🇷🇺🇺🇸 Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa mazungumzo yataanza saa 19:00 GMT badala ya saa 19:30.
Yote unayohitaji kujua kuhusu mkutano huu wa kihistoria👇
THREAD 🧵
1/7
I Came to the United States in 2004 ,and I have helped 7 of my relatives Japa to America and the uk including my best friend. In total we are now 12 family members.
When you are the only one with light in your family ,you are still in darkness
When I traveled to Zambia, people asked why I have a Zambian name as a Togolese( Bemba). In DRC, they wondered if I had Congolese roots for the same reason. In Angola, same thing. And every time I land in Abuja, Nigerian immigration officers insist on seeing my Nigerian passport, convinced I’m from the North and they tell me “ Farida” is a Nigerian name. Funny enough I had a long argument with a Tanzanian politician that was adamant that my first name is Tanzanian.
What surprises me most is that even some Togolese ask if “Bemba” is my marital name, because to some, it doesn’t “sound Togolese.”
But here’s the truth: nationality is not ethnicity. As long as we Africans keep seeing our colonial borders as natural identities, we’ll keep dividing ourselves, questioning and disputing each other’s origins and right to belong.
Ethnic groups stretch far beyond these borders. The Fula people live from West to East Africa. Wolof names found in Senegal are also found among the Dinka in South Sudan.
My father’s full name is Nabourema Bemba Baldet. Nabourema was a name he created in the 70s, after Togo’s dictatorship banned so-called “foreign names” while Eyadema still named his own children Faure, Ernest, Emmanuel etc after French presidents and politicians that he admired.
The name was supposed to be Na-Boureima, meaning “Grandfather Boureima,” but a clerk misspelled it. Bemba was supposed to be Bamba, but the colonial administration changed the spelling to fit their language. It’s our clan name, and my father passed it down to all his children.
The reality is, many of us carry names that were altered or miswritten to fit colonial tongues. In Senegal, Cissé becomes Sessay in Gambia. In Guinea, Diallo becomes Jallow in Sierra Leone. Touré in Togo becomes Turay in The Gambia etc.
Even the concept of a “family name” didn’t exist in many African cultures. Names came from clans, tribes and in sometimes from mothers, not just fathers as it is the case with my mother’s tribe. That’s why siblings can have different surnames in our cultures.
So I say this: let’s reclaim who we are. Let’s stop seeing these passports and nationalities as the essence of our identity. As an African, I belong everywhere on this continent. That is what defines me.
NO REFORMS NO ELECTION: Si Siasa,
Ni Falsafa ya Uasi Halali – Hii Ndio Siri Watawala Hawataki Uijue!"
Na Ukiwa Msomi Mzuri wa Historia na Pia Mfwatiliaji wa Siasa Utakua Umewai Kukutana na Hawa
Great thinkers Rousseau, Hobbes na Machiavelli. Sasa walisemaje...
‼️🇷🇺🇺🇦 The Ukrainian army has now resulted to attacking Russian civilians in Donetsk with american cluster munitions.
There is no word that can describe this but cruelty, an act of terrorism from Zelensky.
Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.
NIMETIA NIA: NITAISHIKILIA NJIA.
Historia ya Maisha yangu haitenganishwi na mapambano ya kuihubiri Haki, Kudai Uhuru wa watu na Maendeleo yao.
Mapambano hayo yamekuwa ni sehemu ya Maisha yangu, Nimeyaishi, Ninayaamini na endapo itanilazimu sana nitakuwa tayari kabisa kuyafia.
CHADEMA kimekuwa ni Chama ninachokiamini, kimenitia moyo, matumaini na kuongeza ari yangu katika mapambano hayo ya kudai haki siku zote. Nitakipenda na kukilinda Chama hiki kwasababu kimebeba matumaini yetu Watanzania wengi.
