WATANZANIA HONGERENI KWA KAZI NZURI, BADO KUNA KAZI NZITO SANA MBELE YETU..!
1. Hongereni sana kwa kazi nzuri Watanzania wote mliopaza sauti na manoendelea kupaza sauti kuhusu kubakwa, kulawitiwa na kudhalilishwa kwa binti dhidi ya askari wa JWTZ.
2.Kwa ufuatiliaji,kuhusu hatua za kinidhamu Jeshini hakuna taarifa yeyote mpya kuhusu kukamatwa kuhojiwa kwa wabakaji na walawiti, na kama tayari wameshakabidhiwa kwa Jeshi la Polisi
ili kukamilisha taratibu za kisheria ikiwemo kuwakabidhi polisi kwa mahojiano na hatimaye kuwafikisha Mahakamani.
3. Haturidhishwi na uzito na umuhimu unao onyeshwa na Jeshi la Polisi katika ufuatiliaji ,upelelezi na uwajibikaji ili kuharakisha na kulikimbiza kwa haraka jambo hili lenye maslahi ya umma.
4.Jeshi la polisi limejikita zaidi kufuatilia na kuhabarisha umma kuhusu kesi ndogo ziziso na msingi wala maslahi kwa umma huku wakishindwa kutoa taarifa kuhusu kukamatwa kwa walawiti na wabakaji
CHANGAMOTO YA HARAKA
1.Binti JM alipelekwa Kituo cha Police Central baada ya wazazi kushawishiwa na kushauriwa kuwa ndiyo wakatoe maelezo kwa jeshi la Polisi kama mlalamikaji
Baada ya Wazazi na ndugu kugundua ni binti yao ndiyo anaye onyeshwa katika video za mitandaoni akibakwa na kulawitiwa na askari
2. JM baada ya kufanyiwa ukatili huu hakuwahi kwenda kushtaki, kulalamika wala kumsimulia mtu yeyote ndani ya familia yake kwa kuhofia usalama wa maisha yake na familia yake dhidi ya watesi wake walio mtisha.
Sababu ya umaskini wa familia zetu na uelewa mdogo wa sheria,JM aliogopa akiamini anaweza kuuwawa au kubambikiwa kesi ya aina yeyote na watesi wake sababu ya uwezo wake mdogo na familia yake pia.
3.Jeshi la Polisi lilimbakiza kituoni binti JM kwa mahojiano.
Wazazi wake waliambiwa waondoke na kumuacha mikononi mwao Jeshi la Polisi kwa kile walichokiita usalama wa Binti JM
4.Mpaka jana ikiwa ni siku ya tatu ndiyo wazazi waliruhusiwa kumuona kwa muda usiozidi dakika 5,
siyo kituo cha polisi tena bali akiwa ofisi zinazosadikika kuwa ofisi za ustawi wa jamii jirani na Ofisi za makamu wa Rais,Magogoni.
akiwa hana simu yake ya mkononi wala haruhusiwi kuongea wala kuonana na Mtu mwingine.
5.Swali lina kuja JM kama muhanga wa ubajakaji na ulawiti analala wapi .? Mahabusu ya jeshi la Polisi.?
Hatuoni tunamzidishia uwoga na mateso.?
Mtoto anaweza kutengenishwa na Mama na Baba yake iwapo ukatili huo angekuwa amefanyiwa na wazazi wake.
Je kumlinda huku kwa kumtenga na wazazi wake kutaendelea hadi lini.? Mpaka kesi itakapoisha.? au milele..?
6. Kazi kubwa inatakiwa ifanyike kumlinda binti JM kumuhifadhi utu wake,kumpa msaada wa kisheria na kisaikolojia na kusimamia kesi yake hadi hapo haki itakapopatikana Mahakamani.
Natoa wito kwa taasisi za kiraia zinazohusika na haki za binadamu ,vyama vya watetezi wa haki za wanawake na Wanasheria wakujitolea kuingilia kati haraka sana kunusuru haki ya Binti JM
7.Access ya Viongozi wa CCM kama katibu wa UVCCM, Jotake Kujua alipo JM na kwenda kumtembelea na kuongea naye.
akimuhaidi kumsomesha au kumfungulia biashara kwa wakati huu ambao Jamii inasubirishwa kwamba kuna upelelezi na uchunguzi
Siyo tu kunapoteza weredi wa jeshi la polisi bali kunaondoa Imani kabisa kama jambo hili watalisimamia kwa haki
HOFU YANGU KUBWA NI..
1. Watuhumiwa wanaweza kabisa kukamatwa na serikali na kufikishwa Mahakamani ili kuridhisha Watanzania waone haki imetendeka
2. Kesi ikaja kuhujumiwa na serikali au watendaji wa serikali hao hao kwa kuja kuharibu ushahidi kwa makusudi kesi itakapofika mahakamani ili kuwanusuru askari hao wa JWTZ
3. Mnakumbuka tarehe 19 April 2024 Rais @SuluhuSamia alitengua uteuzi wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mafia Bwana Seif Ndumbo kwa tuhuma za kumbaka binti wa kazi.
4. Baadae Bwana Seif Ndumbo alifikishwa Mahakamani na kushtakiwa kesi ya jinai namba 15768/2024
5. Tarehe 26 July 2024 kesi ya Jinai namba 15768/2024 ilifutwa na kutupiliwa mbali na Mahakama ya Wilaya ya Mafia baada ya Hakimu kusema;
"Jamhuri hawakufanya juhudi zozote za kumfikisha Mahakamani Binti anayedaiwa kubakwa na Mkurugenzi kutoa ushahidi....
Na kwamba binti ambaye ndiyo muhanga hakuwahi kupatikana Mahakamani yeye au Mama yake wala ndugu zake kwa muda wote.
Hata mlalamikaji wa kesi hii alikuwa ameandikwa ni Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mafia.."
Je ni Kweli kabisa Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) alishindwa kumpata shadhidi muhimu ambaye ni kuhanga wa kubakwa kwende kutoa Ushahidi.?
Ni kweli Kabisa Mkurugenzi wa mashitaka ajui kuwa ili mshitakiwa atiwe hatiani ni lazima Shahidi muhimu alitetendewa jambo hilo la ubakwaji anakuwa shahidi muhimu na Vielelezo kama vile taarifa ya Daktari, taarifa ya Jeshi la Polisi na nyaraka kama cheti cha kuzaliwa vingetumika kama Vielelezo vya muhanga ili kutihibitisha madai ya ubakaji.
Taarifa za ndani kutoka Wilayani Mafia zinasema binti na familia yake walilipwa pesa na kiwanja kama sehemu ya fidia kwa masharti ya kuondoka Mafia kwenda kuishi mkoani Manyara na kupotea kabisa ili kesi ikose mlalamikaji na shadhidi muhimu.
6. Katika kesi hii ya Binti JM pia, kuna uwezekano mkubwa pia wa JM kushawishiwa asilalamike, asitoe ushahidi au asipatikane kuwanusuru wabakaji wake kwa makubaliano na gharama yetote kama tutamwachia kesi hii peke yake na familia yake.
"Justice delayed is justice denied.."
Boniface Jacob
Ex-Mayor
The voice of the silenced Majority
🗣️ "Maswali yamekuwa mengi kuhusu Uwanja wa Mkapa sababu siku ya mchezo dhidi ya Orlando Pirates kutakuwa na mashindano makubwa ya Quran, na inafahamika kwamba uwanja unatakiwa kuwa wazi kwa masaa 72 kabla ya mchezo"- Ahmed Ally. #NguvuMoja