"Njia nyingine nzuri ya kuwekeza katika maisha ni kuwatendea wema watoto wadogo. Wao huridhika na vitu vidogo, hushukuru kwa dhati, na hubaki daima na kumbukumbu ya waliowatendea wema utotoni mwao. Dua zao kwa Mungu husikika zaidi." ~Togolani Mavura.
"Dunia duara lakini usiombe ikuweke kati ikakuzunguka, au izunguke mueleko tofauti na wako. Jitahidi uwezavyo uwe nje ya mduara na uzunguke nayo." ~Togolani Mavura.
"Kujibu kunaweza kuamsha hasira zilizolala, kunaweza onyesha ujinga wako, kunaweza toa taarifa za ziada, kunaweza kukunasisha kwenye mtego, na kunaweza kuhitimisha dhana fulani watu walizonazo juu yako. Kutokujibu hakumaanishi huna majibu, bali kwaweza kuwa kipimo cha busara."
"Mwenyezi Mungu ana wakati wake sisi tuna saa na kalenda zetu. Wakati wake si masaa 24, wiki yake si ya siku 7 wala kalenda yake si ya miezi 12." ~Togolani Mavura.
"Maisha ni bundle unaishi kwa kulipunguza si kibubu kwamba unaishi kwa kuongeza. Ukishazaliwa,siku zako za kuishi haziongezeki tena bali zinapungua kutoka kwenye jumla ya siku zako za kuishi duniani.Kesho si nyongeza bali ni makato.Usihesabu zimebaki ngapi bali zimepungua ngapi."
"Kila unayemuona, hata yule mwenye tabasamu pana kiasi gani na bashasha kama zote, ana yake moyoni na kichwani ambayo kwa kimo na kipimo chake yamemuelemea. Pambana na yako usitamani ya mwenzako." ~Togolani Mavura.
"Baraka ulizopimiwa zinakutosha kwa wakati na mazingira uliyopo, ukizidishiwa zaidi ya uwezo wako kuzibeba, utaelemewa, zitakufanya uharibikiwe, ama utaishia kufanya kufuru. Zipokee na uwe na moyo wa shukrani. Mwenyezi Mungu anayetupimia ndiye anayejua stahili na kipimo chetu."
"Bila kuwasaidia wao kufika hapo ulipo, wewe hutatoka kufika kule unapopatamani kwenda. Inabidi apatikane wa kujaza nafasi yako ya sasa ili nafasi yako ya mbele ifunguke." ~Togolani Mavura.
"Katika maisha yako kuyaelekea mafanikio, watakaokuwekea vizuizi njiani ni wa kizazi chako na watu wa karibu yako ambao watatafsiri kufanikiwa kwako kama tishio kwao au kielelezo cha kufeli kwao. Ukifanikiwa, usiwakoge. Kuwa mnyenyekevu." ~Togolani Mavura.
For too long, Africa’s resources have been extracted, the value captured elsewhere, the environmental damage left behind.
No more exploitation. No more plundering.
The people of Africa must benefit - first & most - from the resources of Africa.
"Zamani tulikuwa tunasema asiyefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu. Tulipo na tuendako, asiyefunzwa na mamae atafunzwa na mitandao ya kijamii (social media). Ule ulioitwa ulimwengu wakati ule, sasa ndio Mitandao ya Kijamii." ~Togolani Mavura.
Thank you to my sister President @SuluhuSamia for the warm welcome to Tanzania and for the productive discussions.
Rwanda and Tanzania are not only neighbors but brotherly countries bound by history and a shared goal of prosperity for our people. Rwanda remains committed to building on this strong foundation by deepening our bilateral cooperation across trade, investment, infrastructure, logistics, energy, and regional integration.
I look forward to continuing our collaboration to achieve tangible results for our citizens and advance the East African Community.
Ninawatakia kila la kheri wanangu wanafunzi wa Kidato cha Sita na Vyuo vya Ualimu kwa ngazi ya Cheti na Stashahada mlioanza mitihani yenu ya kuhitimu leo. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape utulivu wa akili na afya njema ili mfanye mitihani kwa uaminifu, kujiamini na mafanikio.
Serikali inaendelea kuwaandalia mazingira mazuri kwa hatua zinazofuata ikiwemo kuongeza mikopo na ufadhili wa masomo, kujenga vyuo vikuu katika kila mkoa na vyuo vya ufundi kila wilaya, na kuboresha mitaala ili elimu iwe bora na nafuu zaidi, iwawezeshe kujiajiri na iendane na mabadiliko ya dunia.
Katika dini zetu tumefundishwa kuwa Mungu hutujaribu kupitia mali, afya, familia na watoto. Hivyo tuwe na imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu, tuvumilie na tusimame imara katika kila hali. 🤲
Leo, Ikulu jijini Dar es Salaam, nimempokea Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame, aliyewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Tanzania na Rwanda si tu ndugu na majirani, bali pia ni washirika wa kimkakati wenye uhusiano unaoendelea kukua kwa kasi. Takribani asilimia 70 ya shehena ya Rwanda inapitia katika bandari za Tanzania. Biashara kati ya nchi zetu mbili imefikia shilingi bilioni 644 mwaka 2025, na uwekezaji kutoka pande zote mbili unaendelea kuchochea ajira na ukuaji wa uchumi kwa wananchi wetu.
Katika mazungumzo yetu, tumekubaliana kuongeza kasi ya ushirikiano kwa kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi, kuimarisha biashara na uwekezaji, na kuwekeza zaidi katika miundombinu ya usafiri na usafirishaji, mawasiliano, pamoja na nishati ya uhakika. Aidha, tutaimarisha ushirikiano katika masuala ya ulinzi, usalama na ajenda za kikanda na kimataifa.
Karibu tena Tanzania, Mheshimiwa Rais.