Chadema has formally written to UN Secretary-General António Guterres, expressing concern over whether envoy Parfait Onanga-Anyanga was officially mandated to follow up on the violent suppression of civilian protests before and after 29 October 2025 in Tanzania.
BAWACHA kutoka Ubungo ambao juzi walizuiliwa na Polisi Gairo wakiwa njiani kuelekea Mkoani Musoma kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, asubuhi hii wameachiwa.
#BreakingNews
Jeshi la Polisi Musoma mjini linapiga mabomu ya machozi njee ya Kanisa la Kuu la Katoliki wakati ibada inaendelea.
Ikumbukwe leo baada ya Idd Amin Mama kuzuia BAWACHA tusifanye maadhimisho yetu, tuliamua kwenda Kanisa la Katoliki kushiriki misa takatifu.
Jumuiya ya Madola imeipokea na kukubali dhamira ya Serikali ya Tanzania juu ya kupokea na kuwezesha ziara pamoja na kazi za Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Dkt. Lazarus Chakwera ambaye pamoja na msafara wake utachunguza uminywaji wa kidemokrasia na kutofuatwa kwa utawala wa kisheria kufuatia matukio ya kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Hayo yamesemwa baada ya kikao cha 72 cha Kamati Maalum ya Jumuiya ya Madola inayoshughulikia masuala ya demokrasia, utawala bora, na haki za binadamu miongoni mwa nchi wanachama(CMAG) ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum Prof. Palamagamba Kabudi alikutana na kamati hiyo na kufanya mazungumzo.
Taarifa ya CMAG iliyotolewa baada ya kikao chake cha Machi 7, 2026 imesema “CMAG pia ilikaribisha dhamira ya Tanzania ya kumpokea na kuwezesha ziara pamoja na kazi za Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu mwezi Machi 2026.”
Disemba 2025 katika mkutano wake wa 71 wa CMAG ulioongozwa na Dkt. Ian Borg Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Malta uliamua kuiweka Tanzania katika ajenda maalum ya kikao cha machi yakizingatiwa masharti manne yaliyotolewa katika kikao kilichoijadili Tanzania Disemba 2025.
Tanzania ilitakiwa kutoa nafasi iliyokamilika bila kikwazo kwa Msafara Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuweza kukutana na wadau wote katika nafasi za mwanzo. Pia kuondolewa kwa vikwazo kwenye uhuru wa kukusanyika na kujieleza, makundi maalum na vyombo vya habari.
Pamoja na hayo masharti mengine ni Kufanyika kwa jukwaa la mashauriano kati ya vyama vya siasa ili kukubaliana mfumo wa pamoja wa hatua za kuendelea mbele kuelekea uchaguzi ujao. Uchukuaji wa hatua za kisheria na kiutawala zilizo wazi ili kuwawajibisha wahusika wa vitendo vya vurugu na athari zake, pamoja na kutoa fidia kwa waathirika pale inapofaa.
Ujumbe huo utakaoongozwa na Dkt. Lazarus Chakwera Rais Mstaafu wa Malawi unatarajiwa kufika nchini mwezi huu wa tatu huku miongoni mwa hadidu za rejea itakazotumia ikiwa ni taarifa ya Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi ambayo imeundwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
#Video ikionyesha maofisa wa Polisi wa Musoma wakiwakamata na kuwapakia kwenye karandinga lao baadhi ya Wanawake wa CHADEMA ambao walikuwa wanatoka kanisa ambako walienda kushiriki misa takatifu.
Imagine hawa wapumbavu hawataki hata kutuona tukienda kanisani kufanya ibada.
Tukiwa kituoni tulipokamatwa tangia jana usiku dakawa
Huu ni ukatili mkubwa kwa mwanamke wa Taasisi ya Chadema huku ni kubaguliwa kwa sababu ya kuwa Chadema.Tukiaza kubaguana kwa misingi ya Chama baadae tutaongeza misingi mingine ya kubaguana na tutabaguana mpaka kwenye familia
Since last night, Police in Tanzania🇹🇿 are busy arresting & detaining CHADEMA Women travelling from across the country to Musoma town to mark the #InternationalWomensDay2026
Despite this, some of CHADEMA brave women have made to Musoma & will celebrate the day in style
#IWD26
Amri zote haramu za kisiasa, Amri zisizofuata sheria, chama chetu hakitazifuata.
Polisi kwasasa wanatumika kama kisemeo tu cha ccm kutuzuia kufanya wajibu wetu wa kisiasa na hatutakubali.
Nawapongeza sana wanawake wa Chadema kwa kukataa kutii Amri haramu za kisiasa..
Mmeonesha ujasiri na utayari mkubwa sana,
Pamoja na vitisho na mazuio Nchi nzima mmefanikiwa kufika na kufanya siku yenu iwe na maana.
Wote wanaohusika kuumiza, na kunyanyasa wanachama wetu watawajibika wao binafsi..
RPC Mara waachie wanawake unaoshikilia haraka.. unajua hawajavunja sheria yoyote na hawana kosa lolote.
Wanawake wa BAWACHA, msikate tamaa. Mabomu yanaweza kuvunja kusanyiko lenu, lakini hayawezi kuvunja fikra za haki na demokrasia. Ujasiri wenu ni sehemu ya historia ya mabadiliko.
Mungu awabariki wanawake wote majasiri.
Happy Women’s Day
Nawapongeza wanawake wa Chadema kwa ujasiri,
Nyie ni wanawake imara..
Kwa wanawake wote Tanzania, mnajukumu kama walezi na wazazi kupigania haki, demokrasia, rasimali kutumika kwaajili ya wote, matibabu bora, Elimu kwa watoto wenu na maisha ya staha kwenu na kwa Watanzania wote..
Nawapongeza kwa siku yenu.
Msiogope tutashinda.
Kudos BAWACHA 💪🏽🔥
Mmesimama imara na kukataa kunyimwa haki zenu za msingi za kukusanyika na sasa mmemvua nguo Bi Kizimkazi na unafiki wake wa kujifanya anataka maridhiano! Mmekamatwa, mmedhalilishwa, mmepigwa mabomu ya machozi! Ni kama vile kuna vita! Kumbe maadhimisho ya siku ya wanawake! Aibu!
Leo Dunia nzima imeona kuwa dhulma na ukatili wa CCM na Samia iko palepale!
No retreat, no surrender ��🏽🔥
Hadi #TutaelewanaTu
Hongereni na Mungu aendelee kuwasimamia!