi
Shahidi: Sijaleta
Lissu: Nataka maswali yangu yajibiwe kwemye ushahidi wako, jana ulisema hivi baada ya kaungalia hiyo video uliona kwamba mtuhumiwa alidhihirisha nia yake kwa kuchapisha kwa umma, kwa kuchapisha kwemye Jambo TV. Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Shahidi kwenye ushahidi wako kuhusu tuhuma ulisema, uchaguzi mkuu uko kwa mujibu wa Katiba na mlinzi mkuu wa Katiba ni serikali. Umewahi kusoma Katiba?
Shahidi: Kipindi cha nyuma
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimsomee Katiba, Ibara ya 26 - "Kila mtu ana wajibu wa kulinda na kuzifuata na sheria za nchi hii, wewe umesema ni serikali
Shahidi:.......
Lissu: Ulisema kulikuwa na mipango ya kuvuruga uchaguzi kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kupiga watu mawe na mengineyo, waeleze majaji kama hayo maneno yako kwenye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Jana ulisema hivi, hiyo video mliyoiangalia iliwekwa kwenye 'memori kadi' ikafikishwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi ili kuithibitisha, sasa waeleze majaji kama hayo yapo kwemye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kwa kuwa wewe ni shahidi wa 16 na wengine 15 waliopita hawakuwasilisha video Mahakamani naomba waeleze majaji kama umewasilisha hiyo video
Shahidi: Hapana
Lissu: Kwakuwa wewe ni shahidi wa 16 na hakuna aliyewasilisha ripoti ya kubaini uhalisia wa hizo video, waeleze majaji kama umewasilisha hiyo ripoti ya uchunguzi
Shahidi: Hapana
Lissu: Unasema ulimuelekeza Inspekta Michael kuchukua vielelezo pamoja na ripoti ya uchunguzi na kukabidhiwa kwa mtunza nyaraka. Je, hayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Baada ya kufanya yote ambayo mlikua mmeshafanya uliwasiliana na Ma RCO nchi nzima, hiyo ipo sitakuuliza, sasa kwenye maelezo yako jana umetaja majalada ya uchunguzi toka mikoa mbalimbali; Ruvuma, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam. Mimi nakuuliza juu ya jalada la Dar es Salaam, toka ofisi ya ZCO ambalo namba zake ni….. waeleze majaji kama lipo kwenye maelezo yako.
Shahdii: Hayapo
Lissu: Jana ulisema mtuhumiwa alikamatwa Mbinga na kusafirishwa usiku huo huo mpaka Dar es Salaam, Kituo Kikuu cha Kati na kufikishwa ofisi ya Deputy ZCO. Waeleze majaji kama hapo maelezo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Ulieleza pia jinsi ulivyopeleka jalada ofisi ya DPP na baadae jalada kurejeshwa kwenu kuendelea na upelelezi, waeleze majaji kama hicho kipande kipo
Shahidi: Hakipo
Lissu: Unasema mlipata taarifa mashahidi kutishiwa, je kwemye maelezo yapo?
Shahdi: Hayapo
Lissu: Unasema mliwasiliana na ofisi ya DPP ili kuweza kuwapatia ulinzi mashahidi, Je yapo?
Shahdi: Yapo
Lissu: Unasema mliomba kwa barua sema kama yapo
Shahidi: hayapo
Lissu: Unasema ulikula kiapo ili kuwaombea ushahidi, Je yapo?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Hayo ni kutoka kwenye ushahidi wako jana sasa twende kwingine, umewaeleza majaji kwamba umesoma hiyo hati ya kiapo?
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze majaji kwenye hati hii uliyosaini kama ulitaja jina la shahidi yeyote
Shahdi: Hapana
Lissu: Waleze majaji kama ulipewa jina la mwanachadema yeoyote aliyekua hatarini kwa vitisho
Shahidi: Hapana
Lissu: Waleze majaji kama ulitaja mwanachama yeyote alikua akitoa vitisho hivyo
Shahidi: Hapana
Lissu: Waleze majaji kama ulitaja siku au mahali
Shahidi: Hapana
Lissu: Waeleze majaji kama ulitaja aina ya vitisho
Shahidi: Ndio nilitaja
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba nimuoneshe shahidi kiapo chake
Inaendelea.............. (REPOST)
Lissu: Umeeleza kwamba ulipofika kwa Deputy ZCO, George Pademi baada ya kutambulishwa timu, uliwapangia majukumu na ulikuwa na timu tatu. Waeleze majaji hawa watu uliowataja jana kama wako kwenye maelezo yako uliyoandika mwaka jana
Shahidi: Hayapo
Lissu: Nyongeza nyongeza.
