@SuluhuSamia Rais Samia, Mama yangu Kipenzi hongera kwa kuimarisha diplomasia ya uchumi. Mradi wa nishati Tanga utachochea ukuaji wa uchumi. Hongera pia Rais Museveni kwa makubaliano na ushirikiano huu, wewe ni zaidi ya Mjomba kwangu.
Hongereni sana.
Ikulu, Dar es Salaam
Nikiwa nimeambatana na Kaka yangu, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni, tumeshuhudia nchi zetu, kwa kushirikiana na Kampuni ya Vitol ya Ufalme wa Bahrain, zikisaini Hati ya Makubaliano ya Mapendekezo ya Kuendeleza Jiji la Tanga kuwa Kituo cha Nishati cha Kikanda. Ninamshukuru Mheshimiwa Rais Museveni kwa ushirikiano unaoendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Uganda na kuleta manufaa kwa wananchi wa nchi zetu.
Mradi huu ni sehemu ya dhamira yetu ya kuongeza thamani rasilimali zetu na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi. Utekelezaji wake utapanua fursa za ajira na uwekezaji, kuwezesha wananchi kunufaika zaidi na mnyororo wa thamani wa sekta ya nishati, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Uganda.
@SuluhuSamia Mkutano huu unatoa fursa nzuri ya kujadili changamoto za kiuchumi na kisiasa. Afrika inahitaji miundombinu imara ili kustahimili mabadiliko ya dunia.
Mama yangu umekuwa Mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko. Asante sana
Leo jijini Dar es Salaam nimeungana na viongozi wengine wa Afrika kufungua Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika, ambapo Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji. Jukwaa hilo, linaloadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, limekuwa sehemu muhimu ya kuunganisha mitaji, miradi na wataalamu ili kuharakisha maendeleo ya miundombinu barani Afrika.
Katika mkutano huo nimeeleza kuwa, Tanzania inashirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kuimarisha miundombinu, ikiwemo barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege. Hatua hii inachochea ukuaji endelevu wa uchumi kwa kupunguza gharama za usafirishaji, kukuza biashara, kuvutia uwekezaji, kutoa ajira na kuifanya nchi yetu kuwa kitovu cha usafirishaji.
Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kimazingira duniani, nimesisitiza umuhimu wa Afrika kuimarisha miundombinu inayohimili mabadiliko hayo na kuunganisha nchi zetu ili kuendelea kukuza biashara, uwekezaji na uongezaji thamani wa rasilimali zetu.
Julai 17, 2025 jijini Dodoma nilipozindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, nilielekeza ziandaliwe nyenzo za kuratibu, kufuatilia na kuharakisha utekelezaji wake. Leo nimezindua nyenzo hizo na kushiriki mkutano maalum wa mazungumzo na sekta binafsi, pamoja na kushuhudia utiaji saini wa Tamko la Pamoja kati ya serikali na sekta binafsi linalosisitiza uwajibikaji na ushirikiano katika kufanikisha Dira 2050.
Kwa kuwa sekta binafsi inabeba takribani asilimia 70 ya utekelezaji wa Dira, serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi, kushughulikia changamoto zilizopo na kuhakikisha malengo ya Dira yanatafsiriwa kuwa matokeo yanayogusa maisha ya wananchi.
Ninaielekeza Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji pamoja na mamlaka zote zinazohusika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Aidha, ninawasihi Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na utulivu ili kwa pamoja tuhakikishe Dira hii haibaki kuwa maono au waraka wa kisera, bali inatekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa manufaa ya Taifa letu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Baada ya kuwasili jijini Luanda, Angola kwa ziara ya kikazi, nimekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wangu, Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço.
Katika mazungumzo yetu, tumesisitiza umuhimu wa kuendeleza uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Angola. Wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika mataifa yetu yalishirikiana kufanikisha uhuru wa kisiasa; sasa ni wajibu wetu kuimarisha ushirikiano huo katika nyanja za uchumi, biashara, uwekezaji na maendeleo ya kijamii kwa manufaa ya wananchi wetu, tukitekeleza maono ya waasisi wa mataifa yetu.
Mapema leo Ikulu, jijini Dar es Salaam nimekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa mawasiliano, mashauriano na ushirikiano katika masuala muhimu yanayolihusu Taifa letu.
Mazungumzo haya ni fursa ya kubadilishana mawazo na mitazamo mbalimbali kwa maslahi mapana ya Taifa, huku tukiendelea kujenga msingi wa kuheshimiana, kuelewana na kushirikiana.
Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa kisiasa katika kulinda amani, kudumisha umoja wa kitaifa na kusukuma mbele maendeleo yenye manufaa kwa Watanzania wote.
Ninaipongeza Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars), kwa kuanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 nchini Morocco kwa ushindi dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini, (Banyana Banyana).
Ninaungana na Watanzania wote kuitakia kila la kheri Twiga Stars inapoendelea kupeperusha bendera ya Taifa letu katika michezo inayofuata. Endeleeni kupambana kwa moyo huo huo, mkionesha uzalendo, nidhamu na ari ya ushindani inayolitangaza vyema Taifa letu.
Leo jijini Arusha nimefungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali. Ninawapongeza mawakili na maafisa wa sheria wa serikali kwa kazi kubwa mnayoifanya ikiwemo kutoa misaada na kliniki za kisheria, pamoja na kutafsiri sheria kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wazielewe na wajue haki na wajibu wao, jambo ambalo ni msingi wa utawala wa sheria.
Sekta ya sheria ina nafasi kubwa katika kufanikisha utekelezaji wa Dira 2050, kwani kalamu za mawakili zikitumika vizuri zitalinda uhuru wetu, haki za raia na rasilimali zetu. Malengo yetu ni kuwa na sheria bora, mikataba imara, na taasisi zinazowajibika ili kujenga mfumo wa sheria unaoshawishi watu kujielekeza na kuchangia kwenye uchumi imara, shindani na jumuishi.
Serikali tunapoendelea kuwajengea mawakili uwezo wa kitaaluma na mazingira wezeshi, ni muhimu nao wakahakikisha taaluma yao haitumiki kwa nia ovu dhidi ya taifa letu. Chama hiki kiwe chombo cha kujenga weledi, maadili, nidhamu na ubunifu kwa maslahi ya nchi yetu.
@SuluhuSamia President Samia continues to deliver on the global stage. This visit has strengthened economic ties and opened practical avenues through direct air connectivity. Investors now have every reason to choose Tanzania, Thank you Dr. Samia.
My lovely MOM ☺️