Aina kuu 4 za DETOX.
1. Usingizi - Detox ya ubongo.
2. Kupumzika - Detox ya misuli.
3. Kufunga kula - Detox ya mwili mzima.
4. Kufunga kula - Detox ya figo yako.
Moja kati ya vitu vinavyoleta karaha kwenye safari. Basi ni kusafiri mkiwa mmekaa siti zinazofuatana na mtu mnene kwenye basi.
Yaani hiyo safari huwa na kero kubwa sana.
Ukweli unauma. Na ukweli ni kwamba, ukiwa mnene sio mbaya kwako tu, ni kero kwa watu wengine.
#UNFAT
Katika jamii za kilokole. Kuna vitu vinasikitisha.
Wakimuona mtu mzima (miaka 18+) anakunywa zake chupa 1 ya bia (beer) wanamchukulia ya kwamba ni mtu mbaya.
Lakini kuna mzazi anampa soda/juisi mtoto wake mwenye mwaka 1.
Kiuhalisia, huyu mzazi hapa ni mtu mbaya zaidi.
Vyakula vinavyoongoza kupunguza kiwango na ubora wa Shahawa.
1. Sukari
2. Mahindi ya kisasa
3. Energy drinks
4. Mafuta ya mbegu (vegetable oils)
5. Vyakula vya kuchakatwa na kusindikwa.
Kuwa mwanaume. Kula vyakula halisi. Usile takataka.
Tofauti na imani maarufu, lishe inayotegemea nyama za mafuta itakusaidia:
- Kupunguza uzito na kuwa mwembamba
- Kupunguza shinikizo la damu
- Kuzuia ugonjwa wa viungo na guti
- Kuzuia mshtuko wa moyo
- Kuzuia kiharusi
- Kuchochea afya bora ya utumbo
- Kusaidia kutengua kisukari
Idadi ya watu wanaokufa kwa kisukari ni mara 3 zaidi ya wanaokufa kwa kuvuta sigara.
Maana yake, mtu mnene ana hatarisha afya yake zaidi kuliko anayevuta sigara.
Jiunge na mapambano dhidi ya unene:
- Usiwe mnene.
- Usiruhusu watoto wako kuwa wanene.
- Himiza wanafamilia wako wawe na afya njema.
- Kuwa kioo cha mfano cha afya mahali unapooshi.
Dunia bila unene inaanzia kwako.
Kula protini kwa wingi. Chakula chenye protini kidogo kitakufanya:
- Kuhisi tamaa ya vyakula visivyo na afya
- Kushindwa kudhibiti njaa yako
- Kuhisi uchovu kila wakati
- Kuugua mara kwa mara mafua
- Kupambana na uzito uliozidi/unene
Pata kiwango sahihi cha protini.
Kutembelea wagonjwa ni jambo zuri sana.
Lakini watu hukosea sana sehemu hii.
Mgonjwa ambaye amelazwa, tayari ana Ini ambalo linapambana ili aweze kupona. Unapompelekea Juisi za maboksi, energy drinks na matunda yenye sukari. Unazidi kumuumiza bila wewe kujua.
Hivyo basi. Unapompa vitu vyenye sukari (matunda, juisi n.k)
Unazidi kuharibu Ini la mgonjwa huyu.
Kinachosikitosha hata wahudumu wa afya watakuona ukimpa, hawatakwambia chochote. Kwani wengi tunasoma ili kufaulu mitihani na sio kuelewa.
Hutapata kisukari cha mimba na shinikizo la damu.
Epuka sukari, wanga uliokobolewa na kuchakatwa au kusindikwa, vyakula vya kukaangwa na mafuta mengi. (Deep fried)
Mwanamke mjamzito kula:
+ Samaki wenye mafuta.
+ Nyama.
+ Mayai.
+ Mboga za majani kijani.
+ Boga la nazi.
+ Siagi na mafuta ya wanyama.
Kwa wingi.
Hutanenepa na utapata maziwa mazito yenye lishe kwa mtoto wako.
Hutapata upungufu wa damu.
Ikiwa una:
- Kisukari
- Shinikizo la damu
- Ini lenye mafuta mengi
- Unene wa kupindukia
- Triglycerides zilizo juu
Sukari kutoka chanzo chochote itaongeza matatizo kwako.
Ondoa sukari zote. Hakuna majadiliano, hakuna ubadilishaji, hakuna mbadala.
Fikiria unatumia dawa nyingi wakati dawa yenye nguvu zaidi iko kwenye sahani yako na katika tabia za maisha.
Kuchagua lishe na mtindo wa maisha wenye afya badala ya dawa si tu ni mantiki, bali pia ni kuwezesha na kuleta uhuru wako.
Acha chakula kiwe dawa yako.
Kula vyakula vyenye afya ni ghali?
Umewahi kuona bili za matibabu kwa ajili ya dialysis,kisukari, au chemotherapy?
Je, una wazo la gharama kubwa inayotokana na msongo wa mawazo na kupoteza ubora wa maisha?
Kula vyakula vyenye afya si ghali, kula vibaya ndio gharama kubwa.