Pia ulieleza ulikuwa na timu ya watu uliowataja jana pia kama wako kwemye maelezo yako
Shahidi: Hayapo
Lissu: Pia ulieleza ulikuwa na timu ya tatu ya Legal and Advisory, unataka kuonyesha mlifuata sheria, unasema ulikuwa na mtu ambaye jina lake hukumbuki alikuwa na jina la kibantu alitoka ofisi ya DPP Dodoma, je waeleze majaji kama hayo maelezo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Tubaki hapo nilimuuliza shahidi wa kwanza George Bajemu alisema hakukuwa na mwanasheria kwenye timu yenu, je tumuamini nani
Shahidi: Kulikua na mwanasheria
Lissu: Basi tukuamini wewe George ni liongo
Lissu: Unasema mkiwa ofisini kwa kutumia kompyuta mlitazama hiyo video Jambo TV kwa saa mbili na usheee mkiwa timu nzima waambie majaji kama yapo hayo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Hapo hapo, Shahidi wa kwanza, George Bajemu aliambia Mahakama alioneshwa vipande vipande na Kaaya wewe unasema mlitazama mkiwa na timu nzima tumuamini nani
Shahidi: …. Kabla hajajibu….
Wakili wa serikali anakatisha kidogo na kuomba kwamba Ushahidi wa Bajemi ulikua wa tarehe nne na huyu anaongelea ushahidi wa kuanzia tarehe 8 naomba wafuate rekodi sawa sawa
Lissu: Waheshimiwa majaji hawa mawakili wa serikali si wana haki ya re-examination watauliza kwa wakati wao, wako nane wanaanzaje kunifundisha mimi kufanya dodoso wasubiri zamu yao
Kimya kidogo Majaji wanaongea……
Jaji anatoa ufafanuzi waendeleee ila kwa kufuata taratibu
Lissu: Narudia swali langu George Bajem anasema mliona video vipande vipande wewe unasema mlitamza yote Majaji wa amini kipi
Shahidi: George yeye na Kaaya walitazama vipande vipande na mimi baadae baada ya kuteuliwa ndio tulikaa tukatazama kama timu kwemye kompyuta maalumu
Lissu: Waheshimiwa majaji maelezo ya George Bajem yako kwenye 'information' na niliyafanyia dodoso kwa kina na hayakuwa 'tendered' ila yako kwenye rekodi za Mahakama na nina haki ya kumuuliza shahidi kwa kutumia maelezo haya
Shahidi: Hayo sio maelezo yangu hiyo ni rekodi ya Mahakama siyajui
Lissu: Haya ndio maelezo mliyokusanya ninyi Jeshi la polisi na mkayaleta unasema hujui
Shahidi: Maelezo ya George ni ya tarehe 4 na yangu ni tarehe nane
Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi asome maelezo yake yote kuanzia mwanzo
Shahidi: Anasoma maelezo yake…….
Lissu: Mpaka hapo kuna mahali mmeangalia video?
Shahidi: Hapana
Lissu: Tuendeleee, kwenye maelezo yako ya jana umesema ulipotazama hiyo video ulimuona mtuhumiwa Lissu na nyuma kulikuwa na bendera ya taifa na Chadema waeleze majaji kama hayo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kwenye maelezo yako ulisema Lissu alikua akihutubia umma wa watanzania waambie majaji kama hayo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kwenye ushahidi wako ulisema kwamba mliwasiliana na Idara ya Uhamiaji ambayo iliwathibitishia Lissu ni Raia wa Tanzania je hayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Waeleze majaji kama umewasilisha Mahakamani barua kama uliwasiliana Idara ya uhamiaji
Shahidi: Barua zipo
Lissu: Umewasilisha Mahakamani?
Shahidi: Kimya.....
Lissu: Unataka na mawakili wakae hapo na wao ni wakaange?
Itaendelea…..
11-08-2026, Dar Es Salaam.
Lissu anaendelea kumdodosa Shahidi wa 16 wa Jamhuri, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Amin Mahamba aliyeanza naye jana:
Lissu: -Shahidi habari yako ulilala vizuri?
Shahiri: Salama Ahsante
Lissu: Sasa jana nilikua nakupitisha kwenye maelezo yako uliyotoa kizimbani naomba leo ukijibu utoe sauti kikakamavu kama askari anayeweza kuendesha gwaride.
Lissu: Waeleze majaji kama mwaka 2014 uliteuliwa kuwa OCCID Kyela waeleze majaji kama ipo?
Shahidi: Hayapo
Lissu: Waelezema majaji kama (maelezo ya) ulifanya kazi Kyela kama OCCID kwa miaka miwili na baadae ukahamishiwa Ruvuma
Shahidi: Hayapo
Lissu: Na ulikuwa RCO wa mkoa wa ruvuma kwa miaka mitano
Shahidi - Hayapo
Lissu: January 2023 ulihamishiwa Dar kama Naibu ZCO kanda maalumu waeleze majaji kama hayo maelezo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Ukiwa Deputy ZCO ulikua unasinamia wapelelezi wote wa Kanda maalumu
Shahidi: Hayapo
Lissu: Kama RCO Kinondoni ulikuwa mkuu wa wapelelezi wote wa mkoa wa kipolisi Kinondoni waambie majaji kama hayo maelezo yapo
Shahidi: Hayapo
Lissu: Mwezi Mei 2024 ukahamishwa na kupelekwa kwenye kitengo X ambapo upo mpaka leo waeleze majaji kama ipo kwenye maelezo yako
Shahidi - Hayapo
Lissu: Sasa shahidi kwenye ushahidi wako wa jana ulisema hivi tarehe 8/04/2025 nikiwa ofisini kwangu masaa ya mchana nilipigiwa simu na mkuu wangu wa kazi DCP Nganzi kwenye ofisi za ZCO Dar es Salaam, ili kwenda kuratibu na kusimamia upelelezi dhidi ya mtuhumiwa Tundu Lissu, waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako kilelezo namba D15
Shahidi: Yapo
Lissu: Waeleze majaji kama kuna sehemu inamhusu mtuhumiwa Tundu lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Isome tena , Lissu anamsomea tena
Na anamuuliza: Je kwenye maneno uliyasema jana kuna majina Tundu Lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Je una akili timamu bwana afande? kuna jina Tundu Lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Ndio maana nasema unajifanya mjanja huna lolote afande mpelelezi mbobevu
Lissu: Ulisema jana ulipofika ulipoitwa uliona jalada mezani ambalo lilimtaja mtuhumiwa Tundu Lissu
Shahidi: Yapo
Lissu: Kwenye karatasi yapo
Shahidi: Hayapo
INAENDELEA...........
Kesi imeanza na Mwenyekiti Lissu akasema analo neno la kusema kabla ya kuanza kesi.
“ Lengo pekee la DPP (Mkurugenzi wa mashtaka)la kufungua mashauri haya ni ili kupoteza muda tu ili niendelee kukaa Mahabusu .
Leo ni siku ya 166 tangu tarehe 24 Februari tangu Mawakili wa serikali waende mahakama ya Rufaa na huko nikawashinda na sasa tumerudi Mahakama kuu lakini tumerudi baada ya siku 166,tuendelee lakini ipo siku tutazungumza kuhusu haya yote yalioendelea na kuhusu huyo anaewatuma na itambidi awajibike” anasema Mwenyekiti.
“Someone will have to pay for all of this someday” says Honerable @TunduALissu
@bbcswahili Wanachunguzwa wahusuka wa gasia, ila wauaji wa watu wasiopungua 500 wakiwa hawachunguzwi! @bbcswahili mnaonaje mkawahoji ao majaji ambacho wanachunguza juu ya vitu na sio uhai wa watu uliopotea?