Ninayo ndoto na nimeamua kutia nia kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa, (BAVICHA) kwa Mwaka 2024/2029. Ni matumaini yangu tunakwenda kuwa na Baraza la Kikamanda zaidi na lenye mawazo mbadala kwa manufaa ya Taifa letu na Chama Chetu kwa kuuimba wimbo wa KATIBA MPYA asubuhi, mchana, jioni, usiku na asubuhi tena ya kila siku.
Lengo ni lile lile, Awamu hii tutakwenda kuhakikisha tunagusa mahali ambako hapajawahi kuguswa ili mradi tu, Tanzania iende kuwa ni eneo salama kwa kila mmoja wetu kuishi kwa amani na furaha. Hatujui mwisho wa Mapambano yetu utakuwa ni upi lakini uhakika tulionao ni kwamba Tunakwenda kusimama kwa ujasiri kabisa KUHESABIWA.
Deogratias Cosmas Mahinyila (Wakili).
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Dodoma.
28/11/2024.
(Hijra/Njiani kuelekea Kaanani)
Mkapa alinikamata mara moja. Kikwete alinikamata mara tatu. Magufuli alinikamata mara nane. Hii itakuwa mara ya pili kwa Samia kunikamata. Mara zote hizi sijawahi kutiwa hatiani & mahakama yoyote. Sijawahi kutenda kosa la jinai. Mimi ni mpigania Uhuru & Haki. Huo sio uhalifu!
UPDATES KUHUSU WITO WA POLISI
Tumejadiliana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es saalam, Jumanne Muliro pamoja na RPC wa Kinondoni Kitinkwi kuhusu tukio la kurudisha fomu yangu ya kuwania uenyekiti wa Kanda ya Pwani Dar es saalam.
Baada ya watu wangu kuandikia barua Jeshi la Polisi kuhusu maandamano ya kurudisha fomu ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.
Jeshi la Polisi lilituita kutaka kujua na kujadiliana njia tutazotumia kuandamana kutokea Manzese kuelekea Kinondoni, ofisi ya Kanda ya Pwani.
Tumekubaliana kuheshimu haki watumiaji wengine wakati tunatumia barabara za Manzese, Tandale, Mwananyamala na kumalizia Kinondoni kwa kufanyia maandamano.
Shughuli yetu na ratiba yetu ipo palepale. Kesho tarehe 05 September 2024 siku ya Alhamisi, tukutane Manzese.
Pwani yetu Kivyetuvyetu. Pwani Inogile.
Picha hii ilipigwa siku ya tarehe 28 November 2020 nikiwa katika kikao cha kamati kuu ya CHADEMA iliyokuwa imeketi Ledger Plaza, Bahari Beach Hotel,Dar es saalam. Wakati huo nilikuwa mjumbe wa Kamati Kuu kupitia katiba ya CHADEMA ibara ya 7:7:14
“Wawakilishi watano wa madiwani wawili wakiwa madiwani wa kawaida ambao Wenyeviti na Katibu wa umoja wa Madiwani ngazi ya Taifa na watatu watokane na Mwenyekiti, Katibu na Mnadhimu wa Umoja wa Mameya/Wenyeviti wa Halmashauri.”
November 28, 2020 nilimaliza kipindi cha utumishi wangu wa ujumbe wa kamati Kuu ya CHADEMA baada ya kumaliza muhula kuingia wa udiwani na ukatibu wa Mameya wa halmashauri 26 zilizokuwa zinaongozwa na CHADEMA.
Kwa muda wa miaka minne sasa nimekuwa nje ya majukumu ya kiserikali na kichama lakini nimeendelea kuwa mwanachama muaminifu na mtiifu wa CHADEMA nikiwa naongozwa vizuri na itikadi na falsafa za CHADEMA.
Nimeendelea kuwa mwanachama mtiifu kwa chama chetu na mwanachama mwenye nidhamu, utii, shukrani, subira, Jasiri, upendo kwa chama changu na wanachama wenzagu. Kwa kuwa, CHADEMA kwangu ni namna ya maisha yangu.
