nikuelezayo ni machache, ninayo mengi kadhalika/
ninaye muamini yuko hai sio story za kusadikika/
kwenye kiganja cha mkono wake ameniandika/
mimi ndo yule ninaye mu inspire mpaka inspirational speaker/
#usiniitemlokoleniitewakristo#wakristo
unaweza kujua kupika, na usiwe na jiko/
unaweza kujua kuandika, na usiyajue maandiko/
fukuza ujinga kwa kutafuta maarifa/
usipoziba hufa utajenga huo ukuta/
#usiniitemlokoleniitewakristo#wakristo
mini tai sio kuku/
sio najidai kama nawe ni tai basi njo huku/
niliyenae yuko hai, ndio mana sijishuku/
ye ni mti, mi ni tawi, kunyauka marufuku/
kwasababu mizizi imezama mwambani/
kwa mbawa hizi ninapa angani/
sio kwa ujuzi wa kupanda mnazi/
kwa uzuri wa kupanda kazi/
#wakristo
kuwa na imani, ni kuwa na uhakika/
sasa wewe unayo imani alafu una bahatisha/
jaribu kidogo tu unatabika/
unatumia uongo mwingi ili kupata sifa/
#Wakristo