Nilipoiona hii picha ilikuwa majira ya Usiku maeneo ya Riverside tukipata Kahawa na Kashata sambamba na Wastaafu fulani wa taasisi za Kiserikali ndipo ukaja Mjadala wa Mwalimu kutoka Kijiji kidogo Kusini mwa Tanzania kiitwacho Nandagala, anaweza asiwe na nia ila huenda Watu wanamnuia atie nia ukipitia zile comments.
Alianza Mzee Hussein na kusema joto kuelekea 2030 linaanza kuwa kubwa, Bookmakers wameanza kuchochoea Kuni na Wadau wa Uchaguzi wameanza kuchungulia wapitie Mlango gani na yote kwa yote hakuna anayetaka kupoteza karata zake huyu Kijana wa Kusini ni Miongozi kwa Dark Horse alisema Mzee Hussein Baribaru Mzaliwa wa Kigoma.
Akadakia Mzee Makambi Francis aligusia historia kuwa Mtu pekee aliyewahi kuwa Rais kutoka Ofisi namba 4 yaani Waziri Mkuu ni Mwalimu wa Butiama tena tukiwa Tanganyika ila tangu imeitwa Tanzania hiyo haijawahi kutokea, Kijana wa Kusini ana rekodi nzuri sana ila Historia wakati mwingine inamhukumu sana.
Mzee Mushi alikatisha mazungumzo hayo kwa kugusia kuwa ana tofauti na wenzake aliusoma upepo mapema kabla ya kuachia form, alikuwa Mtumbuizaji mzuri aliyefahamu muda sahihi wa kushuka stejini hakutaka kukaa back bencher kama Cleopa Msuya na Mzee John Malecela, hiyo ni kete adhimu kisiasa inaweza kumbeba.
Wakati mwingine ule upepo wa awamu ule Utamaduni wetu wa Mkristo kwa Muislam unaweza kuingilia kati ila hapana historia zipo kwa ajili ya kuvunjwa, katika karata serious ambazo CCM wanazo hii ni moja wapo kuna Yeye, kuna Obama wa Tanga, Mwanarizombe na hata Muungwana wa Mji wa Alizeti alichangia Mzee mmoja mwenye lafudhi ya Kihaya ambaye sikumtambua jina.
Labda niwakumbushe kitu aliingia kwa madaha Mzee Lugwisha kwa Kingereza cha kuchungia Ng’ombe akasema “Heavy is the head that wears the crown” akatamatisha kwa kusema Kassim ni kichwa kizito ndicho kitavaa kofia ya Kifalme kwakuwa amefanya kazi kwenye zama zote ngumu, zama za Muungwana wa Chato na zama mpya za Samia Hassan wa Unguja, zama zote dume na aliperform Kiume sana.
Niliondoka zangu na msemo mpya kuwa huenda Historia itambeba zaidi ya kumhukumu kwasababu Kusini imezalisha Kingpins wengi wa siasa za Tanzania, muda utaamua.
Moshi mweupe unauona Kusini?