Wakati wote niliamini uongozi ni dhamana tu, nilibaki kuwa mwanachama mwenye imani kubwa kwa Viongozi wetu waliopo madarakani katika uzoefu na ujuzi wa kukiongoza chama chetu nyakati zote za heri na shari.
Sikuwahi kuwa na shaka kwa miaka minne hii kwa viongozi wakuu wa CHADEMA, Katibu Mkuu na sekretarieti yake. Kamati kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Sasa nimepumzika vya kutosha, naombeni majukumu mapya.
Kwa uzoefu nilionao wa miaka 19 ndani ya CHADEMA na kupitia nafasi mbalimbali nilizowahi kushika kama Mlinzi wa chama (Red brigade), kiongozi wa CHADEMA, Kiongozi Umoja wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es saalam, Mwenyekiti wa tawi la Ubungo Kisiwani, kiongozi wa kata ya Ubungo, Mwenyekiti wa Jimbo Ubungo, Mwenyekiti wa Mkoa Ubungo, na Mjumbe wa kamati kuu
Nimeona natosha na ninafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani (kanda ambayo inaunganishwa na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani) katika mchakato wa uchaguzi uliotangazwa na chama chetu wiki iliyopita.
Kanda ya Pwani yenye Jumla ya watu Millioni 10.1, Dar es saalam million 8.1 na Mkoa wa Pwani million 2 inahitaji kiongozi mwenye nguvu na uwezo mkubwa wa kushawishi wingi wa watu wa Kanda hii Kuunga mkono mabadiliko na kuondoa CCM madarakani.
Kanda yetu ya Pwani inahitaji Kiongozi mwenye uzoefu na anayefahamu changamoto za kiuchumi katika kuondoa umaskini na kuleta ustawi wa watu wa Kanda ya Pwani.
Kiongozi atakayetanguliza haki za binadamu mbele hasa haki ya kuishi kwa kuhakikisha Kanda ya Pwani inakuwa mahala salama pakuishi na kuboresha sera za ulinzi na Usalama katika usimamizi wa shughuli za vyombo vya Dola.
Kiongozi ambaye atakaye unganisha CHADEMA na Jumuiya za kimataifa na Diplomasia zenye makazi na makao makuu yake Kanda ya pwani
Kiongozi atakaye kabiliana na kasi ya ongezeko laidadi ya watu dhidi ya kasi ya ongezeko la Wanachama wa CHADEMA.
Kiongozi ambaye atakayeiwajibisha Serikali katika ukusanyaji wa kodi na matumizi ya kodi kwa kulinda thanani ya pesa katika huduma zinazotolewa na Serikali kwa watu wa Kanda ya Pwani kama elimu,Afya, miundombinu,Viwanda na biashara, kilimo,ufugaji na Uvuvi.
Mei 28,1992,Miaka 32 iliyopita, CHADEMA ilizaliwa katika Kanda ya Pwani,Mkoa wa Dar es Salaam kisha ikasambaa na kuenea Kanda zingine 9 za Tanganyika na Zanzibar.
Miaka 10 ya mwanzo ilikuwa ya usimikaji wa chama, miaka 10 ya pili ilikuwa ya uenezi na ukuaji wa chama na miaka 10 ya mwisho ni miaka kupigania uimarishaji na ungomeshaji wa chama kuanzia ngazi ya misingi hadi Taifa.Miaka 10 hii ya muongo wa nne ni miaka ya kuchukua dola la kutimiza lengo la kuanzishwa kwa chama chetu.
Miaka hii 10 katika Kanda ya Pwani yenye mikoa ya Dar ea Salaam na Pwani, naitazama mbali, chama chetu kikiwa kimefika katika misingi kila sehemu.
Kanda ya Pwani ina jumla ya Kata 235, Mitaa 643, Vijiji 434,Vitongoji vya mamlaka ya Mji Mdogo 226, Majimbo 19. Matamanio yangu ni kuona chama chetu kinakwenda kushinda maeneo hayo yote.
