1. Haki na Wajibu wa Kisiasa kwa Mujibu wa Katiba
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa) inatambua na kulinda:
Haki ya kushiriki shughuli za kisiasa (Ibara ya 20 na 21), ikiwemo kujiunga na chama cha siasa na kushiriki mikutano ya kampeni.
Uhuru wa mawazo na kujieleza (Ibara ya 18), ambao hujidhihirisha kwenye mikusanyiko ya hadhara kama hii.
Kwa hiyo, wingi wa watu waliokusanyika Kawe ni kielelezo cha haki ya wananchi kushiriki kidemokrasia, mradi tu shughuli hizi zinafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu.
2. Sheria za Uchaguzi na Kanuni za Kampeni
Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani (Sura ya 343) na Kanuni zake, pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zinaweka misingi ya kampeni:
Kampeni lazima zifanyike katika mazingira ya amani na usalama.
Vyama vyote vinapaswa kupewa nafasi sawa ya kufanya kampeni.
Viongozi na wagombea wanakatazwa kutumia lugha za chuki au kuchochea uvunjifu wa amani.
Kwa kuwa umati mkubwa umejitokeza, jukumu la vyombo vya dola na NEC ni kuhakikisha kuwa mikutano inabaki kwenye mstari wa amani na heshima kwa sheria.
3. Uwepo wa Viongozi wa Kitaifa na Wastaafu
Uwepo wa viongozi wa kitaifa na wastaafu una uzito mkubwa:
Kiishara, unaonyesha mshikamano wa kitaifa na mwendelezo wa uongozi.
Kidemokrasia, unathibitisha kwamba hata viongozi wastaafu wanashiriki na kutunza hadhi ya mchakato wa kisiasa.
Pia unatoa taswira ya umoja na mshikamano ndani ya chama na taifa, kinyume na migawanyiko ya kisiasa.
4. Mustakabali wa Taifa
Hali ya amani na utulivu iliyotajwa hadi sasa ni msingi wa mustakabali wa taifa:
Ikiendelea kudumishwa, itahakikisha uchaguzi huru na wa haki.
Wingi wa wananchi wanaojitokeza ni ishara ya imani kwa mchakato wa kidemokrasia, lakini pia changamoto ya kuhakikisha kila upande unapata fursa sawa.
Kwa taifa changa na lenye historia ya mshikamano, mustakabali wake hutegemea kuheshimu demokrasia, kutii sheria, na kudumisha mshikikano wa kijamii.
Kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Uchaguzi, mkusanyiko wa maelfu ya wanachama wa CCM Kawe ni tukio la kawaida la kisiasa, linaloonyesha haki ya kikatiba ya kushiriki katika shughuli za kisiasa. Uwepo wa viongozi wote – wa sasa na wastaafu – unaleta uzito wa kitaifa na kuimarisha mshikamano. Mustakabali wa taifa utategemea zaidi namna vyama vyote, viongozi na wananchi wanavyoshiriki kwa heshima, amani na kufuata sheria kuelekea Uchaguzi wa 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia na kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 27 June, 2025.
🗳️ BUNGE LIMEVUNJWA – JE, WABUNGE WENU WALIWATENDEA HAKI? 🇹🇿
Sasa ni rasmi, Rais amelivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano.
✅ Ni wakati wa kutafakari.
📌 Je, Mbunge wako alisimamia kero zako ipasavyo?
📌 Alihudhuria vikao?
📌 Alikuwa karibu na wananchi au alitoweka mara baada ya uchaguzi?
📌 Umeridhika na Bunge hili kwa ujumla?
👇 Tuambie maoni yako kwa ujasiri:
🔁 Ungependa kurejea Mbunge wako au unataka mabadiliko? Kwa nini?
🧠 #TuhojiTufikieUkweli
🇹🇿 #TanzaniaKwanza | #Bunge2025 | #UchaguziMkuu
Kazi nzuri ya Rais Samia ni injini muhimu ya maendeleo ya Tanzania. Amekuwa na umuhimu mkubwa sana katika kujenga uchumi imara, kuondoa umaskini, na kukuza ustawi wa jamii kwa ujumla. #sisinitanzania
Tsh 600,300,000 kukamilisha ujenzi wa shule Mpya ya Sekondari Mwambasha, kijiji cha Mwambasha, kata ya Lyabisalu, wilaya ya Shinyanga, Mkoa wa Shinyanga. Asante Mama @samia_suluhu_hassan kwa upendo wako.
@Samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa @ikulu_mawasiliano
Safarini kwa treni kutoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma, ambapo pamoja na majukumu mengine, kesho Ijumaa Juni 27 nitahutubia na kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
VIJANA WAMWAGA SIFA KWA SERIKALI KATIKA TAMASHA LA KUPINGA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DODOMA
Katika kilele cha Tamasha la Vijana Kupinga Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya lililofanyika katika Ukumbi wa Generali Mabeyo jijini Dodoma, vijana kutoka maeneo mbalimbali ya nchi walijitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na janga la dawa za kulevya. Tamasha hilo, lililofanyika kwa lengo la kutoa elimu, kuhamasisha mabadiliko chanya, na kushirikisha vijana kama mawakala wa mabadiliko, lilikuwa na shamrashamra za hotuba, burudani, ushuhuda wa waliowahi kuwa waraibu, na maonesho ya kazi za vijana waliopata ujuzi kupitia programu za serikali.
Vijana walioshiriki waliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua madhubuti ilizochukua kudhibiti uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini. Walisema kuwa juhudi hizo zimeokoa maisha ya maelfu ya vijana na kuwapatia matumaini mapya.
Aidha, walieleza kufurahishwa na uwepo wa huduma za tiba kwa waraibu kupitia vituo vya afya vya serikali na mashirika binafsi, sambamba na fursa walizopata za mafunzo ya ujuzi stadi katika vyuo mbalimbali kama VETA na taasisi za kijamii. Mafunzo hayo yamewawezesha vijana kujiajiri na kujitegemea, hivyo kujiepusha na vishawishi vya dawa za kulevya.
Kauli mbiu: "Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya"
#sisinitanzania
#dawazakulevya
#SAMIA2025
#nchiyangukwanza
VIJANA WAMWAGA SIFA KWA SERIKALI KATIKA KONGAMANO LA KUPINGA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DODOMA
Katika Kongamano la Vijana Kupinga Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya lililoandaliwa na Mamlaka ya Kupiga vita na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) lililofanyika katika Ukumbi wa Generali Mabeyo jijini Dodoma, vijana kutoka maeneo mbalimbali ya nchi walijitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na janga la dawa za kulevya.
Kongamano hilo, lililofanyika kwa lengo la kutoa elimu, kuhamasisha mabadiliko chanya na kushirikisha vijana kama mawakala wa mabadiliko, lilikuwa na shamrashamra za hotuba, burudani, ushuhuda wa waliowahi kuwa waraibu, na maonesho ya kazi za vijana waliopata ujuzi kupitia programu za serikali.
Vijana walioshiriki waliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua madhubuti ilizochukua kudhibiti uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini. Walisema kuwa juhudi hizo zimeokoa maisha ya maelfu ya vijana na kuwapatia matumaini mapya.
Aidha, walieleza kufurahishwa na uwepo wa huduma za tiba kwa waraibu kupitia vituo vya afya vya serikali na mashirika binafsi, sambamba na fursa walizopata za mafunzo ya ujuzi stadi katika vyuo mbalimbali kama VETA na taasisi za kijamii.
Mafunzo hayo yamewawezesha vijana kujiajiri na kujitegemea, hivyo kujiepusha na vishawishi vya dawa za kulevya. Wakati wa tamasha hilo, vijana walisisitiza kuwa elimu, msaada wa kitabibu na fursa za kiuchumi ni nguzo kuu za vita dhidi ya dawa za kulevya. Walitoa rai kwa serikali na wadau kuendelea kushirikiana katika mapambano haya kwa kutumia sanaa, michezo, na mafunzo kwa vijana kama silaha madhubuti za kuokoa kizazi cha leo na kesho.
Alhamisi, 26 Juni, ni kilele cha maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya dawa za kulevya, ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete - Dodoma.
Kauli mbiu: "Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya" Mwisho.
#MatokeoChanyA
#DCEA
#OktobaTunatiki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma tarehe 26 Juni, 2025. Pamoja na mambo mengine kesho Mhe. Rais Dkt. Samia atahutubia nakuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
TUJITOKEZE KWA WINGI! TUUNGANE NA RAIS SAMIA KATIKA KILELE CHA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA
Wana-Dodoma na Watanzania kwa ujumla, mnakaribishwa kushiriki katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya kitakachofanyika tarehe 26 Juni 2025, kuanzia saa 1:00 asubuhi, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma.
#dawazakulevya
#sisinitanzania
#matokeochanya
#nchiyangukwanza