Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.
Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.
Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.
Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.
Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.
Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.
Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.
Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha. Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.
“You don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”
Thank you !!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 26, 2026
Last time tuliishia part 276 so leo tunaendelea na -;
Part 277
Mwenyekiti ameingia tayari Mahakamani akiwa vibe.
Amesema naona wameanza kunyoana wenyewe.
Watu 😂😂😂
Amewaona akina Mzee Lwaitama na Jenerali Ulimwengu anasema nyie Wazee hamjakata moto kama wale wazee wengine.
Amemuona Makamu Mwenyekiti Heche anasema Makamu ongeza kupeleka moto.
Tunawaona mashahidi watatu wa Mh. Lissu wapo hapa Mahakamani, John Heche, John Mnyika na Amani Golugwa.
Majaji wameingia tayari muda huu. Na wakati anaingia watu walikuwa wanaimba mtetezi wa wanyonge kwa sauti na kwa vibe.
Nimemuona anaongea na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Wakilli Mahinyila anamuuliza mmeshaandaa mashahidi tayari. Anamjibu kitu anasema haya leo tutamaliza hakuna shida.
Inapigwa high court
Wanaingia Majaji na kukaa sehemu yao.
Anasimama karani Criminal session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Lissu.
Anasimama Ajuaye Zengeli wakili wa serikali yupo na Katuga, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa kikundi chote kinaiwakilisha Jamhuri na Lissu yupo anajiwakilisha mwenyewe.
Waheshimiwa majaji na mimi niko tayari anajibu Lissu. Na mashahidi wangu wako humu naomba watoke ila wasikae mbali.
Majaji wanateta na kucheka kidogo. Makamu Heche, Mnyika, Golugwa na Brenda wanatoka zao nje.
Watu wanajiset kwenye viti vyao hapo wanakaaa.
Majaji wanateta kidogo kisha wanasema tuendeleee.
Mhe. Lissu anasema haitakuwa vibaya mkinikumbusha nilipoishia.
Jaji Ndunguru pale ulipomtaja Askofu Pissa.
Mhe. Lissu sasa leo nataka nijikite kwenye kesi kama ilivyowasilishwa kwenu na Upande wa Mashitaka. Ushahidi wao walivyouleta, Waheshimiwa Majaji naomba niseme utangulizi ufuatao:
1. Mashahidi walioletwa mbele yenu ni mashahidi wa aina gani na ushahidi wao unapaswa upewe uzito wa aina gani?
2. La pili nitazungumzia ushahidi wenyewe. Ushahidi uliotolewa na mashahidi hawa. Na nitaonesha hakuna kosa la Uhaini na hakuna kosa lolote la jinai kwahiyo hayo ndo mawili ya utangulizi.
Sasa nianze na la kwanza kuhusu hao mashahidi.
Wakati wa Preliminary hearing upande wa mashitaka ulileta orodha ya mashahidi 30. Ambao walisema hao ndio wataleta ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za uhaini dhidi yangu.
Upande wa mashitaka haukuleta mashahidi wote hao 30 badala yake walileta mashahidi 17 peke yake.
Hao 13 ambao hawakuletwa, hawakuletwa kwasababu muhimu fulani na nitazisema.
Hiyo ommission ya hao mashahidi 13 is neither insignificant nore without importance.
Sio kwasababu hawana maana na sio kwasababu hawana umuhimu.
Nianze na ambao waliletwa.
Katika mashahidi 17 walioletwa. Mashahidi 8 ni askari Polisi.
Mashahidi 9 waliobaki ni mashahidi wa kificho.
Mahakama haiwafahamu majina yao. Haiwafahamu kabisa, haifahamu wanaishi wapi? Haifahamu wanafanya kazi gani na haifahamu chochote zaidi ya majina ya P, P1, P2 P nini huko.
Inaweza kuwa tumekuwa nao throughout hapa kesi ikiwa inaendelea kwasababu Mahakama haiwajui na upande wa utetezi hauwajui hata kidogo.
Kwahiyo ushahidi wa hao mashahidi 9 ni ushahidi wa watu wasiojulikana na Mahakama wala utetezi, Watu pekeee wanaowajua ni waendesha mashitaka waliowaleta.