Wagombea wenye sifa tunao,Wapiga kura tunao,Sababu za kupigiwa Kura tunazo na nguvu za kulinda kura pia tunazo.
Kama chama kilivyozaliwa Kanda ya Pwani kisha kikakua na kuenea Kanda zingine zote.
Kanda ya Pwani sasa ina wajibu mkubwa wa kuongoza tena zoezi na vuguvugu la kuiondoa CCM madarakani kwa kuhakikisha wingi wa idadi ya wakazi wa Kanda ya pwani unageuka kuwa ndiyo wingi wa kura wakati wa chaguzi zote.
Makusanyo ya kodi Kariakoo kwa siku ni mara 20 ya makusanyo ya kodi Jiji la Dodoma ambao wanakusanya Sh148.89 milioni. Kariakoo ni kitovu cha biashara Tanzania.
Julai-Disemba 2021. Jiji la Dodoma lilikusanya Sh26.8bn. Manispaa ya Kinondoni ilikusanya Sh24.8bn. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilikusanya Sh36.2bn.
Wakati mapato yaliyokusanywa na (TRA) mwaka 2022/2023 yakiongezeka kufika Sh23.658 trilioni, takwimu zinaonyesha Dar es Salaam inaibeba maeneo mengine.
Ripoti ya Uchumi wa Kanda iliyotolewa na Benki Kuu (BoT) 2022/23 inaonesha Dar es Salaam pekee ilikusanya Sh20.45 trilioni. Kinachobaki kinatoka kanda nyingine.
Mapato ya Dar es Salaam ya Sh20.45 trilioni, Kariakoo imevunja rekodi kwa kukusanya Sh40.8 bilioni sawa na 102% kwa mwaka. Wastani wa Sh3 bilioni kila mwezi.
Kwanini takwimu hizi? najaribu kuwaonesha ni kwa kiwango gani Dar es Salaam ni kitovu cha uchumi cha Tanzania. Hii Dar es Salaam ipo ndani ya kanda ya Pwani.
Tunapokwenda kuongoza kanda ya Pwani, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 na uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 lazima tuone mkakati muhimu wa kuikomboa Dar es Salaam, wananchi wanufaike na sera nzuri za uchumi za CHADEMA.
Dar es Salaam ni tajiri kwa uchumi wake na mapato yake yanatakiwa kurandana na maendeleo ya jamii. Kwa kuwa lengo la CHADEMA ni kushinda chaguzi na kuunda Serikali, hili litakuwa moja ya jukumu langu wakati wote. Uchumi ni kipaumbele.
Nchi yetu kwa wakati huu ipo katika matatizo makubwa ya Kiuchumi,Kuongezeka kwa umasikini,ukosefu wa ajira,ongezeko la deni la Taifa,kuongezeka kwa wizi,ufisadi na ubadhilifu wa fedha za umma pamoja na tishio la kiusalama kufuatia kuongezeka kwa wimbi la matukio ya utekaji ,mauaji na ongezeko la watu kupotea.
Kukaa kimya na kuishi bila majukumu ya kisiasa wakati huu wa matatizo yote haya ni sawa kabisa na mtu aliyeamua kuuunga juhudi Chama tawala (CCM)
Hivyo basi mimi Boniface Jacob nipo tayari kuongoza zoezi hili kwa sababu nipo tayari, katika uchaguzi huu natarajia kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa Kanda ya Pwani.
Eeeh Mwenyezi Mungu nisaidie.
Boniface Jacob
Ex-Mayor (Mjumbe wa Kamati Kuu mstaafu)
The voice of the silenced Majority.
[email protected]
0712 239 595
ADUI WA MWANAMKE NI MWANAMKE MWENZIE.....!
