Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa The Great Hall of the People kabla ya kuanza mazungumzo jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.
Tanzania is building the system everyone will eventually run into where capital, cargo and markets meet. We call it positioning.
Thank you, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026.
Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akipokea zawadi ya picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya hafla ya uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026.
Leo, nimeungana na mwenyeji wangu, Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço, kuzindua Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda.
Hospitali hiyo imepewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa heshima ya mchango wake mkubwa katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, hususan nchi za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Angola.
Heshima hii kubwa kwa Taifa letu ni kielelezo cha uhusiano wa kihistoria na urafiki wa kudumu kati ya Tanzania na Angola, uliojengwa katika mshikamano wa kupigania uhuru, na unaoendelea kuimarishwa kupitia ushirikiano wa kiuchumi kwa maendeleo ya watu wetu.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Lourenço wa Angola wazindua Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dosQueimados Presidente Julius Nyerere), Jijini Luanda, nchini Angola.
Invest in Tanzania with Confidence.
Bridge Business and Investments Consultants provides strategic advisory services to international investors seeking to establish, expand, and succeed in Tanzania.
Tanzania 🇹🇿 ×🇸🇬 Singapore
Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam atafanya Ziara ya Kitaifa nchini (Juni 8 hadi Juni 10, 2026) kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan.
Atakuwa Rais wa kwanza wa Singapore kutembelea Tanzania tangu kuanzishwa ushirikiano wa kidiplomasia mwaka 1980.
Arusha imeandika historia! Umati mkubwa wa wananchi umejitokeza kumpokea na kusikiliza Mwenezi wa CCM, jambo linalodhihirisha imani, matumaini na mwitikio mkubwa wa wananchi kwa chama na uongozi wake. Hakika sauti ya maendeleo, umoja na mshikamano inaendelea kusikika kila kona. Arusha leo imeonyesha kuwa nguvu ya wananchi ndiyo msingi wa mafanikio ya taifa letu!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladmir Putin katika Kongamano la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF’26) linalofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa ExpoForum Convention Center nje kidogo ya Jiji la St. Petersburg nchini Urusi, tarehe 05 Juni, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakishuhudia utiaji wa saini wa hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya sekta ya nishati, umeme, mafuta na gesi asilia baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Rwanda, jijini Kigali, Rwanda tarehe 19 Mei, 2026.
Upendo wa Mhe. Angellah Kairuki kwa Wananchi wa Kibamba hauna kipimo, Moyo wake wa Utu na Ubinadamu wake kwa Wananchi anafanya azidi kupendwa sana.
Fursa kwa Wananchi imekuwa nguzo yake kuu kuona Wananchi wanakuwa huru kiuchumi.
Hii ndio tafsiri ya KAZI n UTU alaf kwa pamoja Wananchi wanasonga mbele kuleta matokeo chanya mitaani.
WABUNGE WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAPINDUZI YA USAFIRI WA SGR
Mbunge wa Geita Mjini, Chacha Wambura, amesema huduma ya treni ya kisasa ya SGR imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri nchini, huku akiipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho hayo.
Akizungumza leo Jumatatu Mei 11, 2026 kwa niaba ya wabunge wenzake waliotumia usafiri wa SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa ajili ya kuendelea na vikao vya Bunge, Mhandisi Wambura amesema huduma hiyo imeongeza ufanisi wa safari na kurahisisha usafiri kwa wananchi.
Amesema tangu kuanza kwa huduma hiyo takribani miaka miwili iliyopita, Watanzania wameendelea kunufaika kwa kiwango kikubwa kutokana na ubora wa usafiri huo, akieleza kuwa mazingira na huduma zinazotolewa ndani ya treni hiyo ni za kisasa na zenye viwango vya kimataifa.
“Zamani tulikuwa tunatumia muda mrefu kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, lakini sasa ndani ya saa tatu unakuwa umefika. Haya ni mapinduzi makubwa ya usafiri ambayo yatachochea maendeleo na kukuza uchumi wa nchi,” alisema Mhandisi Wambura.
Aidha, aliipongeza Serikali kwa kuongeza idadi ya treni za SGR na kuomba jitihada ziendelee ili huduma hiyo iweze kufika katika mikoa mingine ikiwemo Mwanza na Isaka, akisisitiza kuwa usafiri huo umeendelea kuwa na tija kubwa kwa Watanzania wengi.
Leo Mei 8, 2026 nimeungana na wajumbe wenzangu katika Kikao cha Shina Namba 1 la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chamwino mkoani Dodoma kilichoitishwa na Balozi wa Shina, Bi. Paulina Mkasanga, kwa mujibu wa Ibara ya 21 na 24 ya Katiba ya CCM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.
Gwaride likipita mbele kwa mwendo wa haraka kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 kwa Mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.