We can experience joy in difficult circumstances only if our lives are rooted in a relationship with God as a loving Father. Only God's love can give us true and perfect joy. If we are deeply convinced that God cares for us as His beloved children, we will not be confused or discouraged, even in the midst of hardship. https://t.co/duKCEN0LpU
Zamani tulikuwa tunaachana kwa sababu ya tabia, siku hizi vijana wanaachana kisaikolojia kulinda afya ya akili na mifuko yao. Ukiona mpenzi wako anakutumia meseji
'Mambo vipi mshua wangu'
katikati ya mwezi, hiyo sio mahaba, huo ni mtego wa dharura ya kifedha.
Kimbia!
Daktari amesema ili kulinda Figo na Akili zetu, tunatakiwa kunywa maji lita 3 kwa siku na kuepuka stress.
Swali langu ni moja tu!
Hivi nikiwa nakunywa hayo maji huku nasoma meseji ya 'Luku imeisha', hayo maji yanaenda kusafisha sumu gani sasa? 😭
Afya ya akili sio anasa.
Ukiona umechoka, unakasirika ovyo, na huna hamu ya kufanya kitu, pumzika. Mwili sio chuma, na hakuna tuzo ya kufa kwa stress za kazi.
"Punguza chumvi mbichi kwenye chakula.
Chumvi nyingi = Presha ya juu = Figo kufeli.
Mapenzi yanaweza kukuacha ukaishi, lakini Figo ikikuacha, maisha yanakuwa magumu sana. Jali afya yako."
"Kama unakunywa maji pale tu unaposikia kiu, unakuwa tayari umechelewa. Kiu ni ishara kuwa mwili wako na Figo zako zimeshaanza kupungukiwa maji (Dehydration).
Weka chupa ya maji mezani kwako sasa hivi."
"Kutafuta maisha kusiwe chanzo cha kupoteza maisha yako. Una miaka 20-35, unakimbizana na madeni, kodi, na malengo makubwa, unajikuta usiku hulali unawaza tu. Hapa kuna namna ya kuilinda akili yako isivurugike:"
-Kubali unachoweza kudhibiti: Huwezi kudhibiti uchumi wa nchi, lakini unaweza kudhibiti matumizi yako ya pesa.
-Punguza Social Media: Mitandao inaleta presha ya bandia. Watu wanaposti mafanikio, wanaficha changamoto. Usijilinganishe nao.
"Unajua kuwa Stress za maisha na Mawazo mengi haziumizi akili yako tu, bali zinamaliza na Figo zako? 🧠 Hapa kuna uhusiano wa siri kati ya Mental Health na Figo ambao daktari wako hajakwambia bado👇"
Stress sugu inapandisha homoni ya Cortisol na shinikizo la damu (High BP).
Presha ya juu ni adui namba moja wa mishipa midogo ya damu kwenye figo zako.
Figo ikikosa mtiririko mzuri wa damu, inaanza kufeli polepole bila maumivu.
"Emotional security" ni kupata mtu anayejua vizuri upande wako wa giza, mapungufu yako, na makosa yako ya nyuma—lakini bado akakuangalia machoni na kukwambia, "Hapa ndio nyumbani kwako, usihofie kitu."
Jua la Dar likuchome, foleni ya daladala ya Mbagala ikutese, bosi wa ofisini akugombeze. Then urudi geto ukutane na mpenzi anayekuporomoshea lawama na kelele zingine? Hiyo ni hatari kwa afya yako. Mpenzi anapaswa kuwa "Safe Space" ya kupumzisha akili, sio uwanja mwingine wa vita
Mwanaume anayetoa "emotional security" sio yule mwenye pesa nyingi tu, ni yule ambaye hata kama ana shilingi elfu tano mfukoni, atakutafuta akwambie: "Usiwaze mke wangu, mambo yatanyooka." Maneno yanayotuliza akili ni mtaji mkubwa sana wa kisaikolojia.