Nimekumbuka msemo wa Mama yangu,kuhusu Wanawake wasivyopendana na kukosa umoja hata katika maswala muhimu yanayosumbua wao kama ukatili,udhalilishaji,ubakaji dhidi ya Wanawake.
Kwamba 100% Wanawake wanaoenda maofisini iwe ofisi za umma au serikali wanapokuta mtoa huduma ni mwanamke mwenzao uwezekano wa kuhudumiwa vizuri bila shida unashuka hadi 5% au 0% kabisaa.
Asilimia 90% ya wanawake hawapendi kuhudumiwa na Wanawake wenzao mahala popote.
Hivyo hivyo katika biashara,Mwanamke anapokuta biashara anafanya na Mwanamke mwezie basi asilimia za kufanyika hiyo biashara zinashuka hadi 5% hadi 0%.
Kanuni hizi nimezikumbuka wakati huu moyo ukiwa na maumivu na majeraha makubwa ya kuona Mwanamke (mtoto wa Kike) anafanyiwa ukatili huku wenye jukumu la Kumlinda na Kumtetea ni Wanawake wenzie.
Pata picha nchi yetu Rais ni Mwanamke,Waziri wa Ulinzi ni Mwanamke,Waziri wa Jinsia ni Mwanamke, Spika wa Bunge ni Mwanamke,Kamanda wa Polisi mahala alipobakwa Binti JM ni Mwanamke pia.
Lakini uwezi amini kuwa pamoja na Kushika madaraka makubwa na kwa wingi wao ,hawana msaada wowote kwa binti JM aliye bakwa na Kulawitiwa kisha video zake zikasambazwa mitandaoni nchi nzima,
Wala hawana msaada wa mkakati wa kukomesha ubakaji na ukatili dhidi ya Wanawake wenzao kwa ujumla.
Inawezekanaje Kamanda Polisi Dodoma ambaye ni Mama na Mwanamke mwenzao anakosa uchungu wa kumsaidia binti wa Kike.
Badala yake anashiriki kuhujumu na kuharibu kesi ya Mwanamke mwenzake kwa kusema maneno mabaya na ya uongo hadharani ili binti akose msaada na kupoteza haki yake kwa tamaa ya fedha au madaraka.
1.Binti JM hakuwa anajiuza kama anavyo sema Kamanda wa Polisi bali ni binti anaye fahamika rekodi yake vizuri ,mwenendo wake vizuri, na ni binti mwenye wazazi Baba na Mama wote wa Kazi wa Dar es Salaam
2.Binti JM kwa sasa anamiaka 17 na mwaka huu angekuwa anahitimu kidato cha nne kama siyo kukatisha masomo yake akiwa kidato cha pili baada ya kushindwa kuelewa masomo darasani.
3.Binti JM akiwa na umri wa chini ya miaka 18 ,aliajiriwa na Askari wa Jeshi la Polisi ASP FATUMA KIGONDO maarufu kama "AFANDE" ambaye pia ni Mwanamke na Mama pia.
alifanya Binti JM kuwa mfanyakazi wa Bar yake inayojulikana kama THE MARION PUB,Dodoma kati ya mwezi April hadi May alipofikwa na tukio la Kubakwa.
4.Binti JM hakuwahi Kuishi Buza au Jirani na shule ya Msingi Dovya kama ambavyo kwenye Video anayobakwa anawatajia wabakaji wake sehemu anayotoka Dar es saalam huenda ilikuwa ni njia ya Kujilinda wasimsumbue zaidi.
Binti JM amewahi Kuishi na Bibi yake Mabibo Luhanga,kisha baadae kuhamia kwa mjomba wake Kiluvya Madukani Viwanja vya NSSF ,Karibu na tanki la maji la NSSF.
5.Mabinti ambao ni Wahudumu THE MARION PUB ya "Afande ASP" Fatuma Kigondo ndiyo walio mtambua Binti JM Kama mfanyakazi mwenzao ambao walikuwa wamekodiwa chumba kimoja cha kulala pale MRESHENI LODGE na Wanajua tukio lote la Binti kubakwa na kurudi Dar es Salaam lakini wakinyamaza sababu ya Vitisho.
kama kweli JM na wenzie walikuwa wanajiuza basi walikuwa wanauzwa na Afande Fatuma Kigondo.
7.kwa Mujibu wa wazazi wa Binti JM ,wanaseme Binti JM aliondoka Dar es saalam akiongozana na rafiki yake aitwaye SHADYA kwenye kutafuta kazi ya Hotel kama alivyokuwa anauza moja ya mgahawa wa chakula pale Kariakoo.
Walipoenda Dodoma hakukuta tena kazi ya Hotel bali walilazimika kuanza kufanya kazi kwa Afande Fatuma Kigondo yeye na SHADYA kutoka Mwezi April 2024 hadi mwezi May 2024 aliporudi Kiluvya,Dar es Salaam baada ya Kuugua baada ya Kubakwa na kulawitiwa.
8.May 2024,Baada ya Kukutwa na mkasa wa Kubakwa ,aliwapigia simu wazazi wake kuwajulisha kuwa anaumwa lakini hakuwaambia wazazi wake anaumwa nini.
Baada ya Wazazi kuona anaumwa muda mrefu bila kupata nafuu walimtumia Binti JM nauli aweze kurejea Dar es saalam kwa matibabu.
ambapo Binti JM alifikia kwa mjomba wake alipoluwa anaishi Kiluvya Madukani Viwanja vya NSSF jirani na tanki la NSSF ambapo alijiuguza na kupata nafuu.
Wazazi na ndugu walimuhisi kuwa ametoa mimba kwa jinsi alivyougua muda mrefu akilalamikia maumivu hasa sehemu za tumbo na sehemu zake za siri.
Wazazi na ndugu walikuja kuoanisha tukio la kuugua kwake na Kubakwa baada na wao kuona video za binti yao akibakwa na Kulawitiwa mitandaoni.
9.Katika hali ya kushangaza ni baada ya Mama na Baba wa JM kumpeleka rasmi Central Police,Dar es saalam kufungua malalamiko siku 2 baada ya kuona video zile zilizunguka mitandaoni.
1.Polisi walimbakisha JM kituoni na Kuwataka wazazi waondoke wamuache binti yao
watawasiliana watakapo hitajika,ambapo walikaa siku 3 bila kumuona wala kusikia habari za binti yao.
2.Jeshi la Polisi kwa mara ya kwanza likamtafutia makazi binti aliyebakwa na kuficha sehemu waliyompeleka ni ipi kwa maelezo ya usalama wa binti
au taasisi gani kwa maelezo kuwa ameenda kupatiwa msaada wa matibabu ya kisaikolojia.
3.Jeshi la Polisi likaipiga mkwara familia ya JM isiwasiliane na mtu yeyote kuhusu kubakwa kwa binti yao huku wakitaja Jina langu "Boniface Jacob" ambaye hapaswi kusogelea amilia ya JM.
Baadae Jeshi la Polisi likapiga marufuku ya mtu kuhoji na kuitafuta familia ya JM kwa maelezo kuwa tutaiumiza familia.
Hii inaweza Kutafsirika kama nia ovu ya kujaribu kuzuia Wanahabari,Wanaharakati na taasisi ziziso za kiserikali zinazopigania haki za binadamu na utawala bora.
Cha ajabu leo wao ndiyo wanaiumiza familia kuliko sisi wasamaria wema kwa Afisa wa ngazi ya Juu ya Jeshi la polisi kumbatiza JM jina la Malaya,changudoa ,muuza uchi binti wa miaka 17 aliyebakwa.
10.Jeshi la Polisi likatangaza kutafuta wahalifu wawili katika jalada hilo la Upelelezi wao na kuwaomba raia tuwasaidie Polisi kuwatafuta watuhumiwa hao wawili bila ya..
