@NETO_TANZANIA tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wote walioweza kushiriki katika MAOMBI ya siku tatu kama tulivyotoa tangazo, lengo ni kupata majibu mazuri kutokana na kile tulichowasilisha kwenye Ofisi ya Waziri wa Nchi Menejimenti ya Umma na Utawala Bora Mh Simbachawene
Mpaka sasa zimebaki siku Ishirini na mbili (22) kuelekea kupata majibu ya hatima yetu ya kudai ajira za walimu kulingana na hoja zilizowasilishwa na wajumbe wa @NETO_TANZANIA kupitia kikao kilichoketi mwezi machi, 2025.
Shauku yetu ni kupata majibu mazuri kutoka wizara husika📍
Kilio cha umoja wa walimu wasio na ajira Tz ni AJIRA, hitaji la walimu wasio na ajira nchini ni AJIRA, tunawasihi walimu tusio na ajira na wananchi wote pasipo kujali itikadi zetu za kisiasa, kuwa wavumilivu na kusubiri majibu kwa siku zilizopangwa
#24DAYSLEFT#AjiraNiHakiYetu