Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuna hitilafu imejitokeza katika Gridi ya Taifa leo December 08, 2023 saa 04:14 asubuhi na kupelekea Mikoa inayopata umeme kutoka katika Gridi ya Taifa kukosa umeme.
TANESCO imesema “Hitilafu hiyo imetokana na kusombwa na maji nguzo kubwa za kusafirisha umeme kutoka katika Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III eneo la Mto Gide, Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam”
“Umeme kwa sasa umeanza kurejea kwa awamu katika Mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha Mikoa yote inapata umeme mapema iwezekanavyo, jitihadi nyingine zinazofanywa na Shirika ni kuhakikisha miundombinu iliyoharibika inajengwa ndani ya muda mfupi, kuruhusu kusafirisha umeme unaokosekana katika Gridi ya Taifa kutoka Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III”
“Shirika linawaomba radhi kwa kwa usumbufu uliojitokeza, na litaendelea kutoa taarifa za hali ya upatikanaji wa umeme kwa kadri hali itavyozidi kuimarika”
#MillardAyoUPDATES
Ni huzuni kwa rafiki,ndugu na jamaa.Nimeumia.Ulikuwa rafiki mwenye story na utani.Sitakukuta nitakapo rudi nyumbani,najua ungetaka stori mingi,ungeanza mjomba,Namanga ulitoboa vipi ?huku John Malya akiwa anakoleza. Ingekuwa poa sana.Kwa sasa pumzika kwa amani wakili Adamu Jabir
Nawatakia Watanzania wote sherehe njema za Eid El Fitr. Tusherehekee kwa amani na utulivu huku tukiyakumbuka na kuyaenzi mafunzo mema ya Mtume wetu (SAW) na yote tuliyojifunza wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mwenyezi Mungu awe nasi daima, Inshaallah.
Eid Mubarak.