1.Kutaja majina ya watu wanaowatafuta ilituwasaidie kuwatafuta.
2.Kuweka Picha ya wahalifu wanaotafutwa hadharani.
Hii pia inaweza kutafsirika kama nia ovu ya Jeshi la Polisi kutaka kuwaficha wahalifu na kudanganya Jamii ione kuna watu hao wawili bado wanasakwa.
11.Kitendo cha Kamanda wa Jeshi la Polisi kusema binti alitebakwa alikuwa anafanya biashara ya Kujiuza mwili wake,nina kitafsiri kama nia ovu ya Jeshi la Polisi katika kupoteza haki za Binti JM
Kwa kutumia mbinu ya "Ukitaka kumuua Mbwa basi mpe Jina baya."
Nimitarajia kuona Kesi hii Wanawake wote Tanzania wanaungana Kumtetea Binti JM na kujakikisha haki inatendeka kama sehemu ya Kulinda wanawake wengine dhidi ya ubakaji na udhalilishaji.
Boniface Jacob
Ex-Mayor
The voice of the silenced Majority.
SIYO RAHISI NA HAIWEZEKANI KUWA JAMBO LA SIRI...!
Nimeona mjadala wa kuhusu kurejea kwa Wabunge 19 waliofukuzwa uanachama wa CHADEMA Kurejea tena ndani ya CHADEMA.
lakini katika hali ya taharuki na sintofahamu siyo tu kwa Viongozi wakubwa wa CHADEMA bali hata viongozi wa wilaya na mikoa wa CHADEMA na wao wameonekana kushangazwa na habari hii wakiwa wameshtushwa na jambo hili.
kwamba imekuwaje wamerudi..?
Lakini pia kuna propaganda kutoka ndani na nje ya CHADEMA za kuaminisha wanachama na Wananchi kuwa akina Mdee wamesharejea tayari ndani ya CHADEMA na kwamba mchakato huo wa kuwarejesha Wabunge hao umefanywa kwa mapenzi ya baadhi ya Viongozi fulani.
USAHIHI
Kwa kumbukumbu sahihi ndani ya CHADEMA hadi wakati huu,Wabunge 19 siyo wanachama wa CHADEMA tangu walipofukuzwa tarehe 28 November 2020
Baadae Baraza kuu kubariki maamuzi hayo tarehe 11 May 2022 baada ya rufaa yao kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati kuu ya CHADEMA kutupiliwa mbali na Baraza kuu la CHADEMA.
HAIWEZEKANI KUWA RAHISI
Mchakato baada ya hapo kwa mujibu wa katiba yetu, inasema vizuri kwa uwazi kabisa kuwa,endapo wabunge hao 19 watataka kurejea tena chamani baada ya Kuomba msamaha nini kitafanyika
Katika katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 toleo la 2019, Kanuni za Chama kifungu cha 6.5.4 ina sema
"Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza Kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu ya kutaka kurejea
Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata.
Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza kuu.
Watakaofukuzwa na Mkutano mkuu hawatokuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uwamuzi huo..".
Tafsiri yake ni kuwa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama; wabunge 19 wanatakiwa kurudi kwenye Kamati Kuu mmmoja mmoja au kwa pamoja kwa kuandika barua/maandishi kuomba kurejea kwenye Chama
Baadae Baraza Kuu kufanya uamuzi wa mwisho juu ya maombi hayo. Wala siyo kwa utashi wa kiongozi mmoja kama Mbowe,Lissu au Mnyika
HAIWEZEKANI KUWA SIRI
Baada ya mchakato huo mgumu wa Kikatiba ,Kamati Kuu inapaswa Kuitisha Baraza kuu au Kupeleka ajenda hiyo mbale ya Baraza kuu lenye wajumbe 423
Katiba ya CHADEMA ibara ya 7.7.11 inataja wajumbe hao 423 wote kwa nafsi zo ndani ya chama (a)Wajumbe wote wa Kamati Kuu (b) Makamu Mwenyekiti wa Kanda (c) Makatibu wa Kanda (d)Watunza Hazina wa Kanda (e) Wenyeviti wa Mikoa (f) Makatibu wa mikoa (g)Wajumbe Sita wa kuteuliwa na Mwenyekiti Taifa (h) Wajumbe watano wanaochagukiwa na Mkutano Mkuu wa Kila Baraza (i) Wenyeviti wa Wilaya (j) Makatibu wa wilaya.
