Sambamba na mambo mengine, katika hotuba yangu ya kulifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nimevielekeza vyombo vya sheria hasa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwafutia makosa vijana na watoto wetu ambao kwa kutokujua, walifanya makosa kwa kufuata mkumbo Oktoba 29 mwaka huu.
Nikiwa Mama na Mlezi, ninawasihi vijana wote kuendelea kulinda amani na mshikamano wa nchi yetu, na hata siku moja msikubali kushawishiwa kuichoma nchi yenu wenyewe.

Ahsanteni sana wananchi wa Ilemela na Nyamagana kwa ukarimu na ushiriki mkubwa katika kampeni za Urais za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kama ilivyo kote nchini tulipopita, kujitokeza kwenu kwa wingi katika mikutano yetu ya kampeni ni ishara ya ukubwa wa imani yenu kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kazi iliyofanyika na inayofanyika. Imani hii inatukumbusha sote sehemu na jukumu muhimu la Chama Cha Mapinduzi kwa mustakabali wa nchi yetu. Wingi wenu pia ni ujumbe wa matumaini makubwa mliyonayo kwa kazi inayokwenda kufanyika, mara baada ya kupata ridhaa yenu Oktoba 29.
Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha mfano wa kuwapigia kura Wagombea wa Chama hicho mara baada ya kuhutubia wananchi wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa Mwanza mjini katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, mkoani Mwanza tarehe 08 Oktoba, 2025.
#PICHA Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 22 2025 amepata mapokezi makubwa katika Viwanja vya CCM Tunduru-Nanjoka ikiwa ni mkutano wake mwingine wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Octoba 2025.
Ahsanteni sana Ruvuma.
Mmetukirimu, mmetusikiliza na kutupa heshima na ahadi kubwa ifikapo Oktoba 29. Tutaendelea kufanya kazi vyema na kwa mafanikio zaidi ili tuzidi kusonga mbele.
Nakapanya mmehitimisha kwa kishindo kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Urais kwa Mkoa wa Ruvuma. Ninawashukuru sana kwa sala, dua na baraka zenu tunapoelekea mkoani Mtwara na mikoa mingine kuzungumza na wananchi.