Hongera sana Alphonce Simbu kwa Medali ya Dhahabu ya ushindi wa Mbio Ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo. Ndani ya saa 2:09:48 umeandika sehemu ya historia ya Taifa letu.
Kama nilivyokusihi uliposhika nafasi ya pili kwenye Boston Marathon mwezi Aprili mwaka huu, ushindi wako ni matokeo ya nidhamu yako ya hali ya juu na kujituma kwa bidii kwenye kazi. Umekuwa mfano bora kuhusu nguzo hizo mbili za kazi kwa wanariadha na wanamichezo wenzako, na hata kwa wasiyo wanamichezo.
Endelea kuipeperusha vyema na kuiheshimisha bendera ya Taifa letu.
Mamia ya wananchi wamejitokeza katika viwanja vya guluoni Wilaya ya Kibaigwa jijini Dodoma kumsubiri Mgombea urais kupitia CCM Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili hapo na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa Kampeni za CCM leo Agosti 30,2025.
Serikali imejikita kikamilifu katika kuhakikisha kampeni za amani na halali nchi nzima. Kila chama cha siasa kilichosajiliwa – chama tawala au upinzani – kina uhuru wa kufanya mikutano na kuwafikia wapiga kura, mradi tu kifuate sheria.