Tunaweza kudogosha tunavyoweza, kukosoa tunavyodhani lakini hii haiondoi Ukweli kuwa Dkt Tulia Ackson Kuwa kwake Rais wa Mabunge Duniani kumefungua ndoto za Mabinti wengi wa Kitanzania kuamini kuwa wanaweza kufungua milango ambayo waliona haiwezi kufunguka.
Possibility ya mtoto wa Mwalimu kuja kuwa Mwalimu ni kubwa. Mzazi ndiye Role Model wa kwanza kwa wanae. Kama ambavyo possibility ya mtoto wa Kiongozi kuja kuwa Kiongozi. Uwezekano ni mkubwa. Mtoto wa Askari kuja kuwa Askari na Mtoto wa Daktari kuja kuwa Daktari. Tupunguze chuki kwa watoto wa Viongozi, shida sio wao. Wazazi wetu ndiyo walibugi!
Mzazi ndiye kwa kiasi kikubwa anatengeneza njia ya Mwanaye. Mzazi ndiye Role Model wa kwanza wa watoto wake. Tengeneza njia ya mwanao, acha kelele Mtandaoni. Usipojipanga, watoto wako pia watakuwa walalamishi kama wewe hapo 2050. Usiwachukie watoto wa Viongozi au Matajiri, hawana kosa lolote. Wazazi wako ndiyo walipoteza Ramani ya vita. Jipange vizuri ili na wewe usijekuwa kama wazazi wako kwa wanao. Mafanikio hayaji kwa chuki, ni kujifunza na kujipanga.
Baba Kaliua.