Papa Francis ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Gemelli ya Roma ambako alifanyiwa upasuaji unaohusiana na hernia mnamo Juni 7 na anarejea Vatikani asubuhi ya leo Ijumaa Juni 16, 2023.
Mara baada ya kutoka hospitalini, Papa Francis alitabasamu na kuwapungia mkono waandishi wa habari na watu waliokwepo huku akisukumwa kwenye kiti cha magurudumu hadi kwenye gari tayari kwa safari ya Vatikani.
Daktari wa upasuaji wa Papa, Profesa Sergio Alfieri, amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna matatizo yoyote, na kwamba Papa anatarajiwa kurejesha safari na shughuli zake za kawaida, lakini hapaswi kuinua vitu vizito.
Papa Francis ana Safari za Kitume nchini Ureno, kuanzia tarehe 2 hadi 6 Agosti, kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, na Mongolia, kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 4 Septemba, katika ajenda yake.
#KitengeUpdates
@tanescoyetutz Lakini mvua si zishaanza kunyesha ama?,wakati wa magufuli walikuwa hawafanyi matengenezo au?,sema Nini waziri na watu wake hii wizara ni oversize kwake .
Uzi : CHANGAMOTO KWENYE BIASHARA YA UWAKALA WA HUDUMA ZA KIFEDHA( ELECTRONIC MONEY TRANSACTION), MFANO M-PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY, HALO PESA, NMB, CRDB N.K...ππ
Ukweli ni kwamba,kila BIASHARA inachangamoto zake ingawa CHANGAMOTO hizo zinatofautiana kulingana na...π