Part 278 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Mwanamume mmoja na mke wake walikwenda bustanini. Walipofika, wakamwona nyani dume akicheza kwa mapenzi makubwa na jike lake. Mke akamwambia mumewe, “Tazama, huyu ni mnyama wa kimapenzi sana.”
Baadaye wakamwona simba dume na simba jike wakiwa wametengana. Simba dume alikuwa amekaa kimya pembeni kana kwamba hamtambui kabisa simba jike. Mke akasema, “Hii ni hali ya kusikitisha sana, hakuna upendo kabisa.”
Mume akamwambia, “Tupa jiwe kwa yule simba jike, uone kitakachotokea.” Mke akatupa jiwe. Simba dume akanguruma na kusimama kumtetea simba jike.
Kisha mume akamwambia afanye hivyo hivyo kwa nyani. Alipotupa jiwe, nyani aliruka haraka, akapanda juu ya mti 🌳 na kumuacha jike wake ili kuokoa maisha yake mwenyewe.
Mume akamwambia:
“Usidanganywe na kile unachokiona kwa nje. Mara nyingi, maonesho ya mapenzi yanaweza kuwa mwonekano tu unaoficha moyo usio na upendo wa kweli. Kwa upande mwingine, wapo wanaoonekana watulivu na wasioonyesha mapenzi sana, lakini mioyo yao imejaa upendo wa dhati.”
Leo hii, tuna watu wengi wenye tabia za nyani 🙊 na wachache wenye moyo wa simba 🦁.
Unapokua unatambua jinsi amani ilivyo ya thamani kweli.
Huna haja ya kujibu kila maoni au kujiunga na kila hoja.
Wakati mwingine kuondoka ndiyo njia bora ya kujilinda.
Si kila hali inastahili muda wako wa nishati au umakini.
Usiombe pesa nyingi kwanza.
Omba uwezo mkubwa wa kuzisimamia.
1. Jenga NIDHAMU.
2. Jenga UJUZI.
3. Jenga financial literacy.
4. Jenga MIFUMO.
5. Jenga ASSETS.
Kwasababu..
Pesa nyingi mikononi mwa mtu asiyejua kuzitawala sio uhuru tena ni HATARI.
Utawala usiofuata sheria unafundisha watu kudai haki kwa nguvu…
Huyu mwalimu anafundisha Course ya PS 123: Government and Politics in Tanzania
Dola dhalimu wanamtishia, asitimize wajibu wake wa kufundisha kwa kutoa mifano halisi ya nchini kwetu. Sasa wanaingia mpaka madarasani wanapangia walimu nini wafundishe.
Sheria za Nchi yetu ziko wazi, huwezi kumshikilia mtu kituo cha polisi kwa zaidi ya masaa 24, kama itakua zaidi ya masaa 24 basi isiwe zaidi ya masaa 48 bila mkuu wa kituo kuomba ruhusa ya mahakama.
Leo ni jambo la kawaida watu wanashikiliwa kwenye vituo vya polisi na mahabusu za polisi kwa miezi 6, 3 nawengine hata 8.
Kuna watu wanapigwa na wanakua walemavu na wanaendelea kushikiliwa.
Hivi tunavyozungumza kuna vijana wa Chaso Mbeya walikamatwa na wanashikiliwa tangu tarehe 4/7 wengine wamepigwa vibaya na kuumizwa.
Mimi nilishikiliwa kwa zaidi ya siku 21 kwenye mahabusu ya polisi nikiwa nalala kwenye sakafu.
Huu utawala dhalimu unafundisha Wananchi kwamba Nchi hii hakuna sheria ni kila mtu kujitetea.
Kwa njia kama hizi nani ataheshimu mahakama za Tanzania, wanatumia Mahakama pale tu wanapoona inaweza kuwapa kile wanachokitaka… Huyu ni mhadhili wa chuo anafanyiwa hivi, mahakama inaona jambo kama hili ambalo polisi tangia mwanzo hawakufuata sheria.
Watanzania tuungane wote, tuchangie na tujenge taasisi itakayoondoa uhuni huu kwenye Nchi yetu.
Mimi nilikuwa najua matajiri ni watu wa bahati tu.
Alafu nikaanza kuangalia wanavyotumia weekend zao.
Hiyo Siku nikagundua kitu: weekend yako ya leo ina uwezo wa kuamua hali yako ya kifedha miaka 5 ijayo.
Hizi ni tabia za weekend za watu wanaojenga utajiri wao kimya kimya:
🧵
Vitu Hivi Ni Muhimu Mwanaume Kuwa Navyo..!!
1. Passport ya Kusafiria.
2. NIDA
3. LESENI ya Udereva.
4. Mwanamke Mzuri
5. Kazi ya Kukufanya Uwe Busy.
6. Uwe na Hakiba Ya Fedha muda wote.
7. Bima ya Afya.
8. Simu Nzuri.
9. Michongo Unayoiskilizia.
Ni Muhimu sana Ili Mambo Yako Yaende Vizuri.
Inawezekana mtuhumiwa kutoroka kituo cha polisi?
Naitwa Batuli Selemani Kiberenge, Mwalimu wa shule ya sekondari Mirijo na mkazi wa kijiji cha Mrijo wilaya ya Chemba. Mnamo tarehe 2 Julai 2026 binti yangu mwenye umri wa miaka 8 (jina nalihifadhi ili kulinda faragha yake), mwanafunzi wa darasa la 4 shule ya msingi Sanzawa, alitekwa na kisha kubakwa na kutelekezwa akiwa katika maumivu makali sana.
Tulimpeleka kituo cha Afya Mrijo kwa ajili ya matibabu. Taarifa ya daktari ikathibitisha kuwa binti yangu amebakwa. Tuliripoti tukio hilo kituo cha polisi Mrijo na kufunguliwa jalada RB/MRJ/364/2026 na msako wa kumtafuta mtuhumiwa ukaanza. Mtuhumiwa anaitwa Abdul Yassin, mkazi wa Mrijo wilaya ya Chemba. Kwa kushirikiana na wananchi, tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa tarehe 3 Julai 2026.
Mtuhumiwa alifikishwa kituo cha polisi Mrijo, ili hatua nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa. Kwa kuwa ushahidi ulikuwa wa kujitosheleza, mtuhumiwa alitakiwa kupelekwa Mahakamani jana tarehe 06 Julai 2026. Lakini katika hali ya kushangaza, hakufikishwa mahakamani na polisi walipoulizwa walidai kwamba alitoroka akiwa kituoni.
Najiuliza mtuhumiwa anawezaje kutoroka akiwa kituo cha polisi chenye ulinzi mkali wa askari wenye silaha? Tena Mtuhumiwa wa kesi kubwa kama hii? Na kwa nini atoroke siku ya kupelekwa mahakamani? Sijaridhika na maelezo ya polisi. Naomba unisaidie kupaza sauti ili haki ya mwanangu ipatikane.!
MADINI huchimbwa na huchimbwa kwa gharama kubwa. Na gharama hizo ni:-
1. Muda
2. Fedha
3. Kujifunza
4. Kupoteza
5. Kuvumilia
6. Kupambania
Hayo mambo huleta kitu kinaitwa EXPERIENCE! Ambapo mtu akishea Experience huitwa MADINI
Usione mtu anaongea MADINI, Ujue AMEKULA GHARAMA!
Siku kama ya LEO 24.06.2024 ndio mwanangu alianza kunisaka mtaa kwa mtaa, mitandaoni kushirikiana na watanzania bila kuchoka.
Familia ilibidi isafiri kutoka MBEYA kuja Kuweka kambi Dar kwaajili ya misako ya usiku na mchana, bila kusahau maombi ya KUFUNGA NA KUOMBA kwa pamoja.
Wazazi na watanzania mlijua kunipambania, leo ni miaka miwili na haya yote yapo bado kichwani mwangu na sitamani yajirudie, ndiomaana nakuwa mkali sana kuhusi UTEKAJI maana najua familia zinateseka kwa kiasi gani.
Leo vijana tumeamua kufanya hili dogo kwa wazazi, kama kuwapa FARAJA za mapambano yote waliyoyafanya kwetu.
Zamani hizi zilikuwa NDOTO, leo ni maisha ya kweli tunayoyaishi—ASANTE MUNGU hata kwa hii nafasi.
S/o kwa mwanangu JAMES (Taivina) kwa kuendelea kuwepo kwenye maisha yangu, wewe ni tafsiri ya NDUGU.
TUISHI.🫡