Shida zingine hazihitaji maombi wala kufunga pekee...zinahitaji ujasiri wa kwenda kuomba msamaha kwa wale uliowaletea machozi na maumivu bila hatia.
#FoungPH
WATOTO,wanunulieni wazazi wenu nguo ikiwa mna uwezo. Ikishindikana wapeni hata nguo zenu nzuri ambazo hamzivai. Kwenu zinaweza kuwa nguo za ziada lakini kwao zinaweza kuwa ishara kubwa ya upendo na kuthaminiwa.
#FoungPH
Karne hii imefika mahali ambapo kupoteza INTERNET kwa saa chache kunaleta taharuki kubwa kuliko kupoteza marafiki kwa miezi kadhaa. Tumeunganisha maisha yetu kwenye mtandao kiasi kwamba kukatika kwake huhisi kama kukatika kwa sehemu ya nafsi zetu.
#FoungPH