#ripotizamaseko | KMC Football Club imekamilisha uhamisho wa kiungo Mshambuliaji Ibrahim Ajibu kama mchezaji huru baada ya Kuachana na klabu yake ya Dodoma jiji Football Club.
Ajibu amewahi kuzitumikia klabu za Simba, Yanga, Azam Fc, Coastal Union pamoja na Dodoma jiji Fc.
#ripotizamaseko | Klabu ya Polisi Tanzania @polisitanzaniafootballclub imekamilisha uhamisho wa beki wa kati Joseph Majagi kutoka Geita Gold Kama mchezaji huru baada ya Kumaliza mkataba wake.
Majagi amewahi kuzitumikia klabu za Green Warriors, Alliance Fc, Mbeya Kwanza Fc
#ripotizamaseko | DEAL OFF โ
-
Dili la kiungo Ahmed Pipino kwenda Simba SC limekufa rasmi, Ahmed Pipino ataendelea kusalia kwenye klabu yake ya KMC.
Sababu ni Magnet Youth sports kituo chake cha utotoni kutaka kilipwe Tshs 200M, KMC ikihitaji ilipwe kiasi cha Tshs 150M.
#ripotizamaseko | Klabu ya Polisi Tanzania club imekamilisha uhamisho wa golikipa Haroun Mandanda kama mchezaji huru baada ya Kumaliza mkataba wake na klabu ya Tabora United.
#ripotizamaseko | Wachezaji Valentino (kushoto) Mashaka pamoja na Vedastus Masinde (kulia) wamejiunga na klabu ya JKT Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Simba
Uhamisho huu wa mkopo wa wachezaji hawa ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa Wilson Nangu na Yakubu Suleiman.
#ripotizamaseko | DEAL DONE AND SEALED
Simba sports club imekamilisha uhamisho wa beki wa kati Vedastus Masinde kutoka TMA stars Football Club.
Masinde atajiunga na Jkt Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja.
#ripotizamaseko | DEAL DONE
-
Simba sc imekamilisha uhamisho wa wachezaji Wilson Nangu pamoja na Yakubu Suleiman kutoka JKT Tanzania baada ya kukamilisha malipo ya ada ya uhamisho (Transfer Fee)
Pia Simba sc itawatoa wachezaji wake watatu kwa mkopo wa mwaka mmoja kuelekea JKT
#ripotizamaseko | Kiungo Ezeqiel Mwashilindi amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Mtibwa Sugar Football Club akitokea Tanzania Prisons Sc.
Mwashilindi amejiunga na Mtibwa Sugar kama mchezaji huru baada ya Kumaliza mkataba wake na klabu ya Tanzania Prisons.
Deal Done | Namungo Fc imekamilisha uhamisho huru wa mshambuliaji Heritier Makambo kutoka Tabora United.
Makambo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Namungo Fc.
#TransferNews#ripotizamaseko
#ripotizamaseko | Mbeya City Football Club imekamilisha uhamisho huru wa kiungo Greyson Gwalala baada ya kuachana na Coastal Union ya Tanga.
Gwalala kwasasa yuko njiani akielekea Tukuyu Mwakaleli ilipo kambi ya Mbeya City Football Club.
#ripotizamaseko | Kiungo Khalid Aucho amewasili Jijini Arusha kujiunga na kambi ya klabu yake mpya ya Singida Black Stars kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa klabu hio.
#ripotizamaseko | Namungo Football Club imekamilisha uhamisho huru wa beki wa kati Hussein Bakari baada ya kumaliza mkataba wake Simba Sc.
Hussein Kazi amewahi kuzitumikia klabu za Polisi Tanzania, Geita Gold na Simba Sc.
#TransferNews
#ripotizamaseko | Winga Deus Kaseke ni sehemu ya wachezaji walioko kwenye kambi ya Singida black stars Sports Club.
Kuna uwezekano mkubwa wa kaseke kujiunga na Singida black stars kama mchezaji huru baada ya Kumaliza mkataba wake na Pamba jiji Football Club.
#ripotizamaseko | Simba sports club na Jkt Tanzania zimefikia makubaliano juu ya uhamisho wa wachezaji wawili Beki wa kati Wilson Nangu pamoja na Golikipa Yakubu Suleiman.
JKT Tanzania imepokea kiasi kikubwa cha pesa pamoja na wachezaji watatu (3).
#ripotizamaseko | Singida Black Stars imekamilisha uhamisho wa Winga Lamine Jarjou kwa mkataba wa miaka miwili.
Lamine Jarjou amewahi kuzitumikia klabu za Al Hilal, Casa Sports, Grenoble.
Lamine Jarjou tayari ameshawasili kambini Arusha kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya.