Katika Dunia hii moja kati ya jambo baya kuwa nalo ni kukosa UTU,haijalishi uwe masikini ama tajiri.
Kama unafurahia wengine kuteseka kwa namna yoyote ile wewe ni SHETANI kama MASHETANI wengine.
'Yaaaah ni kweli Damu hunena' katika ukweli usiopingika kuwa damu iliyomwagika huwa ni kafara maalumu na huwa na matokeo chanya bila kujali muda itakayo kaa.
Akili ya mwanadamu huamini kila kitu kama kilivyo uwe ni Ukweli au uongo na huishi nao.
Sasa kama hutaki jambo fulani na unaamini ni uongo njia pekee ni kujizuia kusikiliza ama kuangalia mambo yenye mlengo wa uongo.
Unabii!
Kila mwenye haki atapitishwa kwenye mateso na dhiki kuu kabla ya Ukombozi halisi.
Biblia inaendelea kusisitiza kuwa Mungu atawalinda wenye haki licha ya mateso makali watakayopitia.
Kinachoniumiza ni kuwa ataruhusu wenye haki wachache wakinywee kikombe.