Hawa ndiyo wanaofanya maamuzi ya Baraza kuu,ambapo kama kweli swala la Wabunge 19 lipo,maana yake wao ndiyo wangekaa kuwasamehe au kuwarejesha chamani
Lakini cha ajabu Wajumbe wa Kamati Kuu wanashangaa,Wajumbe wa Baraza kuu wanashangaa na wao wanatuuliza sisi wanachama kama ni kweli Wabunge 19 wamerejea CHADEMA
Wamesahau maamuzi ya mwisho kuhusu kuwafukuza wale wabunge 19 walifanya wao na kama siku wanatakiwa kurejeshwa maamuzi watafanya wao tena au kama kuwakatalia maombi ya kuwarejesha basi maamuzi hayo watafanya wao.
HALI HALISI YA WABUNGE 19
Kwa sasa wabunge 19 hawana mtizamo na msimamo wa pamoja juu ya hatima zao kisiasa wamegawanyika wala hawapo tena pamoja kama mwanzo
1.Kundi la kwanza limeshafanya maamuzi ya kuelekea CCM,Kwa maneno yao hadharani, kwa kuvaa sare za CCM na kushiriki vikao na mikutano ya CCM
Hapa wapo Nusrat Hanje,Jessa Kishoa,Esther Matiko,Hawa Bananga na wengine
Sidhani kama hawa wanafikiri au wameshawahi Kuwaza kurejea CHADEMA
2.Kundi la Pili ni Wabunge ambao waliteuliwa kuwa ktk orodha ya Wabunge 19 lakini siyo maarufu wala hawana majina makubwa ya kisiasa
Hawa wameenda kuvuna pesa za bure na wanajua baada ya hapo siasa haiwadai,wala wao hawaidai
3.Kundi la Mwisho ni wachache wasiozidi wanne wanaotamani kurejea CHADEMA,wana ukaribu na mawasiliano na baadhi wanachama wa CHADEMA
Wanafuatilia kila kitu kinachohusu CHADEMA
Lakini wamekuwa wazito kufuata taratibu za hizo za CHADEMA
kwa mfano,sharti la CHADEMA la kuwataka Kujivua Ubunge huo haramu, kisha kuomba msamaha Baraza Kuu kama katiba inavyotaka.
Ili Baraza kuu liamue maombi yao juu ya kukataliwa au Kukubaliwa au kupewa masharti,mfano ya kuwarejesha CHADEMA kama Wanachama tu bila kupewa nafasi za uongozi tena kwa kipindi fulani kwa kadiri wajumbe watakavyo inafaa au kuamua kikaoni.
Je kwa kichwa cha Habari cha gazeti la Mwananchi kusema safari ya kina Mdee na wenzie kurejea nyumbani ipo kweli ...?
kama mpaka sasa hawajaandika barua au maandishi juu ya kuomba msamaha na kurejea CHADEMA..?
Boniface Jacob
Ex-Mayor
Mjumbe wa Kamati Kuu mstaafu.
0712 239 595
Mchango Update Latest: Nilitoa update mara ya mwisho tarehe 13 Juni. Naomba radhi kwa kuwachelewesha sana. Hadi kufikia tarehe 31 Julai, takriban miezi miwili & nusu, mchango umefikia sh. 104,081,139 kutoka kwa wachangiaji 3,540. Wastani ni sh. 29,401 kwa mchangiaji. Nawashukuru!