Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (@engmaryprisca) ameshiriki katika Jukwaa la Tisa la Biashara Barani Afrika, linalofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 16 hadi 17 Februari, 2026.
Kaulimbiu ya Jukwaa hilo ni: Kugharamia Mustakabali wa Afrika: Ajira na Ubunifu kwa Mabadiliko Endelevu” (Financing the future of Afrika: Jobs and Innovation for Sustainable Transformation.)
Jukwaa hili la kimkakati linawakutanisha Serikali, Wawekezaji, Wafanyabiashara, Taasisi za Fedha na Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano na kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika biashara na uwekezaji.
Kupitia ushiriki huu, Tanzania inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuchochea ajira, ubunifu, ukuaji wa viwanda, upatikanaji wa masoko na mitaji, na kuharakisha mabadiliko endelevu ya kiuchumi barani Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiniapisha kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Hafla ya uapisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri imefanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma Nov 18, 2025.📽 @maendeleoyajamii
Nitoe shukrani zangu za kipekee kwa Mungu, Shukrani za dhati kwa Kamati Kuu ya CCM chini ya Uongozi Imara wa Mwenyekiti wetu na Rais wetu Mhe. Dkt Samia S. Hassan. Kazi iliyo mbele yangu ni kuwatumikia kwa uaminifu Watanzania na Wanawake wa Mkoa wa Mbeya kupitia hili BUNGE LA 13
Leo nimeshiriki mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Jijini Mbeya. Mwenge utazindua miradi ya maendeleo Jijini Mbeya kabla ya kuhitimisha rasmi mbio zake katika Uwanja wa Sokoine mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametukabidhi Ilani kwa Wagombea Ubunge Majimbo ya Mbeya na Viti Maalum wakati wa Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu na Wananchi wa Mbeya mjini September 04,2025.#Kazinaututunasongambele.
Tuhakikishe tunaweka matiki matatu, ambayo yataenda kumpa Pawa Mheshimiwa Rais, matiki ambayo yatampa Pawa Mheshimiwa Mbunge CPA Mwantona, na matiki ambayo yatawapa Pawa Waheshimiwa Madiwani na tukaendelea kupata maendeleo.
Uzinduzi Kampeni Jimbo la Rungwe.
.
Uzinduzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Uyole zilizokuwa na lengo la kuomba kura za Urais, Ubunge na Udiwani uzinduzi uliohudhuriwa pia na wagombea Ubunge kutoka majimbo yote ya Mkoa wa Mbeya.
Mgombea Mwenza wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akipiga picha ya pamoja (selfie) na wananchi wa Bumbuli wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo Jumatatu, Septemba 15, 2025, katika Uwanja wa Soni, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu akifungua Jengo la Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Simiyu lililopo Bariadi tarehe 16 Juni, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu lililopo Bariadi tarehe 16 Juni, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu akifungua Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi, mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.