Watoto wengi huwa watu wazima na wasikumbuke sana kama wazazi wao walikuwa maskini au matajiri.
Kinachobaki kwenye kumbukumbu zao siyo njaa waliyopitia utotoni.
Ni jinsi walivyotendewa na jinsi walivyojisikia.
Ni maneno yaliyovunja nafsi na roho zao.
Ni hisia zilizopuuzwa.
Ni nyakati waliumizwa badala ya kukumbatiwa.
Wanapokuwa watu wazima, hawatokumbuka sana siku walizokosa chakula, kama watakavyokumbuka walivyokosa upendo.
Kabla hujaamua kumlea mtoto, jilee nafsi yako kwanza. Ponya majeraha yako, usiyarithishe